Chadema wacheni makelele ,tujenge nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wacheni makelele ,tujenge nchi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwiba, Dec 19, 2010.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tukubalianeni kabisa kuwa uchaguzi umemalizika kwa salama,kama ni mechi ndio imekwisha na mshindi ameshatangazwa ,ikiwa ni rufaa basi wa kushitakiwa na kukabwa ni refa na sio mshindi ,ndivyo mambo yalivyo siku hizi.

  Yale mambo ya lurudiwa mechi hayapo tena au tuseme yameshapitwa na wakati,Kikwete ametangazwa na ameshaunda serikali na sasa wamo katika kutekeleza sera zao na mikakati ya miaka mia ijayo.

  Makelele au malalamishi ya kusema Kikwete sio Raisi halali hayana mshiko kwani tuelewavyo tume ikishatangaza kwa maneno ya Uswahilini ndio tunasema imeshatoka.

  Mtihani ambao sio mdogo, ni wa kuhakikisha kuwa Katiba na tume vinabadilishwa kwa haraka sana na kila anepinga mabadiliko hayo huyo atangazwe rasmi kuwa ni adui wa Taifa hili la Tanzania.

  Hapa tulipo baada ya mayowe ya siku mbili tu ,tayari wapingaji wameshaanza kutapatapa na wanachomoza kila pembe kuleta madai ya kuwa ni gharama kubwa kubadilisha Katiba na tume yake ,wengine wakidai kwa sasa hakuna au suala hilo halina umuhimu.

  Kwa kuanzia kauli hizi ndio za kuanza nazo na kuzipinga kwa hali na mikutano na maandamano ya hapa na pale .kuzipinga kauli zenye kukatisha tamaa kama hizi na sio ziachwe ziote mizizi ,musisubiri nikimaanisha vyama vya upinzani viwe vyenye kutoa kauli nzito kupinga maadui hawa,pale wasemapo tu basi wasipewe muda wakazua jingine ,maana vyama vya upinzani vimetoa kauli za kutraka mabadiliko ,serikali na wasemaji wa CCM nao hawakusubiri wakarusha baruti zao,sasa hizi baruti ni lazima zisambaratishwe kwa kauli za papo kwa papo.

  Tunasema tunahakikisha tunaingia kwenye uchaguzi 2015 na Katiba mpya na tume mpya.
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Dhamira yako Mwiba ni nzuri, ila mbinu unayopendekeza ndiyo inayoonekana kupinda; kwani ili hayo madai ya katiba mpya yaweze kuungwa mkono na wote, kunahitajika kujengwa hoja madhubuti inayoonyesha wazi mapungufu ya katiba tuliyo nayo. Hoja hiyo haiwezi kujengeka bila ya kuonyesha ni kwa kiwango gani, katiba ya sasa imechangia katika kuminya uhuru wa wananchi katika kuchagua viongozi wawapendao.
   
 3. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nchi haijengwi kwa matofali ya theluji. Yaani haijengeki kwenye msingi wa uchakachuaji. Chademe hawana makelele. Wenye makelele ni ccm hawajajua hatma yao. Kifupi wamezingirwa hajengi mtu ni bomoa nchi wote tuwe wakimbizi
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nchi ipi unayozungumzia? Sie tunazungumzia habari za nchi yetu Tanganyika. Wewe na mmeo endeleeni kuijenga zenji. Tuachieni mstakabali wa Tanganyika yetu. You have no right to speak on Tanganyika affairs!
   
 5. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  well done,
  Tupo pamoja kuidai Tanganyika yetu,
   
 6. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,638
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Kumbe hata CUF mnataka katiba mpya!
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuuu sasa kikwete ni raisi wa muungano au tanganyika?? Na je tanganyika raisi wake ni nani?? Mi huwa nachanganyikiwa na haya mambo, au sielewi tanganyika iko wapi masikini tanganyika yangu! Mbona mwiba anashabikia zanzibar yao mimi tanganyika uko wapi?? Kuna siku utarudi tanganyika au ndo uchakachuaji tuu!?
   
 8. c

  chelenje JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yap! mkuu, hapa tuna-deal na Tanganyika tu, Zenji kivyao...:embarrassed:
   
 9. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mwiba ni fisadi la ccm
   
 10. D

  DENYO JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mwiba unazungumza usichokijua kimsingi naona unaropoka na kukurupuka tuuu-madai ya chadema na kila mzalendo -watu wenye fikra finyu na malengo binafsi ndio wana mawazo kama yako. Hutuwezi kumtetea mnyongaji na dictator eti kwa sababu mechi imeisha. Si vema unavyochukulia kirahisi eti mechi imeisha...sawa amefanya mapinduzi ya kijeshi na kubadili matokeo lakini kwa faida ya nani? Yaani ameshinda kwa nguvu ya dola kwa manufaa ya nani?? Ndio maana chadema anawakilisha umma kudai katiba na watanzania sio mabwege tena tunajua haki zetu
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ninaposema wacheni makelele basi msilete uswahiba kama baadhi yenu mnavyoonekana kana kwamba ni wapenzi wa dhati wa Chadema kumbe ni wale msioitakia mema.Wengi wa wakuu wa Chadema wameonekana kuelewa hali tuliyonayo na baadhi ya kauli zao za kuitaka serikali kushiriki katika baadhi ya mambo.

