Chadema should not apologize!

MMJ,
Nakushukuru kwa post yako. i) Kuhusu kwenda kwa Wananchi, ni vema mkaelewa kuwa mara tu baada ya uchaguzi kulikuwa na "Katazo la mikutano ya hadhara". Katazo ambalo awali hatukuielewa imetolewa na nani na imetolewa kwa mamlaka gani, kwa kuwa katazo la aina hiyo kimsingi ilihitaji "Hali ya Hatari kutangazwa" na tangazo la namna hiyo lilitakiwa litolewe na Rais, lakini haikuwa imetolewa. Ilichukua muda na ni baada ya kukusanya na kupata nyaraka kutoka kwa ma OCD wa maeneo mbalimbali ya nchi nzima. Asiyefahamu hilo atadhani tulikuwa tumekaa kimya na si kila kitu tunaweza kuliweka hadharani mpaka pale tunapokuwa tumepata ushahidi. Wengi wanajua kuwa tulipopata ushahidi kamili tulipiga kelele kwa Tamko la Press Conference iliyotolewa na Wanasheria wetu Mhe. Tundu Lissu na Mhe.Mabere Marando. Baada ya Tamko hilo hali imeanza kubadilika na mikutano ya Wabunge wetu imeanza kuruhusiwa japo ya kisiasa bado inaendelea kuzuiliwa. Ndiyo maana ninasisitiza kuwa ni muhimu kama Taarifa haitoshi, tukaulizana kuliko kulaumiana bila kujua misingi ya kinachofanyika. Nadhani Chadema tuko very open, nimekuja kwenye Jamvi hili kwa jina langu na mara kwa mara nimekuwa nikifafanua mambo mbalimbali yanayoihusu Chadema bila kusubiri na bila kigugumizi. Ninaahidi kuwa kama kuna jambo linahitaji niingilie kwa nafasi yangu nipo tayari bila kusubiri kujenga "hisia" ambayo inaweza kupotosha jambo jema, na kazi ya kurekebisha mara nyingi ni ngumu zaidi, na wakati unarekebisha "damage"kubwa inakuwa imeisha kufanyika. ii) Kuhusu Msimamo wa " Lawful na Illegitimate" Press Conference niliyofanya jana haikuwa Kauli ya Dr. Slaa, wala ya Mgombea Urais wa Chadema. Ilikuwa kauli ya Kamati Kuu ya Chadema. Sasa kama tunaamini katika misingi ya Demokrasia ya "collective Responsibility" basi kama kuna mtu au kiongozi alikuwa hakubaliani na wazo hilo, ni siwezi akalazimishwa. Lakini katika Demokrasia uamuzi wa wengi ukifanyika, basi ndio uamuzi, na ambao hawakuwa wanapenda uamuzi huo hawana budi kukubali uamuzi huo. Kwa bahati mbaya hii ndio demokrasia na sina namna nyingine ya kuielezea. iii) Kutoka kweda kwa Wananchi nayo ina stategy yake na ni swala linalohitaji "political timming". Nadhani Chadema as party with strategies, inatekeleza mikakati yake ya lini itoke kwa wananchi kwa timming ambayo italeta maximum benefit na kuepuka damage ya aina aina yeyote ile. Mengine siwezi kuyamwaga hadharani, lakini naamini kama kuna nia njema ninachokieleza kinaeleweka. Wananchi wengi wanaotupigia simu binafsi huwa tunawaelimisha na tunakubaliana nao kwa mengi. Nadhani nimeeleweka MMJ na wana Jamvi wenzangu.
 

Mgsalon, you are one great tinker, yes, tinker and not thinker.
 

Mgsalon, you are one great tinker, yes, tinker and not thinker.

And you claim to be an intellectual? what a shame if our intellectuals are like you.
 

Dokta Slaa, kwa kuwa unapenda kufafanuwa mambo wewe mwenyewe humu jamvini, hicho ni kitu kizuri sana.

Naomba tufafanulie ile kesi yako iliishaje, nadhani ingawa una majukumu mengi lakini utaikumbuka, kama huikumbuki, labda nikudokezee kidogo. Ile ya yule jamaa anaekushutumu kuwa umechukuwa mkewe. Hebu tujuze imefikia wapi?
 
