CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,869
Reaction score
828,403
Uzi wa matukio mbalimbali ya CHADEMA . Madhila wanayopitia.. Vita wanazopigana.. Mafanikio wanayopa .. Na namna wanavyomgaragaza adui kwenye kila kona.. Kila saa na kila wakati
Karibuni wote! Friends and foes!
 
WANACHAMA 7 WA CHADEMA WILAYANI MAGU WAMEACHIWA RASMI NA MAHAKAMA

Baada ya Jamhuri kushindwa kwenye kesi ya kuchoma moto hapa Magu, wameamua kuachana na kesi ya Uhaini kwa kusema Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Hana Nia ya kuendelea na kesi hiyo ya uhaini.

Sasa vijana wetu wote wa Magu wanaenda nyumbani kuungana na familia zao.

Asanteni kwa Maombi yenu, Asanteni kwa msaada wenu, !!!

Taarifa kutoka kwa Wakili Gaston Shundo Garubindi ambaye ni Mkurugenzi wa Sheria wa Chadema.
1772840390945.jpg
 
Mapema leo hii Mhe. Lissu akiwasili Mahakamani Kuu ya Dar es salaam ambapo ameomba kuunganishwa kwenye kesi ya Mgawanyo wa mali za CHADEMA ambayo imefunguliwa na vibaraka wa Idd Amin Mama wakiongozwa na Said Issa.

View: https://www.facebook.com/share/v/1AzdLQctRG/

Mapema leo hii Mhe. Lissu akiwasili Mahakamani Kuu ya Dar es salaam ambapo ameomba kuunganishwa kwenye kesi ya Mgawanyo wa mali za CHADEMA ambayo imefunguliwa na vibaraka wa Idd Amin Mama wakiongozwa na Said Issa.
 
Uzi wa matukio mbalimbali ya CHADEMA 26-30.. Madhila wanayopitia.. Vita wanazopigana.. Mafanikio wanayopa .. Na namna wanavyomgaragaza adui kwenye kila kona.. Kila saa na kila wakati
Karibuni wote! Friends and foes!
Huu ni kama uchuro, mkuu 'Mshana Jr' iwapo tayari tunaanza kukubali ya huko 2030.

Ina maana Mzee Butiku na mashetani wenzie tayari wameibuka kidedea?

Hiyo 2030 unayoizungumzia wewe, naina Tanzania ikishatengemaa muda kitambo sana, kiasi kwamba ya 2026 yatakuwa ni historia mbaya iliyopita muda mrefu sana.

Kama CHADEMA na wao wanasubiri 2030, boti wataikuta shang'oa nanga muda kitambo sana.

Hii ni mada mbaya sana, hata sijui imeingiaje ndani ya akili zako.

Nimemaliza kuchangia, sirudi tena kwenye mada mbovu kama hii.
 
WANACHAMA 7 WA CHADEMA WILAYANI MAGU WAMEACHIWA RASMI NA MAHAKAMA

Baada ya Jamhuri kushindwa kwenye kesi ya kuchoma moto hapa Magu, wameamua kuachana na kesi ya Uhaini kwa kusema Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Hana Nia ya kuendelea na kesi hiyo ya uhaini.

Sasa vijana wetu wote wa Magu wanaenda nyumbani kuungana na familia zao.

Asanteni kwa Maombi yenu, Asanteni kwa msaada wenu, !!!

Taarifa kutoka kwa Wakili Gaston Shundo Garubindi ambaye ni Mkurugenzi wa Sheria wa Chadema.View attachment 3553947
Naona/Natumaini ni 'Heading' iliyotumika ndiyo haikukaa sawa.

Ikikupendeza unaweza kuitengeneza upya.
 