  Nilitegemea Wabunge wa Chadema wangelikataa kuingia kwenye bunge hadi pale madai yao yatakapo sikilizwa hilo halikufanyika wala halikujaribiwa ,kwa maana hiyo uhalali wa wao kuwepo ndani ya bunge na kugombania kuwa chama pinzani ni kukubali na kuikubali serikali iliyopo madarakani.

  Sasa kuwepo kwa wingi kwa wabunge wa upinzani na kushirikiana katika hoja za maana na zenye kuwezesha uwepo wa muamsho wa kudai katiba mpya na tume mpya ,hapo bungeni sio mahala muafaka lakini ndipo ambapo cheche za kudai mabadiliko zinapohitaji kuwashwa na baada ya hapo ni kuzifikisha kwa wananchi ili kutoa msisimko kwa wananchi na kuwaelewesha kwa kina umuhimu na faida za kuwepo katiba mpya.

  Mabadiliko yakatiba ndio ngao ambayo itailinda Tanzania isizidi kuyoyoma katika mabonde ya umasikini,ni mwega ambao WaTanzania wategemea ili kuvuta pumzi na kutweta ili kujipanga kwa kuijenga Tanzania mpya.

  Sasa ikiwa leo wengine watajiona ni wao tu basi mjue CCM itakuwa haina shida kubwa zaidi ya kutugonganisha vichwa.
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni wapi Chadema imewakilisha umma ? Ni uma gani umeituma Chadema mbona ndugu unapotea kiasi hicho ? Madai ya Katiba usiyapeleke upande wa Chadema au CUF au kwenye Chama chochote kile ,kama tujuavyo hili jambo la katiba haliwahusu Chadema au CUF peke yao ,hili ni suala nyeti na linamhusu kila mzalendo wa Taifa hili la Tanzania ,sasa unapolichukua na kuliweka Chadema peke yake utakuwa unakosea kwani WaTanzania wote si Chadema ,upo ndugu mwananchi ?

  Madai mazito kama haya yanahitaji umoja tenaa umoja wa kweli ulio na msimamo thabiti,usio tetereka wala kuwagawa wananchi kama ambavyo mnalivutia suala hili upande wenu ,kusema Chadema ndio wameanza hapo mtakuwa mnakosea sana sana na haifai kabisa kusema hivyo. Tuwe wamoja katika kupeleka maddai haya na kuwashawishi wananchi wayapokee bila ya kujali itikadi za kichama.
   
 13. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mafisadi wa ccm kwa pumba bana hamuwezekaniki
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Du stinkst wie ein Ziegenbock!
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Duuuhhhh mwiba umekwisha. We tuachie Tanganyika yetu. Kaa kwanza Zenji yenu ili sie huku tumalizane kwanza ndipo tutakuita unasikia wee Ziegenbock?
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  kipoipoi kajibinda unkweda kibumbuten
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tanganyika ipi unayoizungumzia ??
   
 18. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #18
  Dec 21, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Acha unafiki, wewe huu si muda wa kuyasema hayo si tumeshawachoka na hizi dhuluma za CCM
  .
   
 19. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #19
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Tanganyika ni nchi huru iliyopata uhuru wake tarehe 9/12/1961 kutoka kwa waingereza,nchi hii ipo Africa mashariki na kati.Tanganyika ilikuwepo,ipo na itaendelea kuwepo daima na milele,hakuna awezaye kufuta historia ya Tanganyika.CCM wamejalibu kufanya ujinga huo lakini wameshashindwa vibaya!!!
   
 20. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hakuna awezae kuifuta Tanganyika ? Sio ipo ilikuwepo !! Imesita kuwepo Historia haifutwi bali inabakia kama ilivyo Tanganyika imebaki kwenye historia ,yaani sasa mnachezea Muungano ???

  Nyie Chadema vipi ? Au mmechanganyikiwa ? Yaani hamueleweki mala Katiba mala uchaguzi mra Tanganyika,haya tuwasikie kwenye majukwaa mkisema Tanganyika ni Nchi ,hapo ndio nitakubaliana.
   
Loading...