Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 887
- 2,201
Moja ya sifa nzuri na thabiti ya kiongozi ni kusimamia anachokiamini hata kama msimamo huo unaweza kumdhuru binafsi au na taasisi anayoongoza.
Msimamo wa CHADEMA ulioamuliwa na Kamati Kuu yake na kutangazia dunia hadharani kupitia kinywa cha Katibu Mkuu wake John Mnyika na Mwenyekiti Freeman Mbowe ni kwamba chama hicho HAKITASHIRIKI Uchaguzi WOWOTE bila kuwepo kwa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.
Huko Mbeya Jimbo la Mbarali Jimbo liko wazi na linatakiwa kuzibwa ndani ya siku 90 kwa mujibu wa Katiba ya Sasa (isiyotakiwa na CHADEMA) kufuatia kifo cha Francis Mtega aliyefariki baada ya kugonga "pawatila" akiwa na pikipiki.
Kwa msimamo huo hatutegemei kuona CHADEMA ikisimamisha mgombea ili kuonesha msimamo.
Si hapo tu. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni mwakani Jumapili ya mwisho wa mwezi Oktoba 2024. Hakika niliyonayo kwa muda uliosalia tutakuwa bado hatujapata Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi. Nitasikitika Chadema ikishiriki Uchaguzi huo.
Kwa mambo yanavyoenda ndani ya CCM na Serikali Samia hawezi kutoa Katiba Mpya ndani ya first term yake. Maana yake yake ni kwamba 2025 Katiba itakayofanya kazi ni hii hii. Kwa mantiki hiyo, sitegemei kuona CHADEMA kushiriki Uchaguzi huo Mkuu maana hakutakuwa na Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi. Kwa msimamo huo CHADEMA itashiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2029 na Uchaguzi Mkuu wa 2030. Simamieni uamuzi wenu ili msionekane wajinga wa maamuzi. Siku njema.