CHADEMA Special Thread

Uzi wa matukio mbalimbali ya CHADEMA . Madhila wanayopitia.. Vita wanazopigana.. Mafanikio wanayopa .. Na namna wanavyomgaragaza adui kwenye kila kona.. Kila saa na kila wakati
Karibuni wote! Friends and foes!
tukio moja muhimu zaidi ni lile la kiongozi mkuu wa chadema kwenda na msosi kizimabani, huenda ansumbuliwa na minyooo wakali zaidi hasa anapobananishwa na watoa ushahidi
 
#Updates Jeshi la Polisi Bunda mapema leo limewakamata jumla ya Bawacha 39 kutoka mikoa ya Dodoma na Iringa. Kati yao, 31 wanatoka Dodoma na 8 wanatoka Iringa.

Awali Bawacha waliotoka Dodoma walikuwa wanasafiri kwa kutumia basi dogo aina ya Coaster, huku wale waliotoka Iringa wakiwa kwenye basi la abiria. Baada ya kufika katika eneo la Bunda, Jeshi la Polisi liliwashusha Bawacha waliokuwa kwenye basi la abiria kutoka Iringa na kuwahamishia katika gari lao la Polisi.

Bawacha hao walipelekwa katika Kituo cha Polisi Bunda ambapo walichukuliwa maelezo yao kuhusu wanakotoka na wanakoelekea. Baada ya hatua hiyo, Mkuu wa Kituo cha Polisi Bunda (OCD) alieleza kuwa kuna zuio la wamama kutoka mikoa mingine kuingia Mkoa wa Mara.

Kutokana na zuio hilo, Jeshi la Polisi limeanza kuwasafirisha kurejea walikotoka. Bawacha waliotoka Dodoma wanarudishwa kwa kutumia basi lao aina ya Coaster huku ndani ya basi hilo wakiwa wamepakiwa askari wa Jeshi la Polisi.

Kwa upande wa Bawacha waliotoka Iringa, wao wamepakiwa katika gari la Polisi aina ya Defender kwa ajili ya kurejeshwa Iringa, licha ya hali ya baridi iliyopo ambayo inaweza kuathiri afya na ustawi wao wakati wa safari.

 
Hii ndio thread sasa
Na hope taarifa rasmi zote nitazipata hapa
Subscribed ✅
 
#UPDATES

Nimejulishwa hapa kwamba Polisi wa Simiyu wamemwambia dereva wa Coaster ageuze gari awarudishe Bawacha wa Dodoma kwao, Dereva kawambia gari haina mafuta ya kutosha kufika Dodoma labda waongee na waliokodi watoe pesa ya mafuta.

Basi Polisi wakawambia Bawacha wa Dodoma watoe pesa ya mafuta ili safari ianze, Bawacha wakawajibu kwamba mlipaji wa pesa ya mafuta yupo Musoma mjini hawezi kulipa mpaka aione gari Musoma mjini.

Polisi wahangaika kupiga simu asa sijui ndo wanaomba maboss zao pesa ya mafuta.
 
Anaandika Godbless Lema

BAWACHA nyinyi ni watu wa maana sana katika nchi yetu. Jipeni moyo mkuu mkijua kwamba hata katika giza refu zaidi, alfajiri huwa haikosekani. Historia ya jamii yoyote ina vipindi vya majaribu, mateso, kadhia na hata udhalilishwaji, lakini yote hayo huwa ya muda tu mbele ya nguvu ya dhamira na imani ya watu wake. Kutakuwa na siku mtatazama nyuma na kujiuliza, “Tulifikaje hapa?” Na katika mshangao huo mtatambua kuwa hatua zenu za leo, uvumilivu, ujasiri na mshikamano, ndizo zilizojenga kesho bora. Hapo ndipo mtakapokuwa na simulizi la heshima la kuwaeleza watoto na wajukuu zenu. Simulizi litakalowafundisha kwamba kukata tamaa si tabia ya wanaotafuta haki na mabadiliko.

Tambueni kuwa thamani ya juhudi zenu si ndogo. Mmekuwa baraka kubwa kwa chama chetu na kwa jamii inayotazama mbele kwa matumaini. Ni mtu mpumbavu tu asiyeweza kuona mchango wenu na mwanga mnaouleta katika safari hii.
Basi endeleeni kusimama imara. Busara iwape mwanga wa maamuzi na ujasiri uwe nguvu ya hatua zenu. Kwa sababu katika falsafa ya maisha ushindi wa kweli haupatikani kwa kukosa majaribu bali kwa kuyavuka kwa heshima, uvumilivu na imani thabiti.
 
Tunamshukuru Mungu,

Licha ya changamoto zote za barabarani walizokutana nazo Bawacha kutoka Mkoa wa Tabora ni miongoni mwa Mikoa ambayo imewasili salama Musoma mjini kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. John Heche amejumuika na viongozi pamoja na wanachama wa Bunda kusikiliza kesi inayomkabili Katibu Mkuu Wa Bavicha Mstaafu Kamanda Yohana Kaunya na wenzake 20.
No Retreat No Surrender
 
#UPDATES_KUHUSU_BAWACHA_DODOMA

BAWACHA wa Mkoa wa Dodoma wamegoma kuendelea na usiku huu kwasababu za kiusalama lakin pia wamechoka sana tangu jana usiku mpaka muda wako barabarani.

Polisi ambao wanaescort gari ya BAWACHA kila baada ya muda fulani wanabadilisha magari kibaya zaidi wanabadilishia magari maporini kinyume kabisa na Utaratibu.

Wakati makubaliano ya BAWACHA hao na Mkuu wa kituo cha Bunda ilikuwa watakuwa wanabadilishia magari kwenye kituo cha Polisi sasa sijui imekuaje hawa wanafanya kinyume.

So kutokana na hayo BAWACHA walimuomba Dereva wa gari yao apaki gari Petrol Station ambayo ipo Wilaya ya Nzega kwasababu wanahofia usalama wao.

Kunaubishani unaendelea kati ya Polisi na BAWACHA, Polisi walitaka safari iendelee usiku lakin BAWACHA wamegoma wanataka pakuche kwanza ndo waendelee na safari.

Ikumbukwe BAWACHA kutoka Mkoa wa Dodoma na Iringa walikamatwa leo jioni Wilayani Bunda wakati wanaelekea Musoma mjini kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake, baada ya kukamatwa Polisi waliamua kuwarudisha kwao kwa escort ya Polisi.
 
Kalamu ya Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza PhD
MAADUI WAKIISHA, MARAFIKI WATAGEUKA MAADUI.

Ajabu ya Wajaluo: Ukizoea kumsingizia adui kwa kila tatizo lako, siku ukimmaliza huyo adui, utawageuza marafiki zako wawe maadui ili upate wa kusingizia kila tatizo lako.

Nimesikia viongozi wetu wakidai wanaliunganisha taifa. Wengine wamesema taifa ni tulivu. Na wengine wameajiri mawakala wa kutafuta maridhiano. Sasa najiuliza:

1. Mawaziri wako London, New York, Addis Ababa na Brussels kueleza jinsi nchi ilivyotulia, LAKINI huku nyuma polisi wanakataa kwamba ndani ya Chadema hakuna wanawake na chama chote ni wanaume! Tulisitisha maadhimisho ya Uhuru; tunazuia hata siku ya wanawake wa dunia? Je, Tuna mashaka kama hao ni wanawake sawasawa?!

2. Mikutano ya hadhara inaonyesha kuna kero nyingi kuliko watatuaji, LAKINI kuna watu mitandaoni wanapongeza jinsi nchi ilivyo tulivu na maendeleo yanapaa! Tunaficha uchi, tutazaaje?

3. Janga la utekaji linaendelea na mamia wako mafichoni, LAKINI viongozi wetu hata kwenye mikutano ya hadhara hilo halizungumzwi! Kama serikali haihusiki na utekaji basi inahujumiwa na watekaji. Kauli ya serikali ilitakiwa toka juzi ileee.