Mwanakijiji ameingia mitini, kumbe ni mwanasisiem sio mwanakijiji tena. Mwanakijiji eti amekuwa fisadi na yeye duuh wabongo wakilishwa asali wanachonga na mzinga wanasahau walipo toka.
 

How will that help Tanzania..... pse tafuta muda wako peke yako uulize hayo otherwise hapa unawaste our and your time as well
 
Dar-Es-Salaam,
Nashukuru sana. Kesi ya kumpoka mtu mke? Nadhani ni vema wakaulizwa walioianzisha. Mimi sawa na wewe sijui ilikoenda. Ukifanikiwa kujua nijulishe ili nami nijue ilikoenda au ilikoishia baada ya uchaguzi.
 
Dar-Es-Salaam,
Nashukuru sana. Kesi ya kumpoka mtu mke? Nadhani ni vema wakaulizwa walioianzisha. Mimi sawa na wewe sijui ilikoenda. Ukifanikiwa kujua nijulishe ili nami nijue ilikoenda au ilikoishia baada ya uchaguzi.

naona aibu kukuita muongo kwa sababu wewe ni mtu mzima mwenzangu, lakini hii haiwezekani kwa sababu najua taarifa za maendeleo ya kesi hii wanazo wa wanasheria wako ambao ni watu mnaokutana nao mara kwa mara, mambo ya uchaguzi yamekwisha ni bora ungeomba usiulizwe masuala ya kesi hii kuliko kudanganya kwani hata uongo mdogo kwa heshima yako na watu wanaokuamini inakuwa kwenye mashaka.
 
Mm sina hakika na Uadilifu wa Mwanakijiji au wati wote ambao ID zao halisi zimefichwa,nevertheless,si lazima kila mtu ambaye ID Yake haiko wazi basi tuseme ana hila!
That wud utterly wrong,napotofautiana na MM ni kwamba;Kwa sababu tu CDM wameshindwa kusimamia hoja ya mpaka mwisho hiyo haimaanishi kwamba Uchaguzi ulikuwa Huru na Wa Haki!!

Hila ya Mwanakijiji ni kwamba anajaribu kuonyesha(japokuwa sio moja kwa moja) kwamba kwa kuwa CDM wameshindwa kusimamia hoja ya maana yake si sahihi kusema kwamba uchaguzi haukuwa huru na wa haki!!
Hatuhiitaji CDM to tell us the election was not free and fair,it is crystal clear,and the CDM argument wasnt baseless!!
Should one choose to read btn lines,there is a malice in MM's declaration arguing Cdm to apologise to Ccm and Tanzanians!
If there is one politcal party that shud apologies to Tanzanians,Its CCM!! Maovu ya Ccm ni Mengi kiasi mtu haitaji kueleza katika ukurasa huu!!!
 

This post belongs in Mahusiona not Siasa...... Hapa tunaongelea siasa....
 

Dr. Slaa,

Nimesoma sana Katiba yetu hiyo ibara ya 41 kifungu cha 7 kinasema hivi: "Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake." Inaonekana kuwa uongozi wa CHADEMA unaangalia rangi ya bluu tu katika kifungu hicho na kushindwa kuangalia rangi nyekundu. Hakuna mwanasheria anayeweza kuonyesha kuwa kifungu hicho kinataka rais awe amachaguliwa kwa mujibu wa ibara ya 41 yote, ambapo pamoja na mambo mengine ni lazima kifungu chya 6 kiwe kimetimizwa, ambacho kinasema kuwa "Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote. "

(1) Kama kweli kuna ushahidi kuwa matokeo ya Kikwete yalichakachuliwa na hakuwa amepata kura nyingi kuwazidi wagombea wengine na hivyo Tume ilifanya makosa kwa kumtangaza Kikwete kama mshindi bila kutekeleza matakwa yote ya aya 41 ya Katiba, je hamuoni kuwa kifungu cha 7 kitakuwa hakifanyi kazi tena kwa vile rangi nyekundu haikutimia na hivyo matokeoa hayo yanaweza kupingwa?

(2) Iwapo itakuwa ni vigumu kuhoji matokeo hayo, je hamuoni kuwa kuna haja ya kuishitaki tume kwa kosa la kuvunja katiba ya nchi ibara 41(6) kwa kumtangaza mtu ambaye hakupata kura nyingi? katiba haitoi kinga yoyote kwa tume dhidi ya kushitakiwa kwa sababu yoyote ile.

