Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,250
- 44,578
Hili Swali nilielekeze kwa Mzee Mwanakijiji maana anaweza kutupa maelezo ambayo yanaweza mwanga kidogo..
Ni kwanini Dr. Slaa alimkaribisha Lowassa Chadema?
Sidhani kama hili ni swali sahihi; kama nijibu nadhani alilitoa mwenyewe na linaeleweka. Lakini kwamba "alimkaribisha" inadhania mambo mengi sana. Rejea majibu yake jinsi gani Lowassa aliomba kuingia lakini pia usisahau kuwa ushahidi mkubwa uliopo ni kuwa tayari Lowassa alishaanza dili ya kutaka kuingia CDM mapema sana kabla ya kukatwa CCM na mtu mhusika mkubwa hakuwa Slaa katika hili. Kimsingi hata kile kinachoitwa "kupitishwa" kwa Slaa kugombea ilikuwa ni geresha tu kwani kuna waliokuwa wanajua mapema dili wanalotaka kuchezewa lichezwe vipi. Slaa alikuwa ni chaguo lao la pili; chaguo lao la kwanza tunalijua sasa.
Asante sana GalaxyS3 kwa mchango wako nzuri ambao kwa namna moja au nyingine umenipa mwanga kuhusu ujio wa Lowassa ndani ya Chadema, pamoja na hayo bado sina mashaka na Dr. Slaa...
Kwanini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu:
Kwa jinsi Dr. Slaa alivyomueleza Lowassa jana, hivi kulikuwa na umhimu wa yeye kuwa "mposaji" wa Lowassa kuingia Chadema? Hivi hakuona kuwa kitendo cha Lowassa kuwa mwanachama wa kawaida tiyari kilikuwa kinatia doa kubwa ndani ya Chadema?
Na kama katibu mkuu anawajibu wa kulinda chama chake, kuhakikisha kuwa kila kiongozi anafuata maadili ya chama, hivyo basi inapotokea mtu anayetaka kujiunga na chama kwa minajri ya kugombea urais (kama ulivyoeleza hapo juu) lakini maadili yake ni machafu mtu huyu hakupaswa hata kujadiliana naye maana anaelewa kuwa ni fisadi na chama chake hakipokei mafisadi..Kwa hili tusimtetee Dr. Slaa tatizo limetoka kwake.
Na huu mjadala wa Gwajima Dr. Slaa na Lowassa hakuanza baada ya Lowassa kukatwa bali ulianza muda mrefu na ndio maana Gwajima alipompigia simu " alimwambia kuwa jamaa kakatwa" na Dr, Slaa akajibu niongee na Mwenyekiti kwa hii sentesi inaonyesha kuwa walishapanga kuwa akikatwa tu basi aje Chadema.
Nafikiri tuangalie haya mambo bila upendeleo unapompeleka mtu sehemu fulani iwe kwenye chama au kazini au sehemu yeyote ile basi ili apokelewa kutatokana na jinsi ulivyomuelezea kwa wanachama/au boss/Mwenyekiti wako. Haiwezekani leo ulete mwanachama ambaye anampango wa kuwa mwakilishi wa chama/kampuni yenu mwenye madoa doa na baaadaye usema "nimemleta nyie ndio waamuzi wa mwisho" Jamani kama ninafahamu fulani ni wezi/jambazi/fisadi tena fisadi kwanini nimpe hata nafasi ya kuongea na boss wangu?
Kama Lowassa angeletwa na mtu mwingine na Dr. Slaa akareact kama alivyo react jana ningemuelewa tena ningemtetea sana,
Kama Dr. Slaa hasingekuwa anamfahamu Lowassa vizuri juu ya ufisadi wake na akaja kufahamu baada ya kuwa ameishamtambulisha katika chama na hapo pia ningemuelewa lakini si sasa, alimfahamu vizuri kuwa Lowassa ni fisadi, alifahamu vizuri kuwa chama chake kinapingana na ufisadi na Lowassa na yeye ndiye alikuwa mpiga debe wa Lowassa kujiunga na chadema kuingia. Jamani jamani wanasiasa kuweni na aibu tena kwa watu wenye umri kama Dr. Slaa kwa kweli inasikitisha.
