jMali
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 8,379
- 4,899
Utangulizi:
Lengo hapa si kujadili uhalali wa waraka, bali baadhi ya mambo yaliyoibuliwa na waraka ambayo kwetu sisi tunayoipenda chadema, lakini si wanachama, yametupa maswali, maswali ambayo kama yatapuuzwa yataleta changamoto kubwa kwa watanzania kuikubali chadema kama mbadala wa CCM mwaka 2015. waraka ninaozungumzia ni huu
Napenda kuonya kuwa nauliza maswali haya kwa nia njema kabisa kwa kumaanisha vyema. Situhumu, bali nauliza nikitaka kujua ukweli. Najihami hivi kwa sababu kuna tabia ya wanachama (au labda ni mashabiki zaidi) wa Chadema kulipuka kwa kebehi pale wanapoulizwa maswali ya msingi kabisa humu jukwaani kuhusu CDM wakidhani wote wanaohoji ni wapinzani wa CDM. Watanzania wengi, mimi nikiwemo hatuna kadi ya chama chochote, huwa tunapiga kura tu. Wananchi tulio wengi tumeichoka CCM, lakini hii haimaanishi kuwa tuko tayari kuchagua zimwi lingine lolote lile. Hata CCM huwa wana majibu ya kiungwana kuhusu madudu yao!
Naomba kwa heshima na taadhima kwa anayejua majibu ya maswali haya kujibu kipengele chochote kile anachoweza kujibu.
1. Ukomo wa uongozi: Wakati tukiufanyia mwongozo wetu mabadiliko mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Lakini wakati mwongozo unachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela.
Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha juu mno cha hivi karibuni kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa na wilaya na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa tano maamuzi hayo hayajatekelezwa. Lakini kuna michango ya watu binafsi kama yule mtanzania mwenye asili ya kihindi, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. Hapo hatujataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.

Swali: Je ni kweli kuwa kipengele hiki cha ukomo wa kugombea kilichakachuliwa? kama kweli, je ni sababu gani iliyofanya kipengele hiki kuondolewa? Utamaduni wa kuweka ukomo wa vipindi vya uongozi ni ustaarabu uliozoeleka katika taasisi zote za kidemokrasia. Tuhuma hii ni nzito mno kwa chama kinachoojita cha demokrasia kudaiwa kuufuta, tena kinyemela! Ninategemea nipate sababu za msingi za kufutwa kwa kipengele hiki, vile vile utaratibu uliotumika kukifuta. Kwani kama wanachama wa ngazi ya juu kama Samson mwigamba na mkumbo (mwandishi na mhariri waraka) hawajui, sidhani kama utaratibu uliotumika ulikuwa halali. Of course, kwa upande wa pili ninaweza kujibiwa kuwa utaratibu huu bado upo na alieandika hivi kwenye waraka ni mzushi na viongozi wanaomaliza ukomo wao wataondoka accordingly! Lakini all in all naomba majibu.
2. Mambo ya fedha: Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani mkuu kabisa, mtendaji mkuu na mkuu wa fedha kwenye taasisi yetu. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha. Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje.
Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha juu mno cha hivi karibuni kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa na wilaya na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa tano maamuzi hayo hayajatekelezwa. Lakini kuna michango ya watu binafsi kama yule mtanzania mwenye asili ya kihindi, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. Hapo hatujataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.
Maswali:
1. Je ni kweli kuwa watu watatu tu ndio wenye maamuzi juu ya fedha za CDM? Sizungumzii hawa mabwana kuwa signatories, nazungumzia uwezo wa maamuzi yao. Kwamba hawa mabwana wana uwezo wa ku-ovveride maamuzi ya vikao halali kuhusu fedha, na wamefanya hivyo kama waraka unavyodai?
2. Kwamba akaunti maalum kwa ajili ya 2015 haina fedha na kwamba zimetumiwa bila vikao maalum kuidhinisha.
3. Kwamba maamuzi ya kupeleka fedha katika mikoa, wilaya
kwa mujibu wa maazimio ya vikao hayajatekelezwa ingawa fedha zilishatolewa.
4. Fedha za michango ya wananchi kama sabodo na sisi wengine kupitia michango kama ya Mpesa n.k ziko chini ya nani, na mwanachama anapataje taarifa juu ya fedha hizi.
5. Je ni kweli kuwa Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za taasisi.?
3. Intelijensia ya CDM: Hakuna kamati maalum inayowathibitisha maaintelijensia hao bali wakuu wenyewe wanawachukua wanaowataka
Maswali:
1. Katiba ya chama inasemaje kuhusu hawa intelijensia wapo kikatiba kwenye chama? Nani anaajiri hawa watu, kuna kamati yoyote?, na wanadhibitiwa na nani, wanajibu kwa nani, kwa utaratibu upi. Swali hili lizingatie kuwa si mara chache viongozi wa chadema wamekuwa wakitoa matamko ambayo supposedly ni taarifa za kiintelijensia, ambayo mwisho wa siku yana-embarrass chama. Mfano; Madai ya vikao vya siri vya JK na wanae hoteli ya mwanza 2010, ambayo bila hata kukanushwa na Ridhiwani yalionekana kabisa kuwa ni ya mashaka, malori ya kura za bandia ambayo yalikuwa invisible kwetu sote isipokuwa katibu mkuu tu, na mengineo mengi yanayotolewa kwa mbwembwe na tambo nyingi za kuonyesha kuwa CDM imekubuhu kiintelijensia lakini kwa bahati mbaya yanaonekana uzushi badala ya ukweli na hivyo kuathiri taswira ya chama hata kwa sisi tunaoipenda chadema!
4. Mali za chadema: Bila aibu, mkuu wa taasisi ndio amekuwa mnunuzi wa vifaa vyote vya chama nje ya nchi kwa bei anayoijua mwenyewe na ambaye haihojiwi popote
..Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya taasisi na taasisi inanufaika vipi na mauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya taasisi vinauzwa. Jambo hili linajulikana kwa wakuu tu
Swali:
Utaratibu upi unatumika kununua au kuuza mali za chadema? Kamati au mkuu wa taasisi?
Ombi: Kwa kuwa mwandishi wa waraka, pamoja na mhariri wako humu jukwaani itakuwa vizuri kwa wao kutoa mifano hai ya tuhuma hizi endapo zitakanushwa visivyo. Sidhani kama kutoa mifano hai ya tuhuma hizi itaathiri mwen endo wa kesi wanayoikabili ndani ya CDM.Utaratibu upi unatumika kununua au kuuza mali za chadema? Kamati au mkuu wa taasisi?