Chadema wagomea mwaliko wa Tendwa

Kwani ruzuku inatoka mfukoni mwake, cdm hawamkubali tendwa sio ofis ya msajili akate ruzuku apo ndo atajuta kuzaliwa na kuropoka ovyo kama lusinde
 
Tendwa anamambo ya kitoto sana, anajua kabisa Ruzuku inatolewa kisheria kwa chama husika kupitia ofisi ya msajiri wa vyama vya siasa na wala sio sadaka au msaada binafsi unaotolewa na Tendwa.

Ruzuku ni haki ya Chadema kisheria.

Tendwa wivu utamuua, anaona Chadema wanafaidi sana kupata ruzuku na amejaribu kwa hali na mali kutafuta namna ya kuwanyima ruzuku na sasa ameona bora aropoke kabisa.

Chadema walisema hawatatoa ushirikiano kwa Tendwa hii ni kutokana na namna anavyominya demokrasia.
 
Nilikuwa sijui kwamba Tendwa ndio anatowa ruzuku kwa vyama vyenye Wabunge. huu ulevi wa madaraka ni mbaya kuliko mlevi wa ulanzi au dengeruwa.
 
Katika kile kinachoonekana kuwa ndio mwelekeo wa matukio kama Pipooz pawa itaendelea, na CDM kuendelea kumgomea Msajili wa vyama Jaji John Tendwa, yeye ameenda mbali zaidi na kutishia kukata ruzuku ya CDM.

CDM wamealikwa pamoja na vyama vingine vyote kwenye kikao cha "usuluhishi" na mashauriano kati yake na vyombo vya serikali lakini wamekataa mwaliko huo.

Kikao hiki ni kufuatia matukio mabaya sana yaliyopelekea wananchi kadhaa kupoteza maisha katika mihadara na maandamano ya CDM mikoani ambayo udhibiti wake uliofanywa na Jeshi la Polisi umeleta utata mkubwa.

Tishio la Tendwa ingawaje siyo direct, linawakaribisha CDM kuendelea kususia shughuli zinazopangwa na Msajili wa Vyama, na kwa vile ofisi ya Msajili ndiyo inayo shughulikia ruzuku ya vyama, basi matokeo yake yatakuwa dhahiri-ikiwa ni sawa na kususia ruzuku!!

Source: Majira(front page) and Mwananchi(page 4)

My Take:
CDM dont let your fame go to your head!!!

Unajuwa ni vizuri kwa mtu wa level na taaluma yake akaquote kifungu cha sheria anachokisimamia kutoa kauli/vitisho vyake vinginevyo tunazidi kumuona adui no 1 wa demokrasia nchini.

Na kama kuna shabiki wa CCM ambaye ana mawazo chanya hatoweza kamwe kushabikia vitendo vya kitumbafu vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wa serekali wenye dhamana kama kina tendwa na kamuhanda (just to mention few) kwani badala ya kuubomoa upinzani kama wanavyodhani kinauongezea umaarufu na kuwafanya hata wasioushabikia wafanye hivyo kwani huhitaji akili nyingi sana kuonana kukerwa na yanayofanywa.
 
Jaji Tendwa kwenye hili la kukata ruzuku ningependa alifanye haraka haraka, lengo kuu hapa ni kutuokolea fedha zetu wananchi zisiende katika matumbo ya hao MAJAMBAZI wasiotumia silaha.

Jeuri na kiburi chao tuone kitaishia wapi wapuuzi hao, kwanza kwanini asirejee katiba ya nchi imejieleza waziwazi kuhusu kutokuwa na uhalali wa hiki chama katika siasa za hapa nchini.

Katiba ya nchi imekataa kuwa na chama cha siasa ambacho kimeundwa kikanda, hapa kwenye hili la ukanda ukiangalia vyama vyote vya siasa utaona ni CHADEMA pekee ndio wamejazana WACHAGA na WA-ARUSHA.

Kama baba wa taifa angekuwa na akili kama ya hawa MAGWANDA leo hii nafasi zote ndani ya chama angewajaza watu wa MUSOMA, lakini akufanya hivyo, aliamini katika "binadamu wote ni sawa" na wote wana haki ya kupata fursa katika nafasi yeyote ndani ya chama au kitaifa.

Wewe mwananchi unaeipigania CHADEMA na kuiunga mkono, fanya tafiti na ukijue kwa undani wake, usiridhike kwa maneno ya hao wasanii wachumia tumbo, wataongea lolote hili wakuteke akili yako kwa lengo la kukutumia.

Mabadiliko ya hili taifa yatatokana na CCM, jambo la maana ni kuiacha serikali itekeleze ilani ya chama ya mwaka 2010 na muifanyie tathmini kutokana na yale yaliyoelezwa kwenye ilani ya chama, kama yametekelezwa au laa.

"BADILIKA UBADILI TAIFA".
 
Unajuwa ni vizuri kwa mtu wa level na taaluma yake akaquote kifungu cha sheria anachokisimamia kutoa kauli/vitisho vyake vinginevyo tunazidi kumuona adui no 1 wa demokrasia nchini.

