CHADEMA waifungulia CUF njia…

CHADEMA waifungulia CUF njia…

CUF seezed to be part of any relevant oposition in Tanzania the moment it went into "mariage" of convinience with CCM in Zanzibar. Further more I find image of CUF to be one of "separetists" thus lack a national "outlook". I just cant see how CUF can overcome the above embeded haddles and become what you have tried to potray here.
 
Muulize Hamad Rashid zile pesa slizo pewa na Ccm ili awe mdhamini wa chama kipya alipewa kama nani, pia ile ndoa ya ccm na cuf huko Zanzibar ina maana gani, mke mmoja hawezi olewa na waume wawili
 
Mtu yeyote akiangalia hii video ataona kuwa chadema inafanya bunge kama genge la magumzo!!!

Kama CDM wasingekuwemo Bungeni,ningeutumia muda huo wa kuangalia Bunge kusikiliza muziki wa kunifariji nisichoke ku fight licha ya dhulma ya hata kile kidogo nipatacho inayofanywa na serikali yangu!masaa 18 ya kufanya kazi,nabaki na 30% tu ya kipato!ni sawa na kutumiwa kwa masaa 12 alafu yangu ni hayo 6 tu yaliyobaki!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Magamba Mtajichanganya sana lakini mmeshashtukiwa juzi vuvuzela alienda kujaribisha cd yake ya ugaidi Moshi ikakosa soko tungeni move nyingine chapchap hiyo ishadunda kabla haijaingia mtaani.
 
Hivi kumbe Ze marcopollo ndo yeye!Duh!Hajakubali tuu!Ee Mungu ingilia kati kwa watu kama hawa wanaohimiza kwa nyimbo tamu udhalimu wa wanyonge huku wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Kimbe na wewe unasapoti ugaidi na watembea na sumu mifukoni hadi bar.
 
Mkuu nini maoni yako kuhusu machafuko yaliyokuwa yanatokea Zanzibar pamoja na Hali tete ya kisiasa iliyokuwepo visiwani kabla ya serikali ya umoja wa kitaifa.
Aliyeyaratibu machafuko hayo ni nani kama siyo ccm kuiba kura za cuf. Hii inshu naijua vizuri maana kipindi hicho nilikuwa nasoma zanzibar.Au unataka nikueleze jinsi tulivyotumiwa na ccm kuhihujumu cuf kwenye uchaguzi wa mwaka 2000?
 
Magamba Mtajichanganya sana lakini mmeshashtukiwa juzi vuvuzela alienda kujaribisha cd yake ya ugaidi Moshi ikakosa soko tungeni move nyingine chapchap hiyo ishadunda kabla haijaingia mtaani.

Kinachokumbatia ugaidi ni chadema...au humfahamu vizuri lwakatare..sasa ccm wamejichanganya kwa lipi
 
Chama kinachoshindwa kuplay role ya chama kikuu cha upinzani Bungeni ni dhahiri kuwa hakwezi kusimamia dola...

Nilishakuambia akili yako sidhani kama ipo sawa maana jumbe zako kila siku ni kulalamika tu tena unalalamikia chadema tu. Tulizana na si lazima uandike hapa.
 
Wanaosema kuwa unaleta mada KISHABIKI na KIAFIKI wako sahihi kabisa:-
1. Unashindwa kukukumbuka kuwa bunge la tisa lilikuwa linaongozwa na nani? Na alichaguliwa katika mazingira gani?
2. Unashindwa kubaini ni changamoto zipi za muhimu ambazo zilijitokeza wakati wa Bunge la 9 na spika wa wakati huo alitumia busara kiasi gani kuliongoza bunge kukabiliana na changamoto zile.
3. Huyu mama ambaye ndiye kiongozi wa bunge la sasa, ana upeo gani wa mambo ya sheria, alichaguliwa kwa malengo gani na ni akina nani walifanikisha yeyey kuwa spika? Hayo yote hutaki kuyafahamu, na hata kama unayafahamu basi unajitoa AKILI NA KUBAKI EMPTY HEAD, kweli kushabikia ccm hadi uwe na AKILI ZA MAITI.

