CHADEMA waanzisha operation inaitwayo futa, delete kabisa CCM

CHADEMA waanzisha operation inaitwayo futa, delete kabisa CCM

Hakuwa na maana hiyo alitaka kujibu mafanikio ya M4C yalivyowachanganya magamba wakafikia hatua ya kuua watu ovyo na mlaaniweeee!!

Mbone unamsemea kwa kumlisha maneno??? Yeye kasema kifo cha Mwangosi ni moja ya mafanikio ya M4C. Wewe unakurupuka huko maliwatoni na kuja kukana kuwa hajamaanisha hivyo??? Sasa tumsikilize nani? Acha hizo banaaa. Huo umbea wa kuwasemea watu haukubaliki.
 
Viongozi wa chadema ni wajanja sana. Wanatengeneza mazingira ya kulipana posho walizokosa BMK.

Umenifungua akili sana. Kumbe ndo mpango.

Hilo ni kama lile picha la mbowe aliyerudisha gari la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni asubuhi mbele ya waandishi wa habari, kisha usiku akazikacha kamera na kwenda kulichomoa kimyakimya. Ni shida tupu. Yaan tanzania hakuna upinzani...

Wamejaa wachumia matumbo watupu.
 
Hakika hawa CHADEMA ni walaghai sana. Ukiona Operesheni inaanzishww basi ujue kuna mpunga wa maana umepigwa mahala fulani hivyo wwnataka kuhalalisha matumizi yake

Asante kwa kututonya kuna ka ukweli flani
 
mhh Msalani umeamka?? anza na hili bomu apa usijiweke upofu

SERIKALI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imegeukia kutekeleza sera kutoka katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), licha ya awali kudai sera hizo ni ndoto za mchana zizizotekelezeka.

Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010, wapambe wa timu ya kampeni ya mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete, walimbeza aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa kuhusu sera hizo ambazo sasa wamezigeukia na kaunza kuzitekeleza.

Awali, Serikali ya Rais Kikwete ilianza kubeba sera ya elimu ya CHADEMA wakati wa kipindi chake cha kwanza, pale alipoamua kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma.

Ilani ya CHADEMA ya 2005/2010, inaeleza kuwa kama wangechaguliwa kuongoza serikali, wangejenga vyuo vikuu kila kanda ya nchi ikiwemo kanda ya kati ambapo chuo hicho kingejengwa mkoani Dodoma.

Rais Kikwete alikiri kwamba wazo hilo halikuwemo katika ilani ya CCM lakini kutokana na umuhimu wake, aliona busara ya kulibeba na kulitekeleza na sasa chuo hicho kinaendelea kutoa elimu ya juu kwa
Watanzania wengi.

Kwa mara ya pili, mwaka 2011, baada ya uchaguzi mkuu, Rais Kikwete alibeba sera ya katiba mpya kutoka CHADEMA na vyama vingine vya upinzani, ambavyo viliahidi kuandika katiba mpya vikiingia madarakani.

Mathalani CHADEMA katika ilani yao ya uchaguzi 2010/2015, waliahidi kuanzisha mchakato wa katiba mpya ndani ya siku 100 ili kuweka mazingira bora ya maridhiano na kutafuta muafa wa kitaifa wa kuwezesha kuandikwa kwa katiba inayokidhi matakwa ya wananchi.
Lakini serikali ya CCM baada ya kubeba sera hiyo, ghafla Rais Kikwete aliridhia mchakato uanze huku kukiwa hakuna maridhiano ya pamoja hata ndani ya chama chake na kitaifa kuhusu masuala nyeti kama muundo wa muungano.

Suala hili ndilo linatajwa kukwamisha mchakato huo wakati huu ukiwa katika ngazi ya Bunge Maalum la Katiba kutokana na msigano mkali wa muundo wa muungano, ambapo maoni ya wananchi kwenye rasimu ya katiba yanataka serikali tatu lakini CCM inataka serikali mbili.

Mwaka 2012, Halmashauri Kuu (NEC) na CCM iliazimia kuishauri serikali iangalie uwezekano wa kushusha gharama za vifaa vya ujenzi ili kuwawezesha wananchi kujenga yumba bora na za kisasa.

