CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

“Tunawindwa kila kona ya nchi hii, polisi hawalali kwa ajili yetu sisi…nawaambia tutakufa nao katika hili, haturudi nyuma,” alisema Mbowe.

Hii sio kauli ya kiongozi,ni kauli ya uchochezi wa raia na polisi,ni kosa Bwana Mbowe,hapa umeenda mbali.Mauji na majeruhi huko Soweto Arusha, hiyo damu haijakutosha,nani aliyewafidia wahanga?

Kiongozi yeyote makini hawazi kuchonganisha utawala uliopo madarakan na wananchi.Sisi wote ni Watanzania na Wa-Africa,polisi ni sisi wenyewe,ni vijana,wetu,ni ndugu zetu na tumewaweka hapa kwa kutulinda sote bila ubaguzi,wala uchama.

Wewe tayari ni kiongozi ambae kwako tungetaka mfano.Hata ungekuwa raisi leo,si kweli kwamba wananchi wote,vyama vyote wangekuchagua,au wangekukubali na hiyo hasa ndio demokrasia ya kweli.Hizi kauli za namna hii ni za kichochezi,kati ya raia na raia,polisi na raia,chama na chama,hukuna hoja nyingine?Hakuna lugha nyingine?

=====================

JESHI la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu wawili wanaodaiwa kuwa makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao ni vijana wa kikosi cha ulinzi cha chama hicho (Red Brigade), wakidaiwa kuwa na sare za jeshi na silaha zikiwamo za jadi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alisema vijana hao walikamatwa juzi jioni katika eneo la Sogea wilayani Momba, baada ya kutolewa taarifa na raia wema.

Kamanda Msangi aliwataha vijana hao waliotiwa mbaroni kuwa ni Mathayo Mwafongo na Salehe Sichalwe, ambao kwa pamoja walikutwa na visu, manati, mawe ya kurushwa kwa kutumia manati, sare za jeshi na simu tatu za mkononi.

Vijana hao pia walikuwa na fulana ya Chadema, kilemba na barua tatu za kuwatambulisha kuwa wao ni wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda Kata ya Chitete, Msangano na Kamsamba wilayani Momba, kutoa mafunzo kwa vijana wa chama hicho.

Kamanda Msangi alisema kutokana na kushamiri kwa matukio ya ugaidi katika maeneo mbalimbali, jeshi la polisi limeweka ulinzi kudhibiti matukio hayo katika kila kona ya nchi.

“Kwa hiyo wakati askari wakiwa katika doria, walipata taarifa juu ya watu hao na kuzifanyia kazi,” alisema Msangi.

Alisema askari wa doria kwa kushirikiana na wananchi, waliweza kuwakamata vijana hao saa tatu asubuhi wakiwa kwenye pikipiki.

Kamanda alisema vijana hao walikamtwa eneo la Sogea, Tunduma wakiwa wamevaa mavazi meusi, wamebeba mikoba mgongoni na wakiwa wamefunika nyuso zao.

“Raia wema walifika kituoni na kutoa taarifa juu ya hofu yao kwa watu hawa ambao walikuwa wamevaa mavazi tofauti na muonekana wa watu wengine…tulivyowafuatilia tuliwakamata na walipopekuliwa walikutwa na silaha na sare za jeshi.

“Hivi sasa wanahojiwa na polisi na mamlaka nyingine kufahamu lengo la kumiliki vitu hivyo kinyume cha taratibu, baadaye watafikishwa mahakamani,” alisema Msangi.

Kamanda wa Ulinzi Chadema Nyanda za Juu Kusini, Aron Siwale alikiri kumtambua mtuhumiwa Mathayo Mwafongo huku akimkana Salehe na kusema kuwa ni dereva wa bodaboda.

MBOWE

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amedai chama chake kinawindwa na polisi kila kona.

Kauli hiyo aliitoa jana alipozungumza na MTANZANIA akisema kuwa polisi wamekuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha kikosi cha ulinzi cha Red Bregade hakifanikishi malengo yake.

“Tunawindwa kila kona ya nchi hii, polisi hawalali kwa ajili yetu sisi…nawaambia tutakufa nao katika hili, haturudi nyuma,” alisema Mbowe.

Chanzo:Mtanzania
 
Gazeti la Mtanzania tarehe 27-April-2015

“Tunawindwa kila kona ya nchi hii, polisi hawalali kwa ajili yetu sisi…nawaambia tutakufa nao katika hili, haturudi nyuma,” alisema Mbowe.

