OSOKONI
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 10,965
- 5,344
Vyama haviwezi kuungana kama havina itikadi na manifesto angalau inayofanana! kuungana tu ili mradi kuondoa chama tawala madarakani hakuna maana mfano Raila aliungana na Mwai kibaki kuoindoa KANU then what followed? walitengana na uchaguzi uliofuata wakauana kuliko hata wakati wa KANU, so vyama viungane kama vinafanana itikadi na sera!!Mkuu OSOKONI hili suala kwenye nyanja ya upinzani si la kulichekelea na kulipuuza. CDM isidhani kwamba basi peke yake ndio inaweza kutwaa dola bila kuwashirikisha wapinzani wengine. Nchi za wenzetu wapinzani wanaungana dhidi ya vyama tawala lakini hapa kwetu inakuwa tofauti yaani mpinzani anaungana na chama tawala ili kumwangusha mpinzani mwenzake! Hii ni hatari kubwa.