4. Tunakodisha watu kwenda kuteka na kudhuru nje ya nchi BADALA ya kukodisha wapatanishi na mabalozi wa kurejesha nyumbani wakosoaji. Tunasubiri tukalishwe meza moja na Rachel Dangwa mbele ya Katibu Mkuu wa UN?

5. Polisi wanavuruga uwezekano wa maridhiano na kuizika serikali ikiwa hai. Tukumbuke: Polisi walioipigia saluti UNION JACK ndiyo walioipigia bendera ya Tanganyika huru. Serikali inawadanganya polisi na polisi inawadanganya serikali. Mchezo wa kitoto huu.

6. CCM haiko kimya. Ina historia ya kuibuka na kukataa dhuluma. Kuteka, kutesa na kuua si sera yake. Kuiba kura yaweza kuwa sera ya muda lakini si wote wanaipenda. Ukimya wa CCM ni kuchimba kaburi kwa meno yake. Itaamka, na kwa sasa adui wake si CHADEMA ambayo ni “marehemu”. Adui wa CCM anajijua na CCM inamjua. Mkumbukeni John Komba na “Jogoo limewika Dodoma”. Amkeni muokoe nchi na chama.

7. Tumekodisha mawakala wa maridhiano wakati tunavuruga maridhiano. Sasa watatuambia nini wakati hila tunaziona wenyewe? Mnawavunjia heshima hata kama wamejivunjia kwa kudokoa wali kabla haujawiva.

8. Mgonjwa wa kusahau hawezi kukumbuka tatizo lilianza lini. Serikali isiyokosolewa ni ile isiyokuwapo. Serikali isiyokosea na ile isiyofanya chochote. Serikali ipo; haina chanzo ya kutokosea. Ikiri makosa na kuwajibika ili tusonge mbele. Inapoteza muda na fedha kupiga propoganda. Ndevu waweza kuzificha kwa kunyoa; matiti je?

Vituko vyetu vimezidi mpaka Mjaluo amecheka na kutuonyesha mapengo anayoyaita mwanya.

Kwaresima Njema
Ramadhani Kareem
 
Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma limefutua ruhusa iliyotolewa awali kwa Baraza la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) ya kutumia Uwanja wa Matumaini Vijana kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Maadhimisho hayo yaliokuwa yamepangwa kufanyika Jumapili, Machi 8, 2026, sasa hayataweza kuendelea kutokana na uamuzi huu wa Kanisa.

Padre Michael Nyamhanga, Mkurugenzi wa Kituo cha Vijana cha Kanisa Katoliki Musoma, ameeleza katika barua rasmi iliyotumwa kwa BAWACHA kuwa uamuzi wa kufuta ruhusa hii umetokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Kanisa. Padre Nyamhanga alisisitiza kuwa Kanisa haliwezi kuingilia kati hali zilizopo, na hatua hii ni matokeo ya kufuata taratibu na kuhakikisha heshima kwa pande zote zinazohusika.

“Kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu, tunasikitika kufuta ruhusa ya uwanja. Tunawashukuru wote kwa kushirikiana na kuelewa hali hii, na tunawatakia kila la kheri katika shughuli zao za kijamii na maendeleo ya jamii,” amesema Padre Nyamhanga.

Uamuzi huu wa Kanisa unafuata sintofahamu iliyopo kati ya waandaaji wa tukio hilo na hali nyinginezo za kiutendaji, huku Kanisa likisisitiza kuwa hatua hii ni muhimu ili kuhakikisha amani na utulivu unadumishwa katika jamii.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yamekuwa tukio muhimu kwa kuhimiza usawa wa kijinsia na mshikamano wa kijamii, lakini katika hali hii, BAWACHA inashauriwa kuzingatia uamuzi wa Kanisa na kupanga njia mbadala za kuendeleza shughuli zao bila kuvunja taratibu zilizopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…