Kwa akili zako unafikiri CUF na ndoa yao na ccm ndio wangelikuwa wengi bungeni, spika angelikuwa na mambo ya hovyo kama ilivyo sasa? Kwa nini angelifanya hivyo ilihali anfahamu wazi kuwa wasingelikuwa na effect yoyote?

Dawa ya ccm sasa hivi ni JINO KWA JINO, WAKIMWAGA UGALI, TUNAMWAGA MBOGA, wananchi tunaelewa nini tutafanya 2015. Wewe hauna cha kutufundisha.
 
CUF seezed to be part of any relevant oposition in Tanzania the moment it went into "mariage" of convinience with CCM in Zanzibar. Further more I find image of CUF to be one of "separetists" thus lack a national "outlook". I just cant see how CUF can overcome the above embeded haddles and become what you have tried to potray here.

This is interesting.

May you be explicit on the "separist image" of CUF?
 
CHADEMA waifungulia CUF njia…kivipi?

Tatizo hili lilisababishwa na ubinafsi wa kiongozi aliyeng´ang´ania kuhodhi nafasi ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni bila kuheshimu matakwa ya wabunge. Wabunge wengi walipendelea Kiongozi wa Upinzani Bungeni awe kijana aliyeonyesha uwezo wa juu katika Bunge la 9.

Madhara ya nafasi ya uongozi Bungeni kuchuliwa na mtu aliyetoka bench ndio haya.

Bunge letu lingekuwa na manufaa na upinzani ungeonekana kuwa na maana iwapo Kiongozi wa upinzania angekuwa kijana mwenye uwezo mkubwa ulioonekana bayana kwenye Bunge la 9, halafu naibu wake angekuwa hamad Rashid wa CUF ambaye ana uzoefu wa kuwa Bungeni tangu enzi za chama kimoja, halafu Mbowe angekuwa Chief Whip.

Mbowe pamoja na kuwa uwezo wake wa kufikiria ni mdogo kutokana na elimu yake, lakini ana busara za kuzaliwa. nafasi ya chief Whip angeimudu vizuri kama jinsi anavyomudu Uenyekiti wa chama.

Sasa hivi ni too late kufanya marekebisho hayo, lakini ni fundisho kwa upinzani kwa siku zijazo...
 
kweli hiki nacho bila upembuzi wala fkra za wakati, mwenendo na mazingira ya kibunge kati ya nyakati hizi mbili unajaribu kuchezea akili na mantiki za jukwaa makini lenye uwezo mkubwa wa kuchangaua masuala?, kwa hili umepotoka!!
 
CHADEMA imeshindwa kuitumia vizuri nafasi yake kama chama kikuu cha upinzani kwa manufaa ya taifa.

Hali ilianza kuonekana tangu awali baada ya uchaguzi mkuu ambapo CHADEMA ilikataa kushikisha vyama vingine kwenye uongozi wa upinzani Bungeni. Uamuzi huu wa cHADEMA uliwasikitisha wapenda mabadiliko wengi.

Hii ni tofauti na chama cha wananchi CUF ambacho kiliishirikisha chadema kwenye uongozi wa upinzani Bungeni katika Bunge liliopita. Manufaa yake kwa taifa tumeyaona, Bunge la tisa liliweza kusimamia hoja nzito za kitaifa na kuitetemesha serikali mpaka Waziri Mkuu akajiuzuru. Bunge hili la 10 lina wabunge wengi zaidi wa upinzani lakini hakuna mafanikio yoyote katika kujenga hoja!

Zaidi ya hilo, mara kadhaa CHADEMA wamekuwa wakikimbia mijadala kwa mtindo wa kususa ambao haujawahi kuleta manufaa yoyote. Jambo kama la kususia hotuba ya Mkuu wa Nchi halikuwahi kutokea Bungeni wakati CUF ilipokuwa chama kikuu cha upinzani kwenye bunge la 9.

Kadri siku zinavyoenda wananchi wanazidi kushuhudia jinsi CHADEMA inavyoshindwa kuwakilisha maslahi ya taifa Bungeni. Jambo linalosikitisha zaidi ni kwamba siku hizi wabunge wa CHADEMA wakiongea taarifa pekee inayoweza kutolewa ni kwamba “wamemchana kiongozi fulani”.