Hii sio kauli ya kiongozi,ni kauli ya uchochezi wa raia na polisi,ni kosa Bwana Mbowe,hapa umeenda mbali.Mauji na majeruhi huko Soweto Arusha, hiyo damu haijakutosha,nani aliyewafidia wahanga?
Kiongozi yeyote makini hawazi kuchonganisha utawala uliopo madarakan na wananchi.Sisi wote ni Watanzania na Wa-Africa,polisi ni sisi wenyewe,ni vijana,wetu,ni ndugu zetu na tumewaweka hapa kwa kutulinda sote bila ubaguzi,wala uchama.Wewe tayari ni kiongozi ambae kwako tungetaka mfano.Hata ungekuwa raisi leo,si kweli kwamba wananchi wote,vyama vyote wangekuchagua,au wangekukubali na hiyo hasa ndio demokrasia ya kweli.Hizi kauli za namna hii ni za kichochezi,kati ya raia na raia,polisi na raia,chama na chama,hukuna hoja nyingine?Hakuna lugha nyingine?

Usiwe unakula lunde mchana alafu bila maji mkuu...ona sasa madhara yake.unachafua hali hewa humu Jf.nategemea baada ya hii posti yako lazima utakuwa umeenda msalani mkuu
 
Ina maana mpaka sasa Polisi bado hajatambua kwanini wananchi wameanza kuwapiga mawe hadi kuwaua polisi.
Natabiri kutokea wa vifo vingi mwaka huu
 
Tuwakumbushe polisi kwamba vifaa vingine kama hivi viko kwenye mabucha vikakusanywe haraka visije vikahatarisha amani na utulivu.
 
intelejesia dhaifu kabisa tumejua mbinu zao za kale ,sasa ivi hatuangaiki na polisi tunashughulikia kuwapa elimu ya uraia na kulinda kura .kwa hiyo mafunzo ya ukakamavu ni lazima kwa kila mwanachama na hatuangaiki na propaganda dhaifu .
 
Acha kuaminisha watu kitu ambacho hujafanyia utafiti! huwezi kusema chadema ni magaidi eti kwavile kuna vijana wamekutwa na visu na manati.Acha ujinga, inamaana wamasai ni magaidi kwakutembea na visu? wewe hujuwi maana ya ugaidi. Waambie na wenzako hizo propaganda wawaeleze watoto wa chekechea. Tunasema: DIEU EST AMOUR...a ni kuwa, polisi wana vyanzo vyingi vya taarifa, hivyo mmoja wa makamanda wa CHADEMA alifikisha taarifa kwa jeshi la polisi juu ya uwepo wa vifaa vya kivita ndani ya ofisi ya makao makuu na pia kuna mpango wa kusambaza vifaa hivyo kote nchini.

Zifuatazo ndio picha za vifaa hivyo na jinsi CHADEMA ilivyojipanga kuandaa waasi ikitokea imeshindwa uchaguzi mkuu! Yale yanayotokea Kongo yataletwa Tanzania kama serikali haitachukua hatua juu ya jambo hili.

attachment.php

Baada ya vijana wa CHADEMA kuwekwa chini ya ulinzi na jeshi la polisi wakiwa na vifaa hivyo vya kijeshi.

attachment.ph
 
Kwa mtindo huu ndio maana VIPOLISI VINAULIWA NA RAIA KWA MAWE, kwa mtindo huu ndio maana Vipolisi vinanyang'anywa silaha na mtu aliyeshika fimbo.

Mwaka huu hadi kieleweke, BADO Kutonyesha KIFARU kinachomilikiwa na CHADEMA
 
Serikali inaacha kuharakisha kuletwa BVR kusudi WAPIGA KURA waandikishwe haraka na DAFTARI YA WAPIGA KURA ikamilike mapema kusudi kusiwe na uwezekano wa dosari kubwa kuweza kuathiri UCHAGUZI MKUU wao wapo bize na sherehe, kukimbiza moto(mwenge), kupambana na vyama vya upinzani, kupambana na waongozi wa dini, kutishia kufuta makanisa na misikiti nchini.

Matendo ya Dhuluma, hakika tufanye maamuzi kama tulivyoambiwa na waongozi wetu wa dini. Tusicheke tena na hiki chama cha Chenge na Prof.Tibaijuka. Tusicheke tena na hiki chama kinachotaka KUFUTA USAJILI WA DINI ZETU ili tubaki WAPAGANI, huu sio MPANGO WA MUNGU ni USHETANi.

