Chadema wagomea mwaliko wa Tendwa

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekataa mwaliko wa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kushiriki katika semina aliyoiandaa kuhusu amani na usalama wa nchi.

Chama hicho kimesema hakitashiriki katika semina hiyo wakati huu kwa kuwa kinasubiria hatua za Rais kuhusu mauaji ya kisiasa yaliyotokea katika mikoa mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Chadema, John Mnyika, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema chama hicho kimechukua hatua hiyo kikitambua umuhimu wa amani na usalama wa nchi na wajibu wa Jeshi la Polisi pamoja na Vyama vya Siasa katika kukuza demokrasia ya vyama vingi.

Mnyika alisema hatua hiyo imefikiwa kufuatia utendaji dhaifu na wa kipropaganda unaoonyeshwa na Tendwa uliosababisha Kamati Kuu ya Chadema kumtangaza kuwa ni adui wa demokrasia na hafai kuwa katika nafasi aliyo nayo.

“Kamati Kuu iliazimia kuwa pamoja na kuendelea kuheshimu sheria ya vyama vya siasa, Chadema haitashiriki shughuli zozote zitakazosimamiwa na John Tendwa hadi hapo atakapoondolewa katika nafasi yake na kuteuliwa msajili mwingine,” alisema.

Alisema Kamati Kuu ya Chadema ilifanya kikao maalumu Septemba 9 mwaka huu kilichojadili hali ya siasa nchini kufuatia mfululizo wa mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi katika shughuli za kisiasa za Chadema na mipango ya baadhi ya viongozi wa Serikali ya kudhibiti Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) kwa mbinu haramu.

“Katika majadiliano ya kina kabla ya kufikia maamuzi Kamati Kuu pamoja na mambo mengine ilieleza kusikitishwa na kauli za kisiasa ambazo zimekuwa zikitolewa na Tendwa, zenye mwelekeo wa kukibeba Chama Cha Mapinduzi ( CCM) na serikali,” alisema.

Source:Nipashe Ijumaa

Updates.....

Katika Taarifa leo asubuhi Ch 10 Msajili John Tendwa amesikitishwa na CDM kususia semina hiyo na kusema si haki hata kidogo na ni kutokutimiza wajibu na kutokumtendea haki.Pia Tendwa kawashauri CDM kususia pia na Ruzuku ya Serikali.John Tendwa alikuwa anazungumzia hali hiyo kwa huzuni kubwa.Huzuni iliyoonyeshwa na Tendwa imeonyesha wazi semina hiyo ilikuwa inawalenga CDM lakini wakamzidi kete.
 
Kwa mtazamo wangu kataa neno sio wito, ni hayo tu. N ingekua poa CDM ndio kutumia semina hii kumfundisha Tendwa.
 
Wazo lako kama zuri Vile!! Ningeomba yawepo Masharti ya Kuhudhuria ila Tendwa aelezwe Ukweli!! Kwani Namwona Tendwa kama Hajali Vile kwani Kila Jumapili anatinga maeneo ya Kimara Korogwe na kufunguliwa Geti na Kujificha Huko!! Duh Viongozi na NJI HII?
 
i hate the way he talks, tendwa huongea kama mtu wa huakika sana lakini ukisikiliza kinachotoka nyuma ya pengo ni ugolo wa ajabu! jamaa ana boa vibaya sana sema hajijui, naongea kutoka ndani ya rohoo yangu jamaa simpendi jinsi anavyo jiona mjuaji kumbe hakuna kitu
 
541089_348684461890310_950371795_n.jpg

Hii kitu inawatisha sana!
 
Tendwa hana sifa/credibility ya kuendelea kuwa msajili wa vyama vya siasa nchi hii. Hana! Si mara moja, wala mbili amekuwa anatoa matamshi yenye kuegemea upande mmoja na wakati mwingine ya kutishia wanasiasa. Mfano kauli yake wakati wa uchaguzi mdogo Arumeru ilionesha ni jinsi gani hastahili hata kidogo kukalia kiti cha msajili wa vyama.

Nakubaliana na hatua ya CHADEMA kutoshirikiana naye. Haonekani kusimamia haki na wala haonekani kufanya kazi within the parameters za msajili. Anaandaa semina ya amani na utulivu baada ya kutishia kuwafuta? Tayari alishaonesha msimamo wake, sasa anawaitia nini kama sio kejeli?
 
Hali hiyo inamstahili kwasababu kageuka refarii anayependelea upande mmoja
 
Kwa mtazamo wangu kataa neno sio wito, ni hayo tu. N ingekua poa CDM ndio kutumia semina hii kumfundisha Tendwa.

Mhnnn... hawa jamaa wa 'liwalo na liwe' sidhani kama wanafundishika. I support chadema's move against Tendwa. The man should know how serious tanzanians are in preserving peace. hatutaki mauaji, hatutaki wanaoua, hatutaki wanaosapport mauaji aidha direct or indirect ktk ngazi yoyote-from the presidence to a farmer. hatutaki!!! hatutaki hatutaki!!! 'mtanzania mmoja akifa kwa uzembe wa aina yoyote hile ni wengi mno,
 
Polisi wamealikwa kwenye hiyo semina? Nionavyo mimi polisi ndio inawafaa sana hii semina!!
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekataa mwaliko wa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kushiriki katika semina aliyoiandaa kuhusu amani na usalama wa nchi.

Chama hicho kimesema hakitashiriki katika semina hiyo wakati huu kwa kuwa kinasubiria hatua za Rais kuhusu mauaji ya kisiasa yaliyotokea katika mikoa mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Chadema, John Mnyika, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema chama hicho kimechukua hatua hiyo kikitambua umuhimu wa amani na usalama wa nchi na wajibu wa Jeshi la Polisi pamoja na Vyama vya Siasa katika kukuza demokrasia ya vyama vingi.

Mnyika alisema hatua hiyo imefikiwa kufuatia utendaji dhaifu na wa kipropaganda unaoonyeshwa na Tendwa uliosababisha Kamati Kuu ya Chadema kumtangaza kuwa ni adui wa demokrasia na hafai kuwa katika nafasi aliyo nayo.

“Kamati Kuu iliazimia kuwa pamoja na kuendelea kuheshimu sheria ya vyama vya siasa, Chadema haitashiriki shughuli zozote zitakazosimamiwa na John Tendwa hadi hapo atakapoondolewa katika nafasi yake na kuteuliwa msajili mwingine,” alisema.

Alisema Kamati Kuu ya Chadema ilifanya kikao maalumu Septemba 9 mwaka huu kilichojadili hali ya siasa nchini kufuatia mfululizo wa mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi katika shughuli za kisiasa za Chadema na mipango ya baadhi ya viongozi wa Serikali ya kudhibiti Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) kwa mbinu haramu.

“Katika majadiliano ya kina kabla ya kufikia maamuzi Kamati Kuu pamoja na mambo mengine ilieleza kusikitishwa na kauli za kisiasa ambazo zimekuwa zikitolewa na Tendwa, zenye mwelekeo wa kukibeba Chama Cha Mapinduzi ( CCM) na serikali,” alisema.

Source:Nipashe Ijumaa
 
Safisana.Sasa kama anataka kikifuta chama anachodai nicha vurugu na mauwaji ya nini awaalike katika vikao?Hakuna kutoa ushirikiano kwa watu kama hawa.
 
Back
Top Bottom