CHADEMA & UKAWA walitikisa Jiji la Mwanza

CHADEMA & UKAWA walitikisa Jiji la Mwanza

Nicolas J Clinton Gabone

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2014
Posts
892
Reaction score
536
Chama Cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA & UKAWA watakuwa kwa medani za jiji la Mwanza kesho kati ya hawa watakuwepo MBOWE, PROF SAFARI, LISU na MNYIKA medani ni kati ya FURAHISHA & MIRONGO PRIMARY. "UKAWA TUMAINI LETU"
====================

UPDATES
Wakuu leo chama pendwa Tz CHADEMA imetikisa jiji la Mwanza kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara ulifanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mbugani.
Katika mkutano huo mkubwa uliohutubiwa na Mwenyekiti wa BAVICHA taifa kamanda Pastrobasi Pascal Katambi,Naibu katibu bara na Zanzibar John Mnyika na Salum Mwalim na wengineo .

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya watu wa jiji la Mwanza ,mada kubwa zilizohutubiwa na viongozi hao wa kitaifa zilikuwa ni suala la rasimu ya katiba mpya,umuhimu wa kushiriki kwenye zoezi la uandikishaji wa daftari la kupga kura,kuwataka watu wajitokeze kwenye chaguzi za serikali za mitaa,unaotarajiwa kufanyika mwezi wa 12 mwaka huu.

Awali kabla ya mkutano huo wa wazi,ulitanguliwa na kongamano kubwa la vijana ,lililoandaliwa na BAVICHA Nyamagana na kufanyikia Tema hotel iliyopo Mkolani,ambapo katika kongamano hilo ambalo mgeni rasmi alikuwa mwenyekiti wa BAVICHA taifa,vijana walijengewa uwezo wa kushiriki kwenye chaguzi mbalimbali.

Viwanja vya mbugani vimejaa watu ni wengi sana hadi nafasi hakuna. Nnyika, Salum Mwalimu na Parobass Katambi wamefika sasa na uwanja unaendelea kujaa hakika Mungu ni taa ya UKAWA.

Gesi ya machozi inarushwa watu wanataaruki sasa maduka yanafungwa. Polisi wemejiandaa vyema watu wanapiga kelele, Viongozi wa UKAWA wanalazimishwa kuondoka bila maandamano baada ya watu kutaka kumsindikiza MNYIKA.

hawa ni baadhi ya watu waliopo mkutanoni
attachment.php

attachment.php

attachment.php
 
Mbona wa vyama vingine hawapo kwenye orodha yako? Mbona unalitumia vibaya jina la UKAWA?
 
Chama Cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA & UKAWA watakuwa kwa medani za jiji la Mwanza kesho kati ya hawa watakuwepo MBOWE, PROF SAFARI, LISU na MNYIKA medani ni kati ya FURAHISHA & MIRONGO PRIMARY. "UKAWA TUMAINI LETU"

Mbowe amerudi lini kutoka kula bata na warembo afrika kusini? Kesho ataongea pumba halafu akimbilie kujificha Dubai na warembo huku akitumbua pesa za ruzuku ya chama
 
Sasa hivi neno maandamano limekuwa chungu mdomoni mwa MACHADEMA
 
Mkuu, Mbowe karudi juzi na jana kahojiwa na BBC hata anachoongea hakieleweki. Nadhani alikuwa na hanging over za starehe za south.

Mbowe ni.kawaida yake kuongea pumba.. Ngoja kesho tuone kama ataandamana
 
NI SALAAM KWA MAREHEMU DOCTOR MVUNGI NA WAPAMBANAJI WOTE WALIOTANGULIA KUNAKO HAKI NA HABARI NJEMA KWA MZEE WORIOBA NA TUME YAKE YOTE TUKIZINGATIA ZAIDI 'UKAWA'NI TUMAINI KUU LA WATANZANIA WALIOCHOKA KUNYONYWA NA KABURU WEUSI.~~~~~~UKAWA KaZa!!!.
 
Hii post imevamiwa na laki si pesa na lizabon ni hatari alfu mjieshimu hapa si mahali pa matusi kama hamkulelewa na wazazi msiwape wengine laana zenu, mkome kuwatusi watu muwe na adabu mjitathimini na midomo yenu michafu.
 
Mbona wa vyama vingine hawapo kwenye orodha yako? Mbona unalitumia vibaya jina la UKAWA?

Ktk msafara wa Mamba na Kenge vipofu wanajiunga na wanajitia kimbelembele, wewe Gamba na UKAWA wapi na wapi, hata wakitaja Chama kimoja kilicho ktk UKAWA inaihusu wapi ccm kujinyea nyea kila UKAWA inapotajwa?
 
Ilianza UKAWA sasa ni CHADEMA+UKAWA??????
Hahaha unafiki huu ni hatari. Mwaka huu tutaona kila rangi zenu za unafiki. Nasikia mmemsajiri na Warioba?
 
Chama Cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA & UKAWA watakuwa kwa medani za jiji la Mwanza kesho kati ya hawa watakuwepo MBOWE, PROF SAFARI, LISU na MNYIKA medani ni kati ya FURAHISHA & MIRONGO PRIMARY. "UKAWA TUMAINI LETU"
siuoni ukawa hapo zaidi ya magwanda. acheni kujificha nyuma ya ukawa, jitambulisheni wenyewe kama magwanda.
 
Tunashukuru kwa taarifa kamanda,tuko pamoja. Viva ukawa,viva chadema.
 
Mkutano wa kesho ni wa Chadema na tayari umeanza kutangazwa, ila member wa UKAWA wataalikwa kwa ajili ya kuendeleza mashirikiano ambayo tayari yamekwisha kuanza. Watu wa CCM lazima muelewe kuwa uwepo wa UKAWA haujafuta uwepo wa vyama vya CUF,NCCR na CHADEMA wala shughuli zao za kujiimarisha kama vyama vya siasa, kimsingi UKAWA unahimiza kila chama kuendelea kuimarisha ngome zake ili kwa pamoja tuwe na nguvu ya kukabiliana na mafisadi CCM ifikapo uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
 
Ilianza UKAWA sasa ni CHADEMA+UKAWA??????
Hahaha unafiki huu ni hatari. Mwaka huu tutaona kila rangi zenu za unafiki. Nasikia mmemsajiri na Warioba?

Mkutano wa kesho ni wa Chadema na tayari umeanza kutangazwa, ila member wa UKAWA wataalikwa kwa ajili ya kuendeleza mashirikiano ambayo tayari yamekwisha kuanza. Watu wa CCM lazima muelewe kuwa uwepo wa UKAWA haujafuta uwepo wa vyama vya CUF,NCCR na CHADEMA wala shughuli zao za kujiimarisha kama vyama vya siasa, kimsingi UKAWA unahimiza kila chama kuendelea kuimarisha ngome zake ili kwa pamoja tuwe na nguvu ya kukabiliana na mafisadi CCM ifikapo uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
 
Mkuu Kwann unasema CHADEMA NA UKAWA, au cdm hako ndan ya ukawa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom