CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

Nilijua tu ... kuwa sare za kijeshi na silaha zitakuwa ni hizo nguo za mitumba na manati. Hii nchi bwana, inahitaji wanasheria shupavu kwa wingi sana ...
 
Ndio madhara ya chama kuongozwa na mtu mwenye intelligence ndogo, Mbowe should be careful with what he is doing because he is going to cost CHADEMA the votes.
Dada kuandika kwa lugha ya kiingereza hakukusaidii wewe kuonekena msomi! Ona sasa umejifedhehesha kwa kuandika kiingereza kibovu kupita kiasi! kwa wenye lugha yao hata hawakuelewi ulitaka kusema nini! pole sana limbukeni wewe.
 
Wakuu nimeona leo nishee nanyi hapa jamvini tena kuhusu sakata la makada wa CHADEMA waliokamatwa na zilisomemwa kuwa silaha za kivita ambazo ni manati 1,visu vidogo 2,na mawe 40 pamoja na mavazi yanayofanana na ya jeshi na mabuti yake.

Linalonisukuma leo kujadili pamoja nanyi siyo suala la CHADEMA kuonewa au hawajaonewa, la hasha leo naongea katika picha ambayo yawezekana CHADEMA kukutwa na vifaa hivyo ilikuwa sawa?

RPC Msangi kuja navyo hadharani badala ya OCD wa wilaya ya Momba kuvionesha vitu hivyo lilikuwa ni sahihi?

Suala limekuwa tofauti miongoni mwa jamii kutokana na uhusika wake RPC Msangi kwenye manati hizo.Yumkini jamii isingeona kama leo inavyoona kuwa ni propaganda na kuchafua taswila ya CHADEMA tu badala ya jamii kuona ni kesi kama jinai nyingine.

Hii ni kutokana na historia ya RPC MSANGI mwenyewe

1. Alipo kuwa RCO wa mkoa wa Morogoro alikuwa anafahamika "mzee wa kuuza MURDER CASE,"Kwa watu mbali mbali ambao alikuwa haelewani nao basi wengi walifunguliwa kesi za mauaji.

2. Kuhusishwa kwake katika suala la kumtesa DK.Ulimboka na hata kutambuliwa alipoingia Muhimbili akiwa ni ZRCO na Dk. Ulimboka mwenyewe.Kumemfanya kuonekana ni polisi aliyekuwa akitumiwa visivyo na Dola.

3. Kutajwa kwake na Dk. Reginald Mengi katika kuhusika kwake katika njama za kutaka kumtega na kumuwekea mtoto wa Mengi madawa ya kulevya na hata alipotajwa na mzee Mengi ITV aliishia kubadilishwa kituo kutoka Kanda Maalum ya DSM na kwenda kuula u-RPC Mbeya.

4. Historia yake mbaya wakati wa sakata la Wilfred Lwakatare wakati wa kesi yake ya ugaidi. Yeye ndiye alioenekana kufurahi zaidi na kushabikia kesi ile kiasi cha kwamba mawakili waliingilia kati apelekwe mahakamani tofauti na RPC Msangi (ZRCO) alivyokuwa nataka Lwakatare aendelee kusota pale Central kwa zaidi ya wiki moja.

5. RPC Msangi akiwa ZRCO ndiye aliyeendesha zoezi la kukamatwa kwa mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni FRERMAN AIKAEL MBOWE na kumshikilia kwa order ya mahakama ili kumrudisha Arusha kwa gharama kubwa za ndege ya kivita wakati wangeweza kumwambia Mbowe aende Arusha kujisalimisha.

Haya yote niliyoyataja ni machache tu miongoni mwa yale yanayofanya suala la kukamata manati lipuuzwe.
 
Duh!!!maajabu haya kwa Tanzania kisu na manati ya kuwinda ndege imekuwa silaha kali za kijeshi,hahahaha only in Tanzania!!
 