NEC ilikiri kwamba kwa jinsi gharama za vifaa zilivyo kubwa, wananchi wengi hawamudu kujenga nyumba bora za makazi.

Hata hivyo, uamuzi huo wa CCM uliibua mjadala kwa wananchi, wakidai imekuwaje suala hilo liwezekane sasa wakati chama hicho kiliendesha propaganda wakati wa uchaguzi mkuu kumpinga Dk. Slaa kwamba anapotosha watu kuhusu upunguzwaji wa bei za vifaa hivyo.
Kuhusu uendelezaji makazi na nyumba, Dk. Slaa alisema kuwa serikali ya CHADEMA itavunja Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kutokana na kushindwa kuleta mabadiliko ya makazi ya watu kama ilivyokusudiwa.

Badala yake Serikali ya CHADEMA itaunda Mamlaka ya Taifa ya Uendelezaji Makazi na Nyumba (National Housing and Residence Development Authority) ambayo itakuwa na nguvu na muundo utakaowezesha kusimamia ujenzi katika makazi ya watu, miundombinu, na ubora wa makazi hayo ili yaendane na maisha ya kisasa.

Dk. Slaa aliahidi kuwa CHADEMA wangeanzisha Mpango wa miaka kumi kuanzia 2010-2020 wa Uendelezaji Makazi ya Taifa (National Housing Development Plan) utalenga kuhakikisha kuwa; ujenzi wa nyumba za matope, fito na nyasi unatoweka nchini ifikapo mwaka 2020.
Kiwango cha chini cha nyumba yoyote inayojengwa itakuwa ni nyumba ya matofali ya kuchoma na yenye kuezekwa bati. Hivyo, tutaandika sheria mpya ya ujenzi ili kuanza kukidhi mahitaji ya teknolojia ya kisasa pamoja na kufanya majengo yetu yawe ya kisasa kwa kila hali.

Agosti 26 mwaka huu, akiwa mkoani Morogoro, Rais Kikwete alisema kuwa serikali inaangalia uwezekano wa kufuta ada katika shule za sekondari, kama namna ya kuboresha Sera ya Elimu na kuhakikisha kila mwanafunzi anayeanza darasa la kwanza anamaliza kidato cha nne.

Kauli yake inapingana na ile aliyoitoa mwaka 2010 wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu akiwa jimboni Peramiho mkoni Ruvuma, akikataa sera ya mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Slaa kuhusu elimu ya bure.

“Serikali haiwezi kutoa huduma za jamii bure…Nimebahatika kukaa serikalini muda mrefu. Hiyo sera ya elimu bure tulijaribu na ikatushinda; na wakati huo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, tulikaa naye tukaona haiwezekani, tukaamua tubadilishe. Sasa nawashangaa wenzetu wanawadanganya eti watatoa bure,”alisema Kikwete.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaitafsiri kauli ya Rais Kikwete kukubali elimu ya bure kama propaganda za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu kwa sababu wanahoji utekelezaji wake kwa sasa wakati halimo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM 2010/2015.

Kuhusu elimu, CHADEMA iliahidi kuwa itatilia mkazo sana ubora wa elimu badala ya bora elimu kwa kuwa inaamini elimu bora ni walimu bora.
Hivyo basi, itaweka mkazo katika kuwapatia walimu mafunzo bora na ujira stahiki ili waweze kuwa na maarifa ya kutosha na kutulia mashuleni.

“Tutaweka mkazo katika kuwapatia watoto wa shule kiwango cha juu katika elimu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu. Mkazo utawekwa katika kuhakikisha kuwa shule na taasisi zote za elimu zinatoa elimu inayochochea fikra, udadisi, maarifa na ugunduzi na inayoibua vipaji.
Kuhusu Elimu ya Msingi na Sekondari, CHADEMA ilisema itadili mfumo wa elimu ya msingi ili iweze kujitoshekeza kwa kuhakikisha kuwa wahitimu wanapata maarifa na stadi za maisha zitakazowawezesha kujitegemea kimaisha.

Ili kufikia adhima hii, muda wa elimu ya msingi utaongezwa kutoka miaka saba (7) hadi miaka kumi. Hii inamaanisha kuwa watoto watamaliza shule wakiwa na umri wa miaka 16/17, umri unaomwezesha kuanza maisha ya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi na kimataifa.

