JokaKuu,..mbona Magufuli naye amesema aombewe?
..tangu anachukua fomu Magufuli amekuwa akisema aombewe.
..kwanini hukulalamika wakati huo, unalalamika sasa hivi?
Mkuu mnashangaa nyie lakini mimi hainishangazi kabisa. Na najua watu watasema mimi mdini lakini ndio hali halisi (Reality) na ndivyo Edo alivyo. Hakuomba aombewe tu ila kasema ni zamu ya Warutheli na ndio kauli yake!..Wengi wanamsikia tu hawajui ya Nigeria na Ujarumani..
Kama aliweza kurudisha shule na Hospital zilizojengwa na Mkoloni Mjarumani mikononi mwa kanisa lake atashindwa nini? Yeye Mrutheli, Mbowe sijui, Mtei sijui, Wakaskazini wengi sijui...kwa nini anapewa support kubwa hivyo sijui!. Panapofuka moshi kuna moto! Mimi ningependa tu kujua huyu Gwajima Askofu mzima ameingiaje katika uongozi wa Chadema au UKAWA hadi awe mshauri na msemaji wao?
- Unategema nini kitaandaliwa hapo? Nimeandika haya najua yatakuja mashambulizi ya hali ya juu kwa sababu watu hawatazami reality, wanataka kudanganyana na bikra ya ndimu! Udini upo mkuu wangu na hautakwisha kirahisi...
Tangazo la Serikali Na. 294 la tarehe 27/7/2015 chini ya kifungu cha 124A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, ukurasa wa 5 kifungu 2.1(k) kinasema:-Twende taratibu ni sek. ya ngapi anasema hayo maneno yaani hapo kwenye nyekundu?
Unafikiri mahali muafaka pa kujisafisha dhidi ya tuhuma za ufisadi ni jukwaani na sio kwenye vyombo vya sheria?
Na hii ndio shida tuliyo nayo watanzania. Kashfa ya Richmond imekuwa ni gumzo kwa miaka 8 kwa sababu tumekuwa ni watu wa kupiga makelele tu majukwaani halafu inaishia hapo! Vyombo vya dola (DPP, Polisi, TAKUKURU, etc..) hawajachukua hatua yoyote kwa miaka 8 huku watu wakiendelea kupiga kelele mtaani kuwa na "nyaraka" za ufisadi za Lowasa! Yeye mwenyewe ameshasema mwenye ushahidi dhidi yake aende mahakamani mbona mpaka sasa hakuna aliyekwenda ikiwamo Dr Slaa mwenyewe?
Leo hii naweza kwenda kwenye press nikakutuhumu wewe Galaxy S3 kwamba ni mwizi na nina nyaraka, halafu nakwambia kama unabisha njoo ukanushe ili niibue madudu zaidi (tishia nyau). Vyombo vya dola vinafanya kazi gani?
Na huu ndio utamaduni wa hovyo tuliojijengea kuwa ni watu wa kupiga kelele majukwaani huku wenye wajibu wa kuchunguza na kushitaki wakiwa likizo ndio tunapaswa kuupiga vita kabisa.
JokaKuu,
Ukweli utatuweka huru. Sikubalini kabisa na nadha ya kutumia 'dini' kama nyenzo ya kupata madaraka. Hilo moja.
Pili, kwa kumbukumbu zangu, hakuna siku hata moja Magufuli amehudhuria Ibada kanisani, akapanda madhahabuni, akachukua kipaza sauti na kuwaaambia waumini wengine kuwa wamuombee kwa sababu yeye ni wa 'dhehebu' lao. Na hakuna mahali Maguful amewachambua marais waliopita kwa dini zao ili kukazia 'sifa yake ya udini'.
Alichofanya Lowassa si kuteleza ni za mwizi 40 zimefika. Nitaeleza kwa kifupi sana.
Lowassa alikuwa kampeni meneja wa Kikwete 2005. Na Mkakati wake wa kutwaa madaraka kupitia kwa wanamtandao' ulijumuisha kwa kiasi kikubwa dhana ya udini. Lowassa alikuwa anazungukia majumba ya ibada kumnadi swahiba wake pamoja na kuchukua pesa (hasa temples za wahindi). Askofu Kilaini 'anasemekana' naye alikuwa mwanamtandao na ndio sababu akaja na ule msemo wake wa chaguo la mungu. Baada ya saga ya Richmond, Lowassa alianza kuunda mtandao upya kwa kutumia baadhi ya makanisa ya 'protestant' chini ya usimamizi za Gwajima.
Anachokifanya Lowassa sasa hivi ni 'activation' ya mtandao wake mpya ambao unafanana na kile alichofanya 2005. Na safari hii amekuja na sababu mahsusi, 'Ulutheri'. Na yeyote atakayejaribu kutia mchanga kitumbua chake atakutwa na kadhia ile ile iliyompata Dr Salim Ahmed Salim- character assassination.
..Lowassa ameshaomba radhi kwa suala hili.
..pia tume ya uchaguzi imemkemea kwa kitendo hicho.
..sasa tuondoke huko, turudi kwenye masuala yanayotuunganisha.
..humu JF wengine tumekuwepo kwa muda mrefu kidogo, hivyo tunajuana. kuna wenzetu ambao ni wadini kwelikweli and I can see kwamba wanataka mjadala wetu huu ukwame ktk hoja hii ya udini.