Anayeongoza katika tabia hii ya “kuchana” ni Sugu ambaye jana ameelezewa kuwa alimchana mbunge wa Iramba Mashariki. Huo ndio ulikuwa mchango wake kwenye bajeti ya Waziri Mkuu!!!

Kwa kweli inasikitisha pale input ya speech ya mbunge katika kuchangia bajeti ya Waziri Mkuu inapokuwa ni kumchana kiongozi! Mambo haya hayakuwepo Bungeni wakati CUF ilipokuwa chama kikuu cha upinzani Bungeni. Hamad Rashid wa CUF alikuwa maridadi zaidi katika kusimamia shughuli na hoja za upinzani Bungeni kuliko anavyofanya kiongozi wa upinzani wa Bunge hili la 10.

Picha inayowekwa na CHADEMA ni kwamba upinzani ni vurugu. Wananchi wastaarabu wanaanza kuchukizwa na tabia za uvunjifu wa kanuni na kumkosea heshima Spika zinazofanywa na wabunge wa chadema. Hamad Rashid wa CUF hakuruhusu hili, lakini kiongozi wa sasa wa upinzani Bungeni anaona vurugu na kubishana na Spika kama burudani.

Nikumbushe tu kuwa taarifa zilizopo zinaonyesha hakuna mbunge hata mmoja wa CHADEMA aliyeweza kutekeleza ahadi zake alizotoa kwa wananchi jimboni. Kwahiyo wananchi wanaweza kuwa na imani na wabunge wa CHADEMA iwapo wataona angalau Bungeni wana michango yenye tija.

Kwavile jimboni wabunge wa chadema hawatekelezi ahadi na Bungeni wanaenda “kuchanana” wananchi watakuwa hawana sababu ya kuchagua CHADEMA. Hasahasa ikizingatiwa kuwa chadema kimekuwa ni chama kinachoainisha matatizo bila kutoa jinsi yoyote ya utatuzi.

Vilevile CUF watakuwa na sababu ya kuwaambia wananchi kuwa CHADEMA wameharibu image ya upinzani Bungeni - jambo ambalo ni kweli. Jambo hilo litaiwezesha CUF kuchukua kura nyingi za wapenda upinzani ambazo zingeweza kuwa za CHADEMA katika majimbo ya Tanznia Bara. Kwa vigezo hivyohivyo CHADEMA itaendelea kukosa kura za Zanzibar.

Bottomline: CHADEMA imeligeuza Bunge kuwa jukwaa la kampeni. CUF walipokuwa wanaongoza upinzani Bungeni walisimamia hoja kwa maslahi ya taifa. Tabia ya vurugu na kumkosea heshima Spika inayofanywa na CHADEMA ni mtaji wa kisiasa kwa CUF.

Ushauri: CHADEMA ijiepushe na tabia za mipasho mbele ya TBC mkiwa Bungeni. Sugu apewe mafunzo maaluma ya kuchagua maneno ya kuongea Bungeni – itafaa zaidi iwapo hotuba zake zitapitiwa na Mnyika kabla hajazisoma.
Kaka/Dada,
Mbona kama vile umechelewa? CUF kimebaki Zanzibar peke yake na huko pia kimeolewa. Huku Bara CUF kwishney.
 
Yawezekana unaifahamu siasa kwani ulicho ongea ni ukweli mtupu endelea unaweza kuja kua mwanasiasa mzuri TZ
 
Jembe Letu 'SUGU'hapend ubabaishaji na ndio mana anaongea kwa uchungu,kama hukumuelewa ntafute nliyempgia kura nikueleweshe! GREENCITY FOREVER
 
CHADEMA imeshindwa kuitumia vizuri nafasi yake kama chama kikuu cha upinzani kwa manufaa ya taifa.

Hali ilianza kuonekana tangu awali baada ya uchaguzi mkuu ambapo CHADEMA ilikataa kushikisha vyama vingine kwenye uongozi wa upinzani Bungeni. Uamuzi huu wa cHADEMA uliwasikitisha wapenda mabadiliko wengi.

