CHADEMA waipigia kura CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]IJUMAA, OCTOBA 12, 2012 09:18 NA SAFINA SARWATT, MOSHI

UCHAGUZI wa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, ulikumbwa na mvutano mkali kati ya vyama viwili vya upinzani, hali iliyosababisha mgombea wa CCM kushinda uchaguzi huo.

Uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashari hiyo, ambapo mgombea wa CCM, Evarist Momburi alishinda kwa kupata kura 24 kati ya 44, huku mgombea wa Chama cha Tanzania Labour, (TLP), akipata kura 17.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya kutokea mvutano mkubwa baina ya vyama vya TLP na Chadema, kutokana na TLP kusimamisha mgombea, kinyume na makubaliano, ambapo awali inadaiwa vyama hivyo viliafikiana Chadema isimamishe mgombea.

Kutokana na hali hiyo, mgombea wa Chadema, Alex Umbela ambaye ni Diwani wa Kata ya Kirua Vunjo Mashariki, alitangaza kujitoa katika kinyang’anyiro hicho na kumwacha mgombea wa CCM, Evarist Momburi akipambana na Jese Makundi wa TLP.

Katika kinyang’anyiro hicho, mgombea wa CCM alishinda baada ya madiwani wa Chadema kuonekana kumuunga mkono, ili kumwangusha mgombea wa TLP, ambaye alikuwa anagombea nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.

Akizungumza wakati wakujitoa katika kinyang’anyiro hicho, mgombea wa Chadema Alex Umbela, alisema amefikia uwamuzi huo ili kulinda heshima ya chama chake.

Akizungumza katika uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Moris Mkoi aliwataka watendaji wa halmashauri hiyo kwenda vijijini, ili kusikiliza kero za wananchi.

Siasa za Kilimanjaro zinanitoa JASHO wakati MWINGINE...
 
Kumbe hata huko nyumbani hawajajipanga vizuri. Wanakimbilia Arusha, na sijui kama 2015 Chama chetu cha Chadema kama kitakuwa hai. Tuungane tujenge Chama chetu. Siyo vizuri kufagia uchafu nje huku ndani hapakaliki.

Afande nashukru, aaaa samahani Kamanda pamoja sana
 
wewe aha kelele cdm haina kwao ni ya watanzani.
 
Kumbe hata huko nyumbani hawajajipanga vizuri. Wanakimbilia Arusha, na sijui kama 2015 Chama chetu cha Chadema kama kitakuwa hai. Tuungane tujenge Chama chetu. Siyo vizuri kufagia uchafu nje huku ndani hapakaliki.

Afande nashukru, aaaa samahani Kamanda pamoja sana

Kaa kimya wewe gamba achana na chama chetu kabisaa!!
 
Chama chetu cha CHADEMA ili kiendeleee kuwa hai lazima pia kijenge tabia ya kuwa wakweli haswa pale kinaposhindwa na hii ni kukijenga chama tuache propaganda
 
Kaa kimya wewe gamba achana na chama chetu kabisaa!!

Chadema waipigia kura CCM halafu mnasema mnataka kuwang'oa madarakani, Chadema mnachofanya kwenye siasa za Tanzania ni sawa na kuziba shimo la panya na mkate wa nyama.
 
Ritz baada ya karibu miaka 51 bado unakikumbatia CCM kweli? There's something huoni KWELI.
 
Last edited by a moderator:
Chadema waipigia kura CCM halafu mnasema mnataka kuwang'oa madarakani, Chadema mnachofanya kwenye siasa za Tanzania ni sawa na kuziba shimo la panya na mkate wa nyama.

umewahi cheza draft au kamari lazima uliwe ndogo ndio ule kubwa kaa na akili yako ya ki magamba cdm wako jikoni wanapika yajayo
wameshajuwa janja ya tlp

wamachame na wamarangu wameshindwa kuungana kuing'oa ccm, wachagga pesa wameweka mbele mno halafu hawa ndio tuwape nchi siwatakula bila kunawa!!!
 
Chadema waipigia kura CCM halafu mnasema mnataka kuwang'oa madarakani, Chadema mnachofanya kwenye siasa za Tanzania ni sawa na kuziba shimo la panya na mkate wa nyama.

sitegemei comments tofauti na hizi maaana ndio upeo wako ulipofika hata hapa umejitahidi sana!
 
Sasa kwa nini mmeipigia kura CCM au ndio mmeishakuwa CCM-C?

Mkuu nadhani hapa akina Juma Duni, Mtatiro na wengineo watapata neno la kusema! CDM na CCM vimeungana kuiangusha TLP.

CCM waliungana na CUF; CUF wakaitwa CCM-B na sasa CCM wameungana na CDM basi hakika na CDM kwa huko Moshi watakuwa CCM-B (au C kwa kuwa B ilishachukuliwa na CUF).

Kwa kifupi hapo CDM wamekosa ukomavu wa kisiasa yaani afadhali CCM ipate kuliko mpinzani mwenzao kupata!! Hakuna upinzani hapa bali maslahi binafsi.
 
sitegemei comments tofauti na hizi maaana ndio upeo wako ulipofika hata hapa umejitahidi sana!

Mkuu OSOKONI hili suala kwenye nyanja ya upinzani si la kulichekelea na kulipuuza. CDM isidhani kwamba basi peke yake ndio inaweza kutwaa dola bila kuwashirikisha wapinzani wengine. Nchi za wenzetu wapinzani wanaungana dhidi ya vyama tawala lakini hapa kwetu inakuwa tofauti yaani mpinzani anaungana na chama tawala ili kumwangusha mpinzani mwenzake! Hii ni hatari kubwa.
 
Last edited by a moderator:
Kimbunga itatuchukua muda sana kujua tufanye nini ili kuishinda CCM. leo watu wanadhani kuishinda CCM kwenye baadhi ya majimbo kunatosha. Kauli za viongozi wetu wa vyama vya upinzani dhidi ya vyama vingine vya upinzani yanakera zaidi kuliko yale wanayoyatoa dhidi ya CCM. Hawajifunzi kabisa kupingana bila kuwekeana hasira ili mbele ya safari washirikiane kwenye jambo jingine.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom