CHADEMA tujadili waraka

jMali

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
8,379
4,899
Utangulizi:
Lengo hapa si kujadili uhalali wa waraka, bali baadhi ya mambo yaliyoibuliwa na waraka ambayo kwetu sisi tunayoipenda chadema, lakini si wanachama, yametupa maswali, maswali ambayo kama yatapuuzwa yataleta changamoto kubwa kwa watanzania kuikubali chadema kama mbadala wa CCM mwaka 2015. waraka ninaozungumzia ni huu

Napenda kuonya kuwa nauliza maswali haya kwa nia njema kabisa kwa kumaanisha vyema. Situhumu, bali nauliza nikitaka kujua ukweli. Najihami hivi kwa sababu kuna tabia ya wanachama (au labda ni mashabiki zaidi) wa Chadema kulipuka kwa kebehi pale wanapoulizwa maswali ya msingi kabisa humu jukwaani kuhusu CDM wakidhani wote wanaohoji ni wapinzani wa CDM. Watanzania wengi, mimi nikiwemo hatuna kadi ya chama chochote, huwa tunapiga kura tu. Wananchi tulio wengi tumeichoka CCM, lakini hii haimaanishi kuwa tuko tayari kuchagua ‘zimwi lingine lolote lile’. Hata CCM huwa wana majibu ya kiungwana kuhusu madudu yao!

Naomba kwa heshima na taadhima kwa anayejua majibu ya maswali haya kujibu kipengele chochote kile anachoweza kujibu.

1. Ukomo wa uongozi: “Wakati tukiufanyia mwongozo wetu mabadiliko mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Lakini wakati mwongozo unachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela”.

Swali: Je ni kweli kuwa kipengele hiki cha ukomo wa kugombea kilichakachuliwa? kama kweli, je ni sababu gani iliyofanya kipengele hiki kuondolewa? Utamaduni wa kuweka ukomo wa vipindi vya uongozi ni ustaarabu uliozoeleka katika taasisi zote za kidemokrasia. Tuhuma hii ni nzito mno kwa chama kinachoojita cha ‘demokrasia’ kudaiwa kuufuta, tena kinyemela! Ninategemea nipate sababu za msingi za kufutwa kwa kipengele hiki, vile vile utaratibu uliotumika kukifuta. Kwani kama wanachama wa ngazi ya juu kama Samson mwigamba na mkumbo (mwandishi na mhariri waraka) hawajui, sidhani kama utaratibu uliotumika ulikuwa halali. Of course, kwa upande wa pili ninaweza kujibiwa kuwa utaratibu huu bado upo na alieandika hivi kwenye waraka ni mzushi na viongozi wanaomaliza ukomo wao wataondoka accordingly! Lakini all in all naomba majibu.

2. Mambo ya fedha: “Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani mkuu kabisa, mtendaji mkuu na mkuu wa fedha kwenye taasisi yetu. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha. Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje.”
“Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha juu mno cha hivi karibuni kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa na wilaya na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa tano maamuzi hayo hayajatekelezwa. Lakini kuna michango ya watu binafsi kama yule mtanzania mwenye asili ya kihindi, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. Hapo hatujataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.”

Maswali:
1. Je ni kweli kuwa watu watatu tu ndio wenye maamuzi juu ya fedha za CDM? Sizungumzii hawa mabwana kuwa signatories, nazungumzia uwezo wa maamuzi yao. Kwamba hawa mabwana wana uwezo wa ku-ovveride maamuzi ya vikao halali kuhusu fedha, na wamefanya hivyo kama waraka unavyodai?
2. Kwamba akaunti maalum kwa ajili ya 2015 haina fedha na kwamba zimetumiwa bila vikao maalum kuidhinisha.​
3. Kwamba maamuzi ya kupeleka fedha katika mikoa, wilaya…kwa mujibu wa maazimio ya vikao hayajatekelezwa ingawa fedha zilishatolewa.​
4. Fedha za michango ya wananchi kama sabodo na sisi wengine kupitia michango kama ya Mpesa n.k ziko chini ya nani, na mwanachama anapataje taarifa juu ya fedha hizi.
5. Je ni kweli kuwa “Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za taasisi.”?

3. ‘Intelijensia’ ya CDM: “Hakuna kamati maalum inayowathibitisha maaintelijensia hao bali wakuu wenyewe wanawachukua wanaowataka”

Maswali:
1. Katiba ya chama inasemaje kuhusu hawa ‘intelijensia’ wapo kikatiba kwenye chama? Nani anaajiri hawa watu, kuna kamati yoyote?, na wanadhibitiwa na nani, wanajibu kwa nani, kwa utaratibu upi. Swali hili lizingatie kuwa si mara chache viongozi wa chadema wamekuwa wakitoa matamko ambayo supposedly ni taarifa za kiintelijensia, ambayo mwisho wa siku yana-embarrass chama. Mfano; Madai ya vikao vya siri vya JK na wanae hoteli ya mwanza 2010, ambayo bila hata kukanushwa na Ridhiwani yalionekana kabisa kuwa ni ya mashaka, malori ya kura za bandia ambayo yalikuwa invisible kwetu sote isipokuwa katibu mkuu tu, na mengineo mengi yanayotolewa kwa mbwembwe na tambo nyingi za kuonyesha kuwa CDM imekubuhu kiintelijensia lakini kwa bahati mbaya yanaonekana uzushi badala ya ukweli na hivyo kuathiri taswira ya chama hata kwa sisi tunaoipenda chadema!

4. Mali za chadema: “Bila aibu, mkuu wa taasisi ndio amekuwa mnunuzi wa vifaa vyote vya chama nje ya nchi kwa bei anayoijua mwenyewe na ambaye haihojiwi popote…” “..Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya taasisi na taasisi inanufaika vipi na mauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya taasisi vinauzwa. Jambo hili linajulikana kwa wakuu tu”

Swali:
Utaratibu upi unatumika kununua au kuuza mali za chadema? Kamati au “mkuu wa taasisi”?

Ombi: Kwa kuwa mwandishi wa waraka, pamoja na mhariri wako humu jukwaani itakuwa vizuri kwa wao kutoa mifano hai ya tuhuma hizi endapo zitakanushwa visivyo. Sidhani kama kutoa mifano hai ya tuhuma hizi itaathiri mwen endo wa ‘kesi’ wanayoikabili ndani ya CDM.
 
Haya maswali niya msingi sna,ila ulipaswa umuulize mzee mtei,mbowe,na liliani mtei,ila ujiandae kupigwa kitofali cha kichwa na lema
 
Maswali muhimu kabisa.

Baada ya kumshutumu Zitto na team yake kwa kuuchimba muungano wa chama kichinichini kwa aina ya kihaini, naona ni muhimu pia tuangalie yaliyoibuliwa na waraka huu.

We cannot afford to be in an either or mode, all or nothing at all is a myth borne out of simplistic utopia.
 
Mjadala juu ya Zitto na kundi lake umeshafungwa, mnachokiita waraka/ripoti ni FEKI,

Mashitaka halisi ni 11 tu, na leo wamebakiwa na siku 8 tu za kujibu,

Mwambieni Zitto awaambie mashitaka aliyokabidhiwa kwa barua, lakini sharti awaambie baada ya kujibu tuhuma hizo kwa cc ya chadema na si vinginevyo.

Maji ya kimwagika hayazoleki hata uwe kama Hung Lee bingwa wa kukausha maji ulimi bila kuyameza wala kuyamwaga tena,
 
image.jpg Zitto kachutama , nyie wapambe mnamharibia , aibu yenu ....mwa chenu afanye tafakuri ya kina ...
 
Ni jambo lisiloingia akilini kuwa eti watu watatu tu ndio wenye maamuzi kwenye swala la fedha.Bajeti ya chama ya mwaka mzima pamoja na mipango ya miaka ya baadae huwasilishwa, kujadiliwa na kupitishwa na Baraza kuu

Sekretarieti kama chombo cha utendaji cha kila siku hupitisha na kuidhinisha matumizi ya kila siku kama inavyokasimishwa mamlaka na kamati kuu ambayo nayo hukasimishiwa mamlaka na baraza kuu hasa katika utekelezaji wa muda fulani

INTELIGESIA.-Kwa kawaida kuna Idara ya Ulinzi na usalama iliyogawanyika katika idara mbili.Ile ya Ulinzi na ile ya Usalama(Intelijensia)

Katiba ya Chadema inatambua uwepo wa idara ya ulinzi hasa vikundi vya Red Brigade.

Pia habari za intelijensia ya chama kwa akili ya kawaida kabisa haziwezi kupitia mikono ya watu wengi na hata vikao halali vya kamati kuu vinajua na vilishakubaliana na hili.

Hilo la kutokaguliwa matumizi ya chama tangu 2010 lilishajibiwa na mkurugenzi wa fedha na utawala kwa press conference

Pia ni bora watu hao wakawa specific .Ni mali gani exactly zilizonunuliwa nje bila vikao vya chama kujua au kuridhia?

Hao waliotoa claim hizo ni viongozi na wajumbe wa kamati kuu sasa tangu 2010 mbona hawaku-raise hilo?Huu si unafiki na ufisadi tunaoupinga ?
 
Slaa tangu jana katangaza Mjadala umefungwa sasa wewe si unafanya Usaliti au umenunuliwa kuvuruga Chama?

Nioneshe kwenye Waraka Aya au Sentensi au Neno linazohusu Uhaini kwa Mujibu wa CC ya Chama chako.
 
Nilitamani sana kuujadili waraka kwa upande wa pili kama ulivyoanzisha. Kwa bahati mbaya sana mimi si miongoni mwa wale "mabwana" hivyo sina majibu nasubiri wenye majibu wayamwage. Wanaosema mjadala umefungwa watuambie ni nani aliyefunga na kwa sababu zipi. Na je ameufunga kwa kufuata misingi ya kidemokrasia au ya KIDIKTETA ya kutaka kuwalazimisha watu.
 
Maswali ya kiusaliti saliti hayo! mwambieni mamluki mwenzenu ajibu barua full stop,hao mamluki wote walikuwa cc ya cdm,walishindwa nn kuuliza huko? wangekosa majibu au kupuuzwa,wangetafuta chama cha kuwafaa.Hebu tujiulize,hao MM,M1 M2, M3 walishindwa nini kuuliza ktk vikao,hadi waje na mpango wa mapinduzi? cdm ni chama kikubwa napendekeza wafukuzwe wote watatu,uhalamia wao waupeleke wanapotaka!
 
Mjadala juu ya Zitto na kundi lake umeshafungwa, mnachokiita waraka/ripoti ni FEKI,

Mashitaka halisi ni 11 tu, na leo wamebakiwa na siku 8 tu za kujibu,

Mwambieni Zitto awaambie mashitaka aliyokabidhiwa kwa barua, lakini sharti awaambie baada ya kujibu tuhuma hizo kwa cc ya chadema na si vinginevyo.

Maji ya kimwagika hayazoleki hata uwe kama Hung Lee bingwa wa kukausha maji ulimi bila kuyameza wala kuyamwaga tena,

Watumwa na watawaliwa ndio mnaoweza kufungwa midomo na Dr. Slaa.

Walio huru wanajadili. Ndio maana mjumbe wa Baraza Kuu ametoa tamko la kupinga uhuni unaofanywa na Mbowe na Mtei.
 
Mjadala juu ya Zitto na kundi lake umeshafungwa, mnachokiita waraka/ripoti ni FEKI,

Mashitaka halisi ni 11 tu, na leo wamebakiwa na siku 8 tu za kujibu,

Mwambieni Zitto awaambie mashitaka aliyokabidhiwa kwa barua, lakini sharti awaambie baada ya kujibu tuhuma hizo kwa cc ya chadema na si vinginevyo.

