Katika kile kinachoonekana kuwa ndio mwelekeo wa matukio kama Pipooz pawa itaendelea, na CDM kuendelea kumgomea Msajili wa vyama Jaji John Tendwa, yeye ameenda mbali zaidi na kutishia kukata ruzuku ya CDM.
CDM wamealikwa pamoja na vyama vingine vyote kwenye kikao cha "usuluhishi" na mashauriano kati yake na vyombo vya serikali lakini wamekataa mwaliko huo.
Kikao hiki ni kufuatia matukio mabaya sana yaliyopelekea wananchi kadhaa kupoteza maisha katika mihadara na maandamano ya CDM mikoani ambayo udhibiti wake uliofanywa na Jeshi la Polisi umeleta utata mkubwa.
Tishio la Tendwa ingawaje siyo direct, linawakaribisha CDM kuendelea kususia shughuli zinazopangwa na Msajili wa Vyama, na kwa vile ofisi ya Msajili ndiyo inayo shughulikia ruzuku ya vyama, basi matokeo yake yatakuwa dhahiri-ikiwa ni sawa na kususia ruzuku!!
Source: Majira(front page) and Mwananchi(page 4)
My Take:
CDM dont let your fame go to your head!!!