Kwa hiyo hizo nguo ni za Kujinyongea au? hivyo visu mbona ni vya kawaida sana hata mimi ninavyo!!
 
attachment.php
 
Mkuu asanusye Bwana Msangi ni aina ya askari wasiofaa kuwemo katika jeshi la polisi.

Namkumbuka Msangi wkati huo akihudumu kituo cha polisi USA River Arusha alitaka kumbambikia kesi ya mauaji mtoto wa mjomba wangu kwasababu alikuwa akipigania haki ya shamba lake liliko maji ya chai.Mbaya zaidi aliyekuwa akimkingia kifua alikuwa mwanamke mmoja ambaye ilikuja kujulikana alikuwa rafiki yake wa karibu sana.

Nilikwenda kwa RPC wakati huo jina limenitoka akaitwa ofisini na kuulizwa maswali akaambiwa afute hiyo kesi mara moja na asirudie tena kubambikia watu wasiohusika kesi.

Niliposikia kawa RCO na sasa RPC nikajua mmasai akaingia disco na sime na mkuki sijui kama kuna kukalika.Nchi hii unaweza kushangaa sana watu wahovyo ndio wanapewa dhamana kubwa.Msangi kama Msangi hakustahili uRPC kama maadili yangekuwa yanafuatwa.

Wakuu nimeona leo nishee nanyi hapa jamvini tena kuhusu.sakata la makada wa chadema walio kamatwa na zilisomemwa kuwa silaa za kivita ambazo ni mati 1,visu vidogo 2,na mawe 40......pamoja na mavazi yananana na ya jeshi na mabuti yake
Linalo nisukuma leo kujadili pamoja nanyi siyo swala la chadema kuonewa au hawajaonewa.la hasha leo naongea katika picha ambayo yawezekana chadema kukutwa na vifaa hivyo ilikuwa sawa je? RPC msangi kuja navyo hadharani badala ya OCD WA WILAYA YA MOMBA KUVIONYESHA VITU HIVYO lilikuwa ni sahihi?
Swala limekuwa tofauti miongoni mwa jamii kutokana na uhusika wake RPC msangi kwenye manati hizo.yumkini jamii isingeona kama leo inavyoona kuwa ni propaganda na kuchafua taswila ya chadema tuh badala ya jamii kuona ni kesi kama jinai zingine.hiii nikutokana na historia ya RPC MSANGI mwenyewe
1.alipo kuwa RCO wa mkoa wa morogoro alikuwa anafahamika "mzee wa kuuza MURDER CASE,"Kwa watu mbali mbali ambao alikuwa haelewani nao basi wengi walifunguliwa kesi za mauaji.
2.kuhusishwa kwake katika swala la kumtesa DK.ULIMBOKA na hata kutambuliwa alipo ingia mhimbili akwa ni ZRCO na Dk.ulimboka mwenyewe.kumemfanya kuonekana ni polisi aliye kuwa akitumila visivyo na Dola.
3.Kutajwa kwake na Dk.Reginald Mengi.katika kuhusika kwake katika njama za kutaka kumtega na kumuwekea mtoto wa Mengi madawa ya kulevya.....na hata alipotajwa na mzee mengi ITV aliishia kubadilisjwa kituo kutoka kanda maalumu ya DSM na kwenda kuula u RPC mbeya.
4.ni historia yake mbaya wakati wa sakata la Wilfred Lwakatare wakati wa kesi yake ya ugaidi. yeye ndiye alioenekana kufurahi zaidi na kushabikia kesi ile kiasi cha kwamba mawakili waliingilia kati apelekwe mahakamani tofauti na RPC msangi(ZRCO)alivyo kuwa nataka Lwakatare aendelee kusota pale central kwa zaidi ya wiki moja.
5.RPC msangi akiwa ZRCO ndiye aliye endesha zoezi la kukamatwa kwa mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni FRERMAN AIKAEL MBOWE.na kumshikilia kwa order ta mahakama ili kumrudisha Arusha kwa gharama kubwa za ndege ya kivita wakati wangeweza kumwambia Mbowe aende Arusha kujisalimisha....
HAYA YOTE NILIYOYATAJA NI MACHACHE TUH MIONGONI MWA YALE YANAYO FANYA SWALA LA KUKAMATA MANATI LIPUUZIWE.
 