..CCM wako very efficient ktk hizi propaganda za udini, ukabila, na ukanda. angetokea mwana-CDM akafanya kile alichofanya Lukuvi kule kanisani chama hiki kingekuwa kimefutwa tayari. Lakini leo Lukuvi yuko ktk kampeni za Magufuli.
..I know what CCM are trying to achieve here. Lowassa put himself and Ukawa campaigns in a bad spot, he should have known better. But at the same time we are encouraged kwamba Lowassa ametoa tamko la kuomba radhi.
..I wish CCM na nyinyi mngekuwa waungwana kuomba radhi kwa kauli na matendo yenu. Kwa mfano kuomba radhi kwa kauli za Mzee Mkapa. Au kuomba radhi kwa umasikini, shida, na kero, ambazo zimesababishwa na utawala wenu mbovu wa miaka 35+.
NB:
Hii itakuwa ni post yangu ya mwisho kujadili hili tukio la Lowassa kanisani.
Alinda,Nimesema hivi kama Richmond ilizaa Dowans kwa maana hiyo Richmond na Dowans ni mikataba ya kifisadi, na haya maneno yanasemwa na serikali (Serikali nikiwa na maana ya Dr. Mwakyembe na Sitta ambao ni mawaziri tena ni wanasheria)
Sasa swali langu kwako au kwa mtu yeyote yule ni kama Richmond ni Lowassa ambayo ilizaa Dowans, Dowans inalipwa mamilion ya shilingi je ni kwanini serikali isisitishe mkataba wa Dowans na kuwachukulia hatua viongozi wote waliohusika na mikataba hewa hiki kigugumizi ni cha nini?
Ningeomba kupata ufafanuzi kutoka kwako....
Swala la Magufuli na nyumba, halihitaji mpaka Magufuli aibuke na kusema hivi au vile kunahitaji mimi na wewe kuhoji ni kwanini aliuza nyumba kwa bei ya kupwa na ni kwanini walihonga nyumba hizo kwa wake zake na wadogo zake? na si nyumba tu kuna hata bil 265 zimepotea katika wizara ya ujenzi, kuna kivuko kibofu cha bil.8 haya ni mambo ambayo hatuwezi kusubiri mpaka Magufuli kuibuka na sema maaana hawezi kuyasema bali ni wajibu wangu mimi na wewe kuhoji na kupata majibu kutoka kwake.
Na kama ndvyo kwa tusubiri mtu mpaka ibuke ndio tumuweke kikaangoni, Je kama Lowassa angekaa kimya inamaana hili Richmond lingepita tu bila kuhojiwa?
Thank youOut of Respect ya mjadala huu (mjadala mkuu), sitachangia chochote juu ya Lowasa na hiyo clip ya video.
Ukiwepo uzi wa Dhana ya udini na Uchaguzi 2015 ntakuja huko kuchangia. Udini sio suala la kuwa sub-topic, ni suala zito ambalo halihitaji mihemko katika kujadiliwa. Na halijaanza leo kwa sababu hiyo clip ya Lowasa imeonekana.
Quality ya majadiliano inaondoka kukikosekana topic maalum inayojadiliwa. Ahsanteni.
Hapana. We loved Slaa but his wife loved him more. That is why I said do not read too much into it. Remember the King who abdicated to be with the woman he loves?Jasusi;
Kwanini tusi-read. Je inawezekana CDM wamemtosa Dr. Slaa kwa sababu mkatoliki?
Sijakuelewa unakata sek ya nini wakati unatakiwa kumuelewa msemaji! Hii hapa rudia kusikilizaTwende taratibu ni sek. ya ngapi anasema hayo maneno yaani hapo kwenye nyekundu?
Hapana mkuu huyu ni mgombea Urais wa kwanza kutumia lugha hiyo kwa hiyo msitake kupotezea wakati hapa tunazungumzia mtu ambaye anaweza kuwa rais wa nchi hii..Tusiyafumbie macho mambo haya kwa kutaka kuyaweka kiporo kwa sababu Udini upo nchini lakini hatutegemei mgombea Urais kuwa kinara wa fikra hizo..Out of Respect ya mjadala huu (mjadala mkuu), sitachangia chochote juu ya Lowasa na hiyo clip ya video. Ukiwepo uzi wa Dhana ya udini na Uchaguzi 2015 ntakuja huko kuchangia. Udini sio suala la kuwa sub-topic, ni suala zito ambalo halihitaji mihemko katika kujadiliwa. Na halijaanza leo kwa sababu hiyo clip ya Lowasa imeonekana.
Quality ya majadiliano inaondoka kukikosekana topic maalum inayojadiliwa. Ahsanteni.
Hapana. We loved Slaa but his wife loved him more. That is why I said do not read too much into it. Remember the King who abdicated to be with the woman he loves?
Hapana mkuu huyu ni mgombea Urais wa kwanza kutumia lugha hiyo kwa hiyo msitake kupotezea wakati hapa tunazungumzia mtu ambaye anaweza kuwa rais wa nchi hii..Tusiyafumbie macho mambo haya kwa kutaka kuyaweka kiporo kwa sababu Udini upo nchini lakini hatutegemei mgombea Urais kuwa kinara wa fikra hizo..
Twende taratibu ni sek. ya ngapi anasema hayo maneno yaani hapo kwenye nyekundu?