Maji ya kimwagika hayazoleki hata uwe kama Hung Lee bingwa wa kukausha maji ulimi bila kuyameza wala kuyamwaga tena,

Una kifua cha kuvumilia kutokuingia kwenye Mjadala unaomhusu Zitto? Mimi ni Mtu wa kwanza ku Bet na wewe kuwa huna ubavu wa kutokuingia kwenye Mjadala unaomhusu Zitto. Please Prove me Wrong
 
Nilitamani sana kuujadili waraka kwa upande wa pili kama ulivyoanzisha. Kwa bahati mbaya sana mimi si miongoni mwa wale "mabwana" hivyo sina majibu nasubiri wenye majibu wayamwage. Wanaosema mjadala umefungwa watuambie ni nani aliyefunga na kwa sababu zipi. Na je ameufunga kwa kufuata misingi ya kidemokrasia au ya KIDIKTETA ya kutaka kuwalazimisha watu.

Huyo aliyefunga mjadala alitaka kuwa Rais wa nchi.

You can imagine nchi ingeendeshwa vipi iwapo ingetokea bahati mbaya akapitishwa.

Mungu aliwaongoza vyema watanzania wasichague muovu kuwa Rais.
 
Ni jambo lisiloingia akilini kuwa eti watu watatu tu ndio wenye maamuzi kwenye swala la fedha.Bajeti ya chama ya mwaka mzima pamoja na mipango ya miaka ya baadae huwasilishwa, kujadiliwa na kupitishwa na Baraza kuu

Sekretarieti kama chombo cha utendaji cha kila siku hupitisha na kuidhinisha matumizi ya kila siku kama inavyokasimishwa mamlaka na kamati kuu ambayo nayo hukasimishiwa mamlaka na baraza kuu hasa katika utekelezaji wa muda fulani

INTELIGESIA.-Kwa kawaida kuna Idara ya Ulinzi na usalama iliyogawanyika katika idara mbili.Ile ya Ulinzi na ile ya Usalama(Intelijensia)

Katiba ya Chadema inatambua uwepo wa idara ya ulinzi hasa vikundi vya Red Brigade.

Pia habari za intelijensia ya chama kwa akili ya kawaida kabisa haziwezi kupitia mikono ya watu wengi na hata vikao halali vya kamati kuu vinajua na vilishakubaliana na hili.

Hilo la kutokaguliwa matumizi ya chama tangu 2010 lilishajibiwa na mkurugenzi wa fedha na utawala kwa press conference

Pia ni bora watu hao wakawa specific .Ni mali gani exactly zilizonunuliwa nje bila vikao vya chama kujua au kuridhia?

Hao waliotoa claim hizo ni viongozi na wajumbe wa kamati kuu sasa tangu 2010 mbona hawaku-raise hilo?Huu si unafiki na ufisadi tunaoupinga ?

"Mida Eight anatumiwa na Dr. Slaa kugombanisha viongozi" - waraka
 
Maswali ya kiusaliti saliti hayo! mwambieni mamluki mwenzenu ajibu barua full stop,hao mamluki wote walikuwa cc ya cdm,walishindwa nn kuuliza huko? wangekosa majibu au kupuuzwa,wangetafuta chama cha kuwafaa.Hebu tujiulize,hao MM,M1 M2, M3 walishindwa nini kuuliza ktk vikao,hadi waje na mpango wa mapinduzi? cdm ni chama kikubwa napendekeza wafukuzwe wote watatu,uhalamia wao waupeleke wanapotaka!

Acha Hoja za Kitoto!! Mbona hujawahi kumuuliza Slaa anaekwambia Tangu Uhuru 1961 CCM haijafanya kitu lakin yeye Mpaka 1995 alikuwa Kada Mwaminifu wa CCM, aliponyimwa kugombea Ubunge Karatu ndo akahama CCM, Mkewe Rose Kamili alikuwa CCM Mpaka 2010 aliposhindwa na Ndugu Mary Nagu ndo akahamia Chadema. Unajua kuwa Slaa na Mkewe Rose Kamili wote wamehama CCM sio kwa jambo lingine zaid ya kutopitishwa kugombea Ubunge na Laiti angepitishwa basi hayo 'mabaya' yote ya CCM asingeyaona.
 
Mjadala juu ya Zitto na kundi lake umeshafungwa, mnachokiita waraka/ripoti ni FEKI,

Mashitaka halisi ni 11 tu, na leo wamebakiwa na siku 8 tu za kujibu,

Mwambieni Zitto awaambie mashitaka aliyokabidhiwa kwa barua, lakini sharti awaambie baada ya kujibu tuhuma hizo kwa cc ya chadema na si vinginevyo.

Maji ya kimwagika hayazoleki hata uwe kama Hung Lee bingwa wa kukausha maji ulimi bila kuyameza wala kuyamwaga tena,
Mi nadhani ungejibu hoja usilete mambo general hapa, umetuchosha sijui ukoje tu, tuambie kama manunuzi yakoje, Mbowe kwa nini anang'ang'ani madaraka?mngejua kama yeye ndo kibaraka mngeshamchukulia hatua, na siku mkimgundua sijui mtaficha wapi sura zenu
 
Hii ni sauti ya Tumaini Makene.naleo umepewa ruhusa ya kujibu? Hivi tumani yuko likizo au amefutwa kazi?

Naomba kujua kama mkopo wa dr slaa kama ulirudishwa na riba.

Ni lini ofisi za chama hasa makao makuu zitajengwa?

Hivi chadema kama ina ruhusu mwanachama wake kumrushia matofali mwanachama mwingine itakwepaje kashifa za kumwagia watu tindikali?
ni jambo lisiloingia akilini kuwa eti watu watatu tu ndio wenye maamuzi kwenye swala la fedha.bajeti ya chama ya mwaka mzima pamoja na mipango ya miaka ya baadae huwasilishwa, kujadiliwa na kupitishwa na baraza kuu

sekretarieti kama chombo cha utendaji cha kila siku hupitisha na kuidhinisha matumizi ya kila siku kama inavyokasimishwa mamlaka na kamati kuu ambayo nayo hukasimishiwa mamlaka na baraza kuu hasa katika utekelezaji wa muda fulani

inteligesia.-kwa kawaida kuna idara ya ulinzi na usalama iliyogawanyika katika idara mbili.ile ya ulinzi na ile ya usalama(intelijensia)

katiba ya chadema inatambua uwepo wa idara ya ulinzi hasa vikundi vya red brigade.

Pia habari za intelijensia ya chama kwa akili ya kawaida kabisa haziwezi kupitia mikono ya watu wengi na hata vikao halali vya kamati kuu vinajua na vilishakubaliana na hili.

Hilo la kutokaguliwa matumizi ya chama tangu 2010 lilishajibiwa na mkurugenzi wa fedha na utawala kwa press conference

pia ni bora watu hao wakawa specific .ni mali gani exactly zilizonunuliwa nje bila vikao vya chama kujua au kuridhia?

Hao waliotoa claim hizo ni viongozi na wajumbe wa kamati kuu sasa tangu 2010 mbona hawaku-raise hilo?huu si unafiki na ufisadi tunaoupinga ?

hivi kwanini chadema mnataka kutonywa hili kukaguliwa?

Hile report report ya siri ambayo ilikuwa ina mhusu zitto ilikanwa na chadema lakini jana kamanda wa lema bw Mungi alisema hile report ni ya kweli na chadema wameikana kwa mkakati mahususi ni kweli.

Cc CHAMVIGA Ritz THE BIG SHOW sixgates.
 
Last edited by a moderator:

Usawa wa dijitali mjadala haufungiki, labda watafunga kwenye vikao vya vyama.
 
Mjadala juu ya Zitto na kundi lake umeshafungwa, mnachokiita waraka/ripoti ni FEKI,

Mashitaka halisi ni 11 tu, na leo wamebakiwa na siku 8 tu za kujibu,

Mwambieni Zitto awaambie mashitaka aliyokabidhiwa kwa barua, lakini sharti awaambie baada ya kujibu tuhuma hizo kwa cc ya chadema na si vinginevyo.

Maji ya kimwagika hayazoleki hata uwe kama Hung Lee bingwa wa kukausha maji ulimi bila kuyameza wala kuyamwaga tena,

Who has the authority to stop us not continuing discussing this? This is free forum and not CDM forum...may be you should tell ur fellows who are the ones catalyze the saga....those who has neutral mind like me we should continue expose pros an cons of the waraka.
 
Back
Top Bottom