CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

kweli mleta mada unatumika vibaya, kilichobaki utasema hata helmet za pikipiki utasema vifaa vya kijeshi

Endelea kijana najua ajira imekuwa ngumu ndo maana fani zinaongezeka
 
Hapa unaona nini:

attachment.php

Bado hivyo visu havijawekwa rangi za bendera za CHADEMA watuaminishe kama walivyofanya kwa CUF.....
 
Hahahahaha...

Leo hii mmeona mrudishe sera ya majambia mliyowasambaratisha Cuf? Mmenoa Mapakacha, sasa vifaa vya kijeshi viko wapi hapo nyie?

Visu na Manati? teh teh teh teh.....!! Mje na hapa nyumbani mi ninavyo vingi huwa nachinjia kuku, mbuzi nk.. kumbe ni vifaa vy kijeshi?

Duhhhhhhhh nchi hii...!!

BACK TANGANYIKA
 
Vifaa vya kijeshi VP izo buti au ayo manati at a watoto Wa shule za msingi wanamiliki na kutengeneza wenyewe kuna kitu apo kama visu ata nyumbani kwako vipo kana kwako kama amna kisu

Umeshasema nyumbani kwako tena utakuwa una maanisha vile vya kukatia nyama ambavyo kiuhalisia havipo kama hivyo vinavyoonekana katika picha.

CHADEMA mnafanya nini na hizo zana hatari ofisini!?!
 
General Election ya Tanzania inakuwa tamu kweli mda ukikaribia......I'm watching new season movies seriously
 
Kumbe Red Brigade wameiva. Kama wanaweza kulinda viongozi, wanachama,na mali za chama nchi nzima kwa kutumia manati mbili, visu viwili na vifaa vya kukinga kuumia magoti na viwiko (ambavyo hata waendesha bodaboda wanatakiwa kuvitumia kwa usalama wao).
 
Huu uzi unalivunjia heshima jeshi letu, hivi kweli unaweza kuwambia watanzania hivyo ni vifaa vya kijeshi! Walau mgekuta kabastola kama kale ka chenge kalikolipua ofisi ya Chadema bariadi. Niulize tu swali kunakifaa cha kijeshi hapo kweli? Naona mleta uzi kavurugwa na operation za Chadema nchi nzima

Hivi ile operesheni digidigi ni ya kusambaza vifaa kama hivyo au ni ya kusambaza sera zenu za majimbo na ukanda?
 
Kumbe ndio maana Jeshi letu hata kwenye 10 bora ya majeshi Africa halipo, Manati ni siraha ya jeshi la Tanzania? Visu vya kuuzia nyama ambavyo Masai wanavyo kila siku? Buti ambazo hata Shilole anavaa? Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaa, Saaaa ya ukoziiiiii imefikaaaaaaa. Hawa PoliCCM sijui wamekula Marage ya wapi hawa.
 
Hivi siku hizi MANATI pia ni silaha ya KIVITA!!!
Yaani mmekosa silaha yoyote ya maana ku-support propaganda yenu mnakuja na MANATI!!!!!!!!!!!!!!!!!???????



Yaani mwaka huu CCM mtakuja mpaka na nyimbo gani sijui ndio mueleweke!!!!


CCM, Novemba 2015 TUNAKUZIKA RASMI hata utapetape vipi!!!!
 
.... Hahahahahaha, Hatudanganyiki, Tafuteni Mbinu Nyingine
 
Hii mbinu si ilishafeli kwa cuf, make naona visu vya mahita vilivyobadilishwa nembo.
 
Hivyo Vifaa Si Hata Nyumbani kwangu ninavyo, kumbe vinapindua nchi???

*
Kweli akili za Vijana wa Lumumba na michepuko yao ACT ni kama Pipa na Mfuniko.....
 
Sijaona vifaa vya kijeshi hapo, nilitarajia kukuta MG, LMG, RPG, mabomu ya kutega ardhini na ya kutupa, kifaru nk, ninachokiona hapo ni nguo za mitumba za mtaa wa kongo wanazovyaa wasanii huko marekani na buti za migodini...teteteh....kama hizo ndo taarifa za kiinterejensia tutashuhudia mengi mwaka huu

Hivyo vitu ni njama za kuichafua Chadema maana ndiyo chama tishio kwa chama cha mafisadi(ccm), Polisiccm wamekusanya bendera za chadema, vifaa vyao na visu wajavipiga picha pamoja na watu feki ili wazitumie picha hizo kuichafua chadema. Usishangae huko mbeleni zitawekwa picha zenye bendera za chadema, bunduki za kivita na hata milipuko yote ni kuwaamanisha wananchi kuwa Chadema ni hatari. Lakini ccm pamoja na polisi wanashindwa kuelewa kuwa Mungu akisema Yes hakuna wakusema no. Angalia Mandela vikwazo alivyopitia, wana wa Israel kule Misri n.k Chadema itapitia mambo magumu lakini itashinda zidi ya mipango ya hila ya dola na chama tawala. Mungu yupo pamoja na wanaonyanyaswa, wanaoteswa lakini hawezi kuwa upande wa wanaonyanyasa na kutesa na kusingizia wengine.
 
Ccm ndiyo itakayoanzisha vita Tanzania.

Hawa polisi, wanatumia ni ni kufikiri, baada ya uharibifu wote huu uliofanywa na ccm kw ataifa, bado wanakubali kutumika kwa hila ili kuendelea kukubali kuwa mamluki wa ccm bila kujaili maisha yao yalivyo duni, mazingira hatarishi wanayofanyia kazi, ndugu zao na wao wanavyopoteza maisha kama sisimizi, na namna ambavyo hata watoto wanaowazaa hawajui wataishi namna gani?

By the way, silaha za kivita hapo ni vipi?

Labda wangekwenda na milipuko kama ile waliyoikuta mskitini morogoro ila hii ya chadema iwe na rangi za chamadema.

Ccm huu ndio mwisho wenu. Wtanzania tunazidi kuwafahamu nini ni viumbe aina gani. Hapa hamvuki nimewaambia!.
 
Ukienda taasisi yoyote utakuta walinzi mchana hawana silaha usiku wana silaha ikiwemo visu tena vikubwa tu yani sime manati ,rungu, nondo nk. Hata majumbani mwetu ukija uvunguni kwangu utakutana na panga kali sana na rungu na ukivamia lazima ukutane na hizo silaha zikiwa active. Nenda hata shule za msingi za serekali utakuta walinzi wakiwa na silaha kama hizo .This is 2015 mambo ya 1995 hayawezi kupata nafasi tumeshatoka gizani tupo kwenye mwanga
 
Mkuu, wanaweweseka mbaya. Yaani manati na visu ndo vifaa vya kijeshi? Kama polisi wanakubali kutumiwa hivo na ccm basi kama nchi tunayo hali mbaya. Yale yale ya visu vya CUF ambavyo Mahita alikuja kukiri kuwa walifanya tu uhuni.
 
Back
Top Bottom