Hii ni tofauti na chama cha wananchi CUF ambacho kiliishirikisha chadema kwenye uongozi wa upinzani Bungeni katika Bunge liliopita. Manufaa yake kwa taifa tumeyaona, Bunge la tisa liliweza kusimamia hoja nzito za kitaifa na kuitetemesha serikali mpaka Waziri Mkuu akajiuzuru. Bunge hili la 10 lina wabunge wengi zaidi wa upinzani lakini hakuna mafanikio yoyote katika kujenga hoja!

Zaidi ya hilo, mara kadhaa CHADEMA wamekuwa wakikimbia mijadala kwa mtindo wa kususa ambao haujawahi kuleta manufaa yoyote. Jambo kama la kususia hotuba ya Mkuu wa Nchi halikuwahi kutokea Bungeni wakati CUF ilipokuwa chama kikuu cha upinzani kwenye bunge la 9.

Kadri siku zinavyoenda wananchi wanazidi kushuhudia jinsi CHADEMA inavyoshindwa kuwakilisha maslahi ya taifa Bungeni. Jambo linalosikitisha zaidi ni kwamba siku hizi wabunge wa CHADEMA wakiongea taarifa pekee inayoweza kutolewa ni kwamba “wamemchana kiongozi fulani”.

Anayeongoza katika tabia hii ya “kuchana” ni Sugu ambaye jana ameelezewa kuwa alimchana mbunge wa Iramba Mashariki. Huo ndio ulikuwa mchango wake kwenye bajeti ya Waziri Mkuu!!!

Kwa kweli inasikitisha pale input ya speech ya mbunge katika kuchangia bajeti ya Waziri Mkuu inapokuwa ni kumchana kiongozi! Mambo haya hayakuwepo Bungeni wakati CUF ilipokuwa chama kikuu cha upinzani Bungeni. Hamad Rashid wa CUF alikuwa maridadi zaidi katika kusimamia shughuli na hoja za upinzani Bungeni kuliko anavyofanya kiongozi wa upinzani wa Bunge hili la 10.

Picha inayowekwa na CHADEMA ni kwamba upinzani ni vurugu. Wananchi wastaarabu wanaanza kuchukizwa na tabia za uvunjifu wa kanuni na kumkosea heshima Spika zinazofanywa na wabunge wa chadema. Hamad Rashid wa CUF hakuruhusu hili, lakini kiongozi wa sasa wa upinzani Bungeni anaona vurugu na kubishana na Spika kama burudani.

Nikumbushe tu kuwa taarifa zilizopo zinaonyesha hakuna mbunge hata mmoja wa CHADEMA aliyeweza kutekeleza ahadi zake alizotoa kwa wananchi jimboni. Kwahiyo wananchi wanaweza kuwa na imani na wabunge wa CHADEMA iwapo wataona angalau Bungeni wana michango yenye tija.

Kwavile jimboni wabunge wa chadema hawatekelezi ahadi na Bungeni wanaenda “kuchanana” wananchi watakuwa hawana sababu ya kuchagua CHADEMA. Hasahasa ikizingatiwa kuwa chadema kimekuwa ni chama kinachoainisha matatizo bila kutoa jinsi yoyote ya utatuzi.

Vilevile CUF watakuwa na sababu ya kuwaambia wananchi kuwa CHADEMA wameharibu image ya upinzani Bungeni - jambo ambalo ni kweli. Jambo hilo litaiwezesha CUF kuchukua kura nyingi za wapenda upinzani ambazo zingeweza kuwa za CHADEMA katika majimbo ya Tanznia Bara. Kwa vigezo hivyohivyo CHADEMA itaendelea kukosa kura za Zanzibar.

Bottomline: CHADEMA imeligeuza Bunge kuwa jukwaa la kampeni. CUF walipokuwa wanaongoza upinzani Bungeni walisimamia hoja kwa maslahi ya taifa. Tabia ya vurugu na kumkosea heshima Spika inayofanywa na CHADEMA ni mtaji wa kisiasa kwa CUF.

Ushauri: CHADEMA ijiepushe na tabia za mipasho mbele ya TBC mkiwa Bungeni. Sugu apewe mafunzo maaluma ya kuchagua maneno ya kuongea Bungeni – itafaa zaidi iwapo hotuba zake zitapitiwa na Mnyika kabla hajazisoma.

kwa hii post yako ishaonekana na nape usiwe na wasiwasi wanao wataenda chooni
 
Back
Top Bottom