Mkuu sikuelewi kabisa unachotaka kusema. Unasema hakuna mahala Dr.Slaa amejadiliwa? hivi kweli una hakika na unayoyaandika au basi tu kutaka nifanya miye nmjinga saaana sijasoma hoja za watu kabla sijaandika hoja yangu. Mtu unaweza anzisha hoja maadam ipo katika misingi ile ile.Mkandara nadhani tuwe fair katika majadiliano.Ulivyoandika hapo juu ni kwa mwelekeo wa kukusanya watu wote kwa pamoja. Kama unafuatilia uzi, watu wanapingana kwa hoja na wamekuwa fair kwa kila mmoja
Pili, si vema ukapandikiza maneno. Ukitusoma hapo nyuma hakuna mahali Dr Slaa alijadiliwa hadi leo.
Nipo katika rekodi ya uzi huu nikiandika hivi Uamuzi wa DrSlaa kukaa pembeni uheshimiwe. Ni mtu aliyekitumikia chama chake hata kufikiamahali pa kuweka maisha yake rehani. Vijana wanaoandika katika mitandao waachemara moja.
Hao iwe ni wa M4C au Team Lowassa. Dr Slaa anastahili kuheshimiwayeye na maamuzi yake. Apewe muda wa kutahmini hali yake ya baadaye. Uamuzi atakaouchukua uheshimiwe
Hayo maneno tumeandika mwezi mmoja uliopita. Sasa unapokuja na tuhuma za watu kusema ni msaliti au mungo si kweli
Hapo juu tumesema, tutatumia maneno yake katika kupima alichosema bila kumuonea au kumhurumia.
jitegemee kaleta point, pamoja na za wengine kama akina Alinda n.k.
Tutazitumia si kutuhumu, si kujibu bali kufanyia uchambuzi.
Ni kama ule wa hotuba ya UKAWA jangwani
Tujadili issue kama zilizvyo na si kama tunavyowahisi wenzetu au hisia zinavyotutuma
Sidhani kama hili ni swali sahihi; kama nijibu nadhani alilitoa mwenyewe na linaeleweka. Lakini kwamba "alimkaribisha" inadhania mambo mengi sana. Rejea majibu yake jinsi gani Lowassa aliomba kuingia lakini pia usisahau kuwa ushahidi mkubwa uliopo ni kuwa tayari Lowassa alishaanza dili ya kutaka kuingia CDM mapema sana kabla ya kukatwa CCM na mtu mhusika mkubwa hakuwa Slaa katika hili. Kimsingi hata kile kinachoitwa "kupitishwa" kwa Slaa kugombea ilikuwa ni geresha tu kwani kuna waliokuwa wanajua mapema dili wanalotaka kuchezewa lichezwe vipi. Slaa alikuwa ni chaguo lao la pili; chaguo lao la kwanza tunalijua sasa.
Alomleta Lowassa Chadema siwezi kumjua zaidi ya mhusika mwenyewe isipokuwa nasema hawezi kuwa Dr.Slaa kwa maelezo ya Tundu Lissu kwa sababu katika maelezo yake uongo umejitenga wazi kabisa..hebu twende taratibu bila jazba.. Ni nani aliyemleta Lowassa Chadema? na kwanini?
Kwa kiwango kikubwa pia ninaweza kukubaliana na fikra za Zakumi katika bandiko lake la #463 anaposema inawezekana Mbowe na Dk. Slaa walizidiana kimaslahi." Tulikuwa tukiambiwa tu kwamba kuna mtu mzito atajiunga na Ukawa. Tusubiri. Sasa mtu huyo nani tukawa hatuambiwi. "Kulikuwa na fununu tu nyingi kwamba ni Lowassa lakini hakuna aliyesema" alisema Makaidi. Mbowe aliwataka wenzake ndani ya Ukawa kutoharakisha kumtangaza mgombea wao kwani "muda ulikuwa unaruhusu".
