Jaji Tendwa kwenye hili la kukata ruzuku ningependa alifanye haraka haraka, lengo kuu hapa ni kutuokolea fedha zetu wananchi zisiende katika matumbo ya hao MAJAMBAZI wasiotumia silaha.
Jeuri na kiburi chao tuone kitaishia wapi wapuuzi hao, kwanza kwanini asirejee katiba ya nchi imejieleza waziwazi kuhusu kutokuwa na uhalali wa hiki chama katika siasa za hapa nchini.
Katiba ya nchi imekataa kuwa na chama cha siasa ambacho kimeundwa kikanda, hapa kwenye hili la ukanda ukiangalia vyama vyote vya siasa utaona ni CHADEMA pekee ndio wamejazana WACHAGA na WA-ARUSHA.
Kama baba wa taifa angekuwa na akili kama ya hawa MAGWANDA leo hii nafasi zote ndani ya chama angewajaza watu wa MUSOMA, lakini akufanya hivyo, aliamini katika "binadamu wote ni sawa" na wote wana haki ya kupata fursa katika nafasi yeyote ndani ya chama au kitaifa.
Wewe mwananchi unaeipigania CHADEMA na kuiunga mkono, fanya tafiti na ukijue kwa undani wake, usiridhike kwa maneno ya hao wasanii wachumia tumbo, wataongea lolote hili wakuteke akili yako kwa lengo la kukutumia.
Mabadiliko ya hili taifa yatatokana na CCM, jambo la maana ni kuiacha serikali itekeleze ilani ya chama ya mwaka 2010 na muifanyie tathmini kutokana na yale yaliyoelezwa kwenye ilani ya chama, kama yametekelezwa au laa.
"BADILIKA UBADILI TAIFA".