Tuukatae Upagani kwa KUPIGA KURA HAPANA Katiba, NA Kuchagua CHama Cha Upinzani Katika Uchaguzi MKUU oktoba
 
Acha kuaminisha watu kitu ambacho hujafanyia utafiti! huwezi kusema chadema ni magaidi eti kwavile kuna vijana wamekutwa na visu na manati.Acha ujinga, inamaana wamasai ni magaidi kwakutembea na visu? wewe hujuwi maana ya ugaidi. Waambie na wenzako hizo propaganda wawaeleze watoto wa chekechea. Tunasema: DIEU EST AMOUR...a ni kuwa, polisi wana vyanzo vyingi vya taarifa, hivyo mmoja wa makamanda wa CHADEMA alifikisha taarifa kwa jeshi la polisi juu ya uwepo wa vifaa vya kivita ndani ya ofisi ya makao makuu na pia kuna mpango wa kusambaza vifaa hivyo kote nchini.

Zifuatazo ndio picha za vifaa hivyo na jinsi CHADEMA ilivyojipanga kuandaa waasi ikitokea imeshindwa uchaguzi mkuu! Yale yanayotokea Kongo yataletwa Tanzania kama serikali haitachukua hatua juu ya jambo hili.

attachment.php

Baada ya vijana wa CHADEMA kuwekwa chini ya ulinzi na jeshi la polisi wakiwa na vifaa hivyo vya kijeshi.

https://www.jamiiforums.com/attachment.ph[/QUOTE]

Msangi toka kutaka kuuwa akina Ulimboka mpaka kuuwa akina DR Mvungi sasa huko Mbeya anataka kuuwa nani aambiwe chadema ni taasisi
 
Acha kuaminisha watu kitu ambacho hujafanyia utafiti! huwezi kusema chadema ni magaidi eti kwavile kuna vijana wamekutwa na visu na manati.Acha ujinga, inamaana wamasai ni magaidi kwakutembea na visu? wewe hujuwi maana ya ugaidi. Waambie na wenzako hizo propaganda wawaeleze watoto wa chekechea. Tunasema: DIEU EST AMOUR...a ni kuwa, polisi wana vyanzo vyingi vya taarifa, hivyo mmoja wa makamanda wa CHADEMA alifikisha taarifa kwa jeshi la polisi juu ya uwepo wa vifaa vya kivita ndani ya ofisi ya makao makuu na pia kuna mpango wa kusambaza vifaa hivyo kote nchini.

Zifuatazo ndio picha za vifaa hivyo na jinsi CHADEMA ilivyojipanga kuandaa waasi ikitokea imeshindwa uchaguzi mkuu! Yale yanayotokea Kongo yataletwa Tanzania kama serikali haitachukua hatua juu ya jambo hili.

attachment.php

Baada ya vijana wa CHADEMA kuwekwa chini ya ulinzi na jeshi la polisi wakiwa na vifaa hivyo vya kijeshi.

https://www.jamiiforums.com/attachment.ph[/QUOTE]

hawa vijana chini ya kiapo cha wanasheria makini wa chadema watasema tu nani yupo nyuma ya Msangi RPC mwenye sifa za uuaji
 
Kwahiyo ninyi mkiingia madarakani mtalifanya jeshi liache kila chama cha siasa kimiliki vifaa vya kijeshi?

Ni vema ukaishi na kumbukumbu sio kuishi na tukio lililopo bila kukumbuka kuwa huko unakokushabikia mabuti ya kijeshi wanavaa na hawajawahi kuulizwa au kukamatwa na vipi juu ya kufundisha watoto matumizi na jinsi ya kushika silaha?
attachment.php

attachment.php
 
Aisee Wahuni kwenye uhuni, Yani Jeshi la Polisi intelegensia yenu imeona visu na kofia za mitumbani kuwa ndio muundo RED Bridgedi, Hakika mipolisi mingi haitumii magezi.
 
CHADEMA hila zenu dhidi ya Amani na utulivu wa taifa hili zinaendelea kubainika!

Watanzania wapenda Amani hatutakubali upuuzi huu!

Majitu ya cccm ni shida wizi wao,uongo wao, cjui tuwaweke kundi gani hapa nchini, mwaka huu mtauwana pale Lumumba na mwisho wenu ni Oct.
 
magaidi au wanajeshi siku hizi wanatumia manati??naomben majibu
 
Back
Top Bottom