Raia Mwema - Lowassa alivyoingia Ukawa
Mwanasiasa mmoja wa Uingereza aliwahi kusema 'siku moja ya siasa ni muda mrefu sana'
Pamoja na unayosema, kuna jambo moja umesahau. Mbona mengi tuliyoongea hapa yanatokea sasa hivi?
Kwasisi wengine 'maandishi yanatimia'
Dr Slaa ametumia haki yake ya kujieleza. Hakuwa na njia nyingine bali kujieleza tu ili abaki na kile anachosema ni credibility. Ameeleza mengi na ana haki hiyo kama walivyo na haki wengine kwa upande mwingine
Tunazidi kupata undani wa nini kilitokea na kwanini.
Tunaweza kusema kwa ufupi, hii ni collateral and colossal damage ya kiwango kikubwa sana kwa UKAWA
Yapo mengi sana yasiyoonekana, inatosha kusema kwa ufupi hayo
Mkuu za siku tele. Bila kupoteza muda, najikita kwenye hiyo redbold.
Nimemsikiliza Dr. Slaa, toka anaanza mpaka anamaliza kujibu maswali. Leo sikutaka kuhadithiwa wala kuwekekewa clips zilizokatwa katwa, ilinifanye tathimini sahihi.
Nadhani si kweli kusema Dr. Slaa hakuwa na shida na ufisadi wa Lowassa. Ninadhani hivyo kwa sababu wakati anaanza kutoa maelezo juu ya kumkaribisha Lowassa alitoa masharti ya kimsingi ambayo alitaka Lowassa ayatekeleze. Baadhi ya masharti hayo ni haya:
1. Lowassa atamke hadharani kuwa ameachana na CCM
2. Lowassa ajibu tuhuma hadharani tena kinagaubaga kwa kusema wazi nani alihusika na Richmond na kashfa nyingine zianzomuhusu yeye Lowassa (Badala ya kusema mwenye ushahidi apeleke mahakamani ama mfunge midomo. Pia suala mahakamani haliwezekani kwa raia wa kawaida , Dr Slaa kasema, kesi za jinai ni serikali ndiyo ufungua mashitaka)
3. Akisha maliza kujisafisha (Lowassa), atangaze anaamia chama gani(Chadema ama chama kingine!);
4. na kisha kama ameamua kuamia chadema, basi chama(Chadema) kiamue kumpokea ama la...!Baada ya kujiridhisha kama Lowassa ni Asset kisiasa(atakuja na viongozi na wabunge wa CCM ambao nao watafuata utaratibu wa 1-3 hapo juu) ama ni Liability kisiasa.
Hivyo nadhani Mkuu, Alinda, si sahihi kumuhisi Dr. Slaa hivyo(redbold).
Binafsi, nadhani kwa kiasi fulani Dr. Slaa alikuwa nafanya siasa sahihi zisizo za kilaghai (siasa za ukweli). Siasa zisizo za kilaghai ndizo zilizonivutia kufatilia maadishi mengi ya Nguruvi3, ya kwako(Alinda) na wengineo hapa jukwaani.
Nadhani kwa leo Dr. Slaa kazitendea haki siasa nilizoziamini na ninazozidi kuziamini yaani siasa za ukweli na wala si siasa za kitapeli.
Mapambano bado yanaendelea kutafuta na kisha kuupata ukombozi wa kweli kwa kufuata siasa za ukweli.
-TUJITEGEMEE.
@Ng'wamapalala kuna hoja hapo, unaweza kutusaidia?Wana duru, naomba kuulizahivi Mchungaji Gwajima ana mamlaka gani ndani ya Chadema mpaka wamruhusukushiriki kuwachagulia mgombea urais.
Na tatizo la Dr.Slaa na Lowassa ni kakaribishwa Chadema kama mwanachama wakawaida au kusimamishwa kama mgombea urais wa Chadema.
Ahsanteni.
Swali la msingi ni Je, Lowassa ni Asset ama Liability kwa CHADEMA??
