Elections 2010 Chadema wacheni makelele ,tujenge nchi

Kwa muundo ulivyo Tanganyika ilpotezwa ndani ya muungano. Zanzibar imebaki na hadhi yake ingawa kivuki kama nchi. Tanganyika hata hicho kivuli haina. Kimtazamo naona katiba mpya kwanza iipe Tanganyika hadhi yake ndo mengine yaendelee.
 
Well said Mwiba, katiba mpya ilianza kuzungumzwa zamani na wazalendo wa nchi hii hasa wanasheria, kuanzia tume ya Nyalali, Kisanga, n.k hatimaye CUF waliichukua na kutengeneza "draft katiba" ...wakati chadema walikuwa pembezoni sana kwenye siasa za Tanzania..

Thank God sasa wana stake kwenye siasa sote twende kwa pamoja tudai tume huru, katiba mpya, yenye kupunguza na kudhibiti madaraka ya Rais wa nchi...zinduka tutafika
 
"Tukubalianeni kabisa kuwa uchaguzi umemalizika kwa salama,kama ni mechi ndio imekwisha na mshindi ameshatangazwa ,ikiwa ni rufaa basi wa kushitakiwa na kukabwa ni refa na sio mshindi ,ndivyo mambo yalivyo siku hizi.

Yale mambo ya lurudiwa mechi hayapo tena au tuseme yameshapitwa na wakati,Kikwete ametangazwa na ameshaunda serikali na sasa wamo katika kutekeleza sera zao na mikakati ya miaka mia ijayo.

Makelele au malalamishi ya kusema Kikwete sio Raisi halali hayana mshiko kwani tuelewavyo tume ikishatangaza kwa maneno ya Uswahilini ndio tunasema imeshatoka"

kwanza nianze na samahani kama nitakosea, hivi mtu kujaribu kutetea ukweli kwa kukemea mabaya ni dhambi au ni kosa. Hv bila kuwatingisha hawa CCM unafikiri kuwang'oa ni kazi rahisi.CCM Ni jabali. Halafu hata tume ni yenye kuegemea upande mmoja kwani siyo huru pia ni Rais aliyeiunda. la maana hapo ni kupata katiba yenye kupinga utawala huu wa kiimla unaompa Rais mabavu. Tuone kama mtu atalalamika maana hata wananchi hawana imani na tume mfano ni Moshi vijijini watu wanalalamikia tume kwa kutoa matokeo ya uongo yenye lengo la kuinufaisha CCM bila ya kuangalia maslahi ya watu wa huko ambao walimchagua Antony C. Komu kwa ridhaa yao.
 
Back
Top Bottom