Baada ya Lissu kuwekwa ndani, Chadema imepoa sana, ni rahisi kui push, wanachama wamekuwa wepesi kukubali vizuizi wanavyowekewa, nguvu ya kuresist imekuwa ndogo sana
 
Katika hali isiyotarajiwa, viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaweza kujikuta kwenye wakati mgumu baada ya uwepo wa taarifa zinazodai kuwa wamefunguliwa kesi nyingine ya jinai kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam wakidaiwa kukiuka amri ya Mahakama iliyotolewa Juni 10.2025

Inatajwa kuwa amri inayodaiwa kukiukwa inatokana na maamuzi ya Mahakama ya maombi Na. 8960/2025 ambayo msingi wake ni wa kesi ya madai Na. 8323/2025 iliyofunguliwa Mahakamani hapo na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Said Issa Mohamed, Maulidah Anna Komu na Ahmed Rashid Khamis dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA, kesi iliyopo mbele ya Jaji Hamidu Mwanga

Taarifa ilizozipata Jambo TV kutoka kwenye vyanzo vyake vya kuaminika imeonesha kuwa maombi hayo yamefunguliwa na waleta maombi kwenye kesi ya msingi ambao ni Said Issa Mohamed na wenzake wawili (2), ambapo vigogo wa CHADEMA wanaodaiwa kukiuka amri hiyo ni pamoja na John Wegesa Heche (Makamu M/Kiti Tanzania Bara), Amani Golugwa (Naibu K/Mkuu Tanzania Bara), Godbless Lema (Mjumbe wa K/Kuu), John Pambalu (Mkurugenzi wa Organization) na Boniface Jacob (M/Kiti Kanda ya Pwani na Mjumbe K/Kuu),

Wengine ni Pamela Maassay (K/Mkuu BAWACHA), Hamad Mussa Yussuf (Mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi Z'bar), Gervas Lyenda (Mkuu wa Idara ya Habari), John John Mnyika (Katibu Mkuu), Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA,
 
Huu ni kama uchuro, mkuu 'Mshana Jr' iwapo tayari tunaanza kukubali ya huko 2030.

Ina maana Mzee Butiku na mashetani wenzie tayari wameibuka kidedea?

Hiyo 2030 unayoizungumzia wewe, naina Tanzania ikishatengemaa muda kitambo sana, kiasi kwamba ya 2026 yatakuwa ni historia mbaya iliyopita muda mrefu sana.

Kama CHADEMA na wao wanasubiri 2030, boti wataikuta shang'oa nanga muda kitambo sana.

Hii ni mada mbaya sana, hata sijui imeingiaje ndani ya akili zako.

Nimemaliza kuchangia, sirudi tena kwenye mada mbovu kama hii.
Hii ni mada mbaya sana, hata sijui imeingiaje ndani ya akili zako.😭

Nimemaliza kuchangia, sirudi tena kwenye mada mbovu kama hii😭
 
SAID ISSA MOHAMED AWAITAA CHAUMA DAR ES SALAAM KUISHAMBULIA CHADEMA

Tunazo taarifa kwamba Said Issa Mohamed amewaita baadhi ya wanachama wa chama cha CHAUMA kutoka Zanzibar kuja Dar es Salaam kwa lengo la kumuunga mkono katika matamko yake ya kuishambulia chama cha CHADEMA na viongozi wake, ambapo pia wamepangwa kuzungumza na waandishi wa habari mara watakapowasili.

Taarifa zinaeleza kuwa waliokusudiwa kuja Dar es Salaam wamelenga kutoa kauli za kumuunga mkono Said Issa Mohamed katika matamko yake ya kuishambulia CHADEMA na viongozi wake.

Aidha, tunazo taarifa kuwa mpango huo unaratibiwa na Said Issa Mohamed kwa kushirikiana na baadhi ya watu wanaofanya hujuma dhidi ya CHADEMA, wakiwemo wanaosimamia kesi yake.

Vilevile, tunazo taarifa kuwa baadhi ya watu hao wamefika Dar es Salaam leo, huku wengine wanatarajiwa kuwasili kesho, na maandalizi ya mahali pa kufikia, ikiwemo hoteli, yamefanyika kwa ajili yao.

Miongoni mwa watu waliotajwa kuwa katika mpango huo ni pamoja na Habibu Ali Khamis, aliyewahi kuwa Katibu wa Kanda ya Pemba, na Haji Abeid Haji, aliyewahi kuwa Mkuu wa Idara ya Organizesheni, Mafunzo, Sera na Uchaguzi Zanzibar, na wengine.

Tunasisitiza kuwa CHADEMA italindwa kwa nguvu zote dhidi ya njama za hujuma, na taarifa hizi za nia mbaya tunazo, tunazishughulikia kikamilifu. Kila anayejaribu kuharibu heshima au amani ya chama atakumbana na matokeo makali.
 
Back
Top Bottom