Na kama kuna shabiki wa CCM ambaye ana mawazo chanya hatoweza kamwe kushabikia vitendo vya kitumbafu vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wa serekali wenye dhamana kama kina tendwa na kamuhanda (just to mention few) kwani badala ya kuubomoa upinzani kama wanavyodhani kinauongezea umaarufu na kuwafanya hata wasioushabikia wafanye hivyo kwani huhitaji akili nyingi sana kuonana kukerwa na yanayofanywa.

Hakuna mwananchi mwenye akili timamu anaebabaishwa na umaarufuu wa kipumbavu wa chadema.

Lijue hilo mkuu.
 
Kumbe rizuku ya vyama vya siasa inatolewa na familia ya John Tendwa.

Ili zee sijuhi uwa linafikiriaga kabla ya kuongea,me nilidhani siku ile itv kipima joto lilipodhalilishwa with data na vijana wadogo kua fikra zake ni finyu nikadhani litakua makini kabla ya kutoa kauli,kumbe wapi!ila sishangai,kama mwenyekiti wa chama anataka kuifanya Kigamboni kua kama New York,na Kigoma kua kama Dubai,huku wanafunzi wanakaa Chini,rais na waziri mkuu wanaongoza nchi huku hawajui kwa nini Tanzania ni maskini,mawaziri wao nao wanawaza uchawi na kusema hawaogopi kurogwa unategemea kuna mfuasi wa iko chama atakua well upstairz?lazima watakua na dead brain
 
jamaa wanapenda sifa hawa balaa mbowe alisema hachukui gari bungen kimya kimya kalichukua leo wanamkataa mtu aliyewapitisha kuwa chadema lkn ruzuku ya serikali wanachukua Baniani mbaya kiatu chake dawa....wanafiki wakubwa kataeni vyote
 
Hakuna mwananchi mwenye akili timamu anaebabaishwa na umaarufuu wa kipumbavu wa chadema.

Lijue hilo mkuu.

Hongera kwa majibu mwanzuri nadhani hata wachangiaji wengine wataona jinsi ulivyo na akili timamu na jinsi ulivyonijibu hoja ambayo sikuitoa mimi....Kweli wewe ni jembe...dah you are among the few great thinkers!
 
Hakuna mwananchi mwenye akili timamu anaebabaishwa na umaarufuu wa kipumbavu wa chadema.

Lijue hilo mkuu.

Tunataka hoja na si matusi,au ndipo ukomo wako wa uwezo wa kujenga hoja ulipoishia?
 
Katika kile kinachoonekana kuwa ndio mwelekeo wa matukio kama Pipooz pawa itaendelea, na CDM kuendelea kumgomea Msajili wa vyama Jaji John Tendwa, yeye ameenda mbali zaidi na kutishia kukata ruzuku ya CDM.

CDM wamealikwa pamoja na vyama vingine vyote kwenye kikao cha "usuluhishi" na mashauriano kati yake na vyombo vya serikali lakini wamekataa mwaliko huo.

Kikao hiki ni kufuatia matukio mabaya sana yaliyopelekea wananchi kadhaa kupoteza maisha katika mihadara na maandamano ya CDM mikoani ambayo udhibiti wake uliofanywa na Jeshi la Polisi umeleta utata mkubwa.

Tishio la Tendwa ingawaje siyo direct, linawakaribisha CDM kuendelea kususia shughuli zinazopangwa na Msajili wa Vyama, na kwa vile ofisi ya Msajili ndiyo inayo shughulikia ruzuku ya vyama, basi matokeo yake yatakuwa dhahiri-ikiwa ni sawa na kususia ruzuku!!

Source: Majira(front page) and Mwananchi(page 4)

My Take:
CDM dont let your fame go to your head!!!

Wakati sheria za vyama vya siasa zinapitishwa....Kama kawaida mambo yaliraisishwa tu fasta fasta bila tafakari yakina......

Kifupi Tndwa na Ofisi yake haina namna yyte ya kuinyma CDM ruzuku kisa kususia mkutano wa kujiosha wa Tndwa Na policcm.

Atasema sana lakini mwisho wasiku ukweli utabaki palepale POLISI WANATUMIKA KUVUNJA AMANI YA NCHI ILI KUWATISHA RAIA. hivyo kama yeye ni muwazi kama anavyofikiri aache kuuma maneno atamke wazi lini na wapi mikutano ya chamachochote cha siasa 'ambayo haikuzengewa na askari' imesababisha vurugu na mauaji?

Mbona maandamano ya jana "waislamu" yalilindwa na askari hao hao waliyoyanyima kibali.................na hakukuwa na bomu,la machozi, maji ya kuwasha, mitama, ngumi wala marungu.

Watanzania tunajuwa tunachokitaka, viongozi wanalazimisha ajenda zao ili waendelee kuwapo ktk nafasi zao hatakama ni kwakuuwa raia, na kwasasa polisi ndio wanaoweza kufanikisha hilo.

Tafakari...............chukua hatua ...................vua gamba..................vaa uzalendo.......
 
Back
Top Bottom