Swali la msingi ni Je, Lowassa ni Asset ama Liability kwa CHADEMA??
Kwa mambo yanayotokea sasa hivi inahitaji utulivu sana kuamini hizi kauli za wanasiasa...
Kwa kauli alizozitoa leo na alizozitoa kipindi cha nyuma kuhusu Lowassa ni vigumu sana kuamini kwamba Dk. SLAA alianza kuzungumza na Lowassa kuanzia May....Hata uso wake tu Dk. SLAA unaeleza kila kitu...
Binafsi tangu mchakato wa kumuingiza Lowassa CHADEMA/UKAWA nimekosa kabisa imani na Mbowe...Lissu et al....Si wa kweli...Hasa walipokanusha kwa nguvu zote Lowassa kuhushuria CC ya CHADEMA kwa mara ya kwanza...
Hivyo nashawishika kuamini kwamba kauli nyingi alizoongea Lissu leo ni za kutunga....Hazina mashiko kwa kweli...
53.Nilifanikiwa kuijenga Chadema na ikawa tumaini jipya la watanzania.....Vijana wangu wa Chadema, naomba niwe mkweli propaganda imekivamia chama.
Hii sentensi zinaondoa credibility ya kiongozi bora, Chadema haikujengwa na mtu mmoja, wapo wengi tu ambao wamepigwa, wamekufa, wamefungwa, wamenyanyasika bungeni wote hawa na viongozi wengine na wananchi wamejenga Chadema na kuifanya tumaini kwa watanzania
....Bado sielewi Slaa anamaanisha nini
Naomba turejee kwenye kauli ya leo ya Mbatia.
Kama Dr. Slaa alikuwa chaguo la pili kwanin alikataa kutangazwa na Mbatia ile siku waliowawekesha waandishi wa habari? Akataka asubiri mbwembwe?
Tundu lisu amesema wazi kuwa Dr. Slaa alikuwa ameshachaguliwa mwezi wa kwanza akathibitishwa na chama mwezi wa nne. Mwezi wa tano the same Slaa akaanzisha mazungumzo na Lowasa.
Sasa alianzisha mazungumo na Lowasa ili aje kuwa mwanachama wa kawaida au apeperushe bendera?
Hapa hatujapewa jibu.
@Ng'wamapalala kuna hoja hapo, unaweza kutusaidia?
Pili, Alinda aliuliza haya
Je, Dr alimkaribisha Lowassa kama nani? Mgombea,mwanachama, au mtu atakayesaidia kampeni?
Mwalimu akaulizahivi ' Gwajima alipompigia simu Dr Slaa na kumwambia, Dodoma wamemkatatufanyeje ? Ina maana gan?
Kuna alihojia kuwa nani hasa alimwalika Lowassa kati ya pande mbili?
Suala la shule za kata lilizungumzwa wakati wa kura za maoni za CCM kama lile la maji.
Chakujiuliza ilikuwaje mambo hayo yakaingia katika mgogoro wao ambao ni yeye na Mbowe/Lissu?
Halafu Dr amesema anaacha siasa. Katika hotuba anasema atazungumka kumpinga Lowassa.
Hapa inakuwaje, kwamba anakuwa na NGO au anampinga kama mtu binafasi au inakuwaje?
Haya ni mambo tunayotakiwa tuyajadili kwa upana wake
Kwa jinsi tunavyomuelewa Dr. Slaa kwa swala la Lowassa hisingekuwa rais Gwajima ampigie simu tu from nowhere kumueleza kukatwa kwa Lowassa na Dr. Slaa ajibu mpaka niongee na Mwenyekiti..
Ndio maana kauli ya Lissu kwangu inaleta mantiki kuwa Dr. Slaa, Gwajima na Lowassa walikuwa na maongezi kabla ya Lowassa kukatwa inaweza kuwa ni May au June au hata July mwanzo...Sasa kama anafahamu uchafu wa Lowassa na huu uchafu wa Lowassa ndio ulimfanya yeye kuachana na siasa ni kwanini yeye kupeleka wazo la Lowassa kuhamia Chadema?