Mtaala wa elimu ya msingi utapanuliwa kwa kuingiza muhtasari wa kidato cha kwanza na cha pili cha sasa kuwa sehemu ya elimu ya msingi.

Kuhusu elimu sekondari itabadilishwa kutoka miaka sita (6) hadi minne (4) kwa kuunganisha mihtasari ya kidato cha tatu, nne, tano na sita kuwa muhtasari mmoja wa elimu ya sekondari. Hii itasaidia sana kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata sifa za kujiunga na elimu ya sekondari.

“Elimu ya ngazi ya msingi na sekondari itagharamiwa na serikali kuu pamoja na serikali za mitaa. Lengo ni kuhakikisha kuwa elimu hii ya msingi kabisa inakuwa ni haki kwa kila mtoto wa Kitanzania na kiwango cha ubora kinalingana kwa nchi nzima,” inasema ilani ya CHADEMA.

Na katika kukabiliana na wimbi la utoro na usinziaji darasani kwa sababu ya njaa miongoni mwa watoto wa shule, Dk. Slaa serikali ya CHADEMA itarudisha utaratibu wa kutoa chakula cha mchana mashuleni, ambayo kitagharamiwa na serikali za halmashauri za miji na wilaya pamoja na serikali za mitaa na vijiji.

“Tutazihuisha na kuanzisha shule mpya za kitaifa za bweni za sekondari. Shule hizi zitachukua wanafunzi wote waliofanya vizuri zaidi katika mitihani yao ya mwisho ya elimu ya msingi. Katika kila mkoa kutakuwa na angalau shule moja ya kitaifa itakayochukua wanafunzi kutoka katika mikoa mingine kwa lengo la kujenga utaifa na uzalendo miongoni mwa wanafunzi.

“Na CHADEMA itarejesha utaratibu wa usafiri wa “Warrant” kwa wanafunzi hao ili kuondoa makali ya gharama za nauli kwa wazazi. Ni wazi kuwa utaratibu huu ni ghali, lakini kuua utaifa ni ghali zaidi,” alisema Dk. Slaa.

Katika kupanua wigo na kuboresha elimu ya juu, Serikali ya CHADEMA itaanzisha mfuko wa elimu uitwao “Uhuru Scholarship Fund” kwa ajili ya kugharamia masomo katika chuo kikuu cha umma kwa wanafunzi wanaofaulu katika kiwango cha Daraja la I na II.
Huu hautakuwa mkopo kwa kijana yeyote ila atalipiwa Chuo kwa kadiri ya kwamba anaendelea kufikia viwango vya juu vya kitaaluma kwa mujibu wa taratibu kwa muda wote atakaokuwa chuoni.

Kwa wanafunzi ambao watafaulu madaraja mengine (daraja la tatu na la nne) mfumo mpya wa kugharimia elimu ya juu utawekwa ili kuhakikisha kuwa gharama ya elimu ya juu haiwi kizuizi kwa kijana yeyote anayetaka elimu ya Chuo Kikuu.

CHADEMA ilisema kuwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu itavunjwa kutokana na uendeshaji mbovu, badala yake serikali itaunda chombo kipya cha utoaji na usimamizi wa mikopo ya elimu ya juu ambacho kitajulikana kama Mamlaka ya Taifa ya Kugharimia Elimu ya Juu (Tanzanian Higher Education Financing Authority – TAHEFA).




M4C imeishia wapi?
 
Outsiders wanatoa uchungu kwasababu nyie wa ndani mmeshaambiwa kuwa,
KAPU LA MJANJA, MJINGA HATII MKONO'.
Acheni wajanja wapige hela kila siku kwa kuja na mbinu zilezile za oparesheni zisizoeleweka ila sisi hatutachoka kuwasemea nyie MAZWAZWA mlioshindwa kujitambua.
Serikali inayotoa pesa ya ruzuku kwa CHADEMA, kwa kuwa CHADEMA ina tija kwa Taifa.

Vinginevyo, ipigie kelele serikali dhaifu inayoruhusu pesa zake ziende pasipo tija.
 
Back
Top Bottom