Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Tukubalianeni kabisa kuwa uchaguzi umemalizika kwa salama,kama ni mechi ndio imekwisha na mshindi ameshatangazwa ,ikiwa ni rufaa basi wa kushitakiwa na kukabwa ni refa na sio mshindi ,ndivyo mambo yalivyo siku hizi.
Yale mambo ya lurudiwa mechi hayapo tena au tuseme yameshapitwa na wakati,Kikwete ametangazwa na ameshaunda serikali na sasa wamo katika kutekeleza sera zao na mikakati ya miaka mia ijayo.
Makelele au malalamishi ya kusema Kikwete sio Raisi halali hayana mshiko kwani tuelewavyo tume ikishatangaza kwa maneno ya Uswahilini ndio tunasema imeshatoka.
Mtihani ambao sio mdogo, ni wa kuhakikisha kuwa Katiba na tume vinabadilishwa kwa haraka sana na kila anepinga mabadiliko hayo huyo atangazwe rasmi kuwa ni adui wa Taifa hili la Tanzania.
Hapa tulipo baada ya mayowe ya siku mbili tu ,tayari wapingaji wameshaanza kutapatapa na wanachomoza kila pembe kuleta madai ya kuwa ni gharama kubwa kubadilisha Katiba na tume yake ,wengine wakidai kwa sasa hakuna au suala hilo halina umuhimu.
Kwa kuanzia kauli hizi ndio za kuanza nazo na kuzipinga kwa hali na mikutano na maandamano ya hapa na pale .kuzipinga kauli zenye kukatisha tamaa kama hizi na sio ziachwe ziote mizizi ,musisubiri nikimaanisha vyama vya upinzani viwe vyenye kutoa kauli nzito kupinga maadui hawa,pale wasemapo tu basi wasipewe muda wakazua jingine ,maana vyama vya upinzani vimetoa kauli za kutraka mabadiliko ,serikali na wasemaji wa CCM nao hawakusubiri wakarusha baruti zao,sasa hizi baruti ni lazima zisambaratishwe kwa kauli za papo kwa papo.
Tunasema tunahakikisha tunaingia kwenye uchaguzi 2015 na Katiba mpya na tume mpya.