Last edited by a moderator:
attachment.php
Intelligencia ya ACP Ahmed Msangi Na Polisi Tanzania ilishindwa kuwanasa hawa Green G...lakini imeweza kutengeneza tukio la Kisanii dhidi ya CDM
 
MANATI na MAWE ni vifaa vya jeshi gani karne hii ya 21??????ONLY IN TANZANIA
 
kama hivi vifaa ni vya kijeshi mama yangu mzazi na bibi yangu watakoma
 
Polisi hawajui hiyo propaganda aliitumia Mahita dhidi CUF sasa hivi tunaifahamu.

Kwa kweli CCM hawana jipya nimeamini yani wote wameshindwa kujua kuwa hii mbinu iliishatumika kipindi cha nyuma?
 
Hii propaganda imeshashindwa hata kabla haijaanza.

Bongo bwana hivyo visu,mabuti na nguo si vinapatikana kwenye mitumba? Au ndo mwendelezo wa kutafuta pakutokea? Kuna taarifa yoyote ya jeshi kama wamepoteza vifaa kama hivyo?
 
Kwa jinsi hii habari ilivyowekwa hapa jamvini: picha kubwa na zingine kushushwa kutoka mtandaoni, kufungwa na kisha tena kufunguliwa na mods, nilidhani kuwa leo, hii habari ya Chadema kukutwa na "silaha za kivita" itakuwa ndio habari mojawapo kuu katika magazeti ya leo. Hata hivyo katika kufuatilia kwangu katika vichwa vya mbele vya magazetini, ni gazeti moja tu la MTANZANIA ambalo limeandika habari hizo. Je! Magazeti mengine hayakupata hii habari? Au ni kwamba habari kama hizi zimezoeleka katika jamii kiasi cha kupuuzwa?
 
Kama taarifa hii ni ya kweli nadhani Mawakili wa Chama lazima wako Momba kwa kazi moja ya kuhakikisha Sheria na haki ya hawa Vijana inalindwa ,pamoja na uchafu dhidi ya Chama.

CC Kurugenzi ya Habari
 
Last edited by a moderator:
ifike pahala tuache siasa zifanywe nan wanasiasa....huku ni kudhalilisha jeshi
 
BAVICHA mna tatizo la kuchukulia mambo diplomatically hapa tupo kwenye uhuru wa habari ambapo kila mmoja ana right ya free of expression ila kwa Kuwa BAVICHA Hamko kidiplomacia ndo kitu kidogo kama hivi unajaza povu jukwaa zima badara Ya kutoa hoja yenye ustaarabu vivyo hivyo unavyokosa uvumilivu humu kwenye media ndo utakavyo act pindi utakapoachwa na vifaa vya kijeshi kwa sababu unakosa ile political tolerance na huu ni utamaduni wenu kuanzia juu mmejaa hasira kwa kila kitu.mitusi ndo kabisa nyumbani kwenu


Kwani ulitaka tukujibu vipi!!!!?
 
Subiri hao waliodakwa wabanwe.Tutajua kila kitu.

Maana hao waliodakwa wana mawili ya kuchagua ama zigo liwabakie wao na watolewe mbuzi wa kafara na CHADEMA au walirudishe hilo zigo kwa CHADEMA wenyewe wenye zigo lao kwa kueleza kila kitu ili wahusika wenyewe washughulikiwe.

Vyovyote iwavyo kuna mtu ndani ya CHADEMA saa hii atakuwa keshashikwa na tumbo la kuharisha au anataka kukimbia nchi.


Kwa kesi gani hapo unayoiona!!!?.Kwa sababu ni mambo ya kutungwa na policeccm tunawasubiria mahakamani.
 
Hivo vifaa vya kijeshi labda upambane na mateja ndo utawashinda
 
Back
Top Bottom