Ningependa jambo hili lichukuliwa kwa umuhimu wa juu sana kabla hatujafikia hatua ya Ivory Coast na Kenya siku za mbeleni.
 
Dar-Es-Salaam,
Nashukuru sana. Kesi ya kumpoka mtu mke? Nadhani ni vema wakaulizwa walioianzisha. Mimi sawa na wewe sijui ilikoenda. Ukifanikiwa kujua nijulishe ili nami nijue ilikoenda au ilikoishia baada ya uchaguzi.

Habari ndiyo hiyo
 
Mbona mimi sijaona uwongo wa Dr. Slaa hapa? Kesi iliisha baada ya uchaguzi. Mtoa mashtaka alidhaminiwa na CCM. Na baada ya uchaguzi CCM wali withdraw udhamini wao. Kesi kwishney. Kama wewe unajua ukweli, kwa sababu kumwita mtu mwongo ni lazima ujue ukweli ni upi, basi uweke hapa tumuumbue Dr. Slaa.
 
Dar-Es-Salaam,
Nashukuru sana. Kesi ya kumpoka mtu mke? Nadhani ni vema wakaulizwa walioianzisha. Mimi sawa na wewe sijui ilikoenda. Ukifanikiwa kujua nijulishe ili nami nijue ilikoenda au ilikoishia baada ya uchaguzi.

Dokta Slaa asnte kwa jibu lako lakini naona unajibu sivyo nilicyoulizan au unachakachuwa? Unasema hujui ilipooenda wakati mimi nimeuliza iliishaje? Sasa Dokta sidhani kama hilo jibu linafanana na swali nililokuuliza. Naomba jibu iliishaje?
 
Dar-Es-Salaam,
Nashukuru sana. Kesi ya kumpoka mtu mke? Nadhani ni vema wakaulizwa walioianzisha. Mimi sawa na wewe sijui ilikoenda. Ukifanikiwa kujua nijulishe ili nami nijue ilikoenda au ilikoishia baada ya uchaguzi.

Dokta Slaa asnte kwa jibu lako lakini naona unajibu sivyo nilicyoulizan au unachakachuwa? Unasema hujui ilipooenda wakati mimi nimeuliza iliishaje? Sasa Dokta sidhani kama hilo jibu linafanana na swali nililokuuliza. Naomba jibu iliishaje? Kwa sababu wewe ni kiongozi wa wengi na kama kweli unakiri kwa kusema ni " vema wakaulizwa walioianzisha" sasa Dokta kama wako walioiamzisha na wewe ndio mshutumiwa si lazima ujuwe imeishia wapi.

Ujuwe tunategemea siku uwe Rais wa nchi hii, bora uwe muwazi na mkweli sasa kuliko kuja kusutwa wakati wa uchaguzi, inalushushia points.
 
Dar-Es-Salaam,
Nashukuru sana. Kesi ya kumpoka mtu mke? Nadhani ni vema wakaulizwa walioianzisha. Mimi sawa na wewe sijui ilikoenda. Ukifanikiwa kujua nijulishe ili nami nijue ilikoenda au ilikoishia baada ya uchaguzi.

Dokta Slaa asante kwa jibu lako lakini naona unajibu sivyo nilivyo-uliza au unachakachuwa? Unasema hujui ilipooenda wakati mimi nimeuliza iliishaje? Sasa Dokta sidhani kama hilo jibu linafanana na swali nililokuuliza. Naomba jibu iliishaje? Kwa sababu wewe ni kiongozi wa wengi na kama kweli unakiri kwa kusema ni " vema wakaulizwa walioianzisha" sasa Dokta kama wako walioiamzisha na wewe ndio mshutumiwa si lazima ujuwe imeishia wapi.

Ujuwe tunategemea siku uwe Rais wa nchi hii, bora uwe muwazi na mkweli sasa kuliko kuja kusutwa wakati wa uchaguzi, ina/itakushushia points.
 

hivi kama wewe tu ambaye hata dr slaa hakujui unajua kama kesi ilikuwa withdrawn baada ya uchaguzi, yeye dr slaa akisema hajui kesi ilipoishia/au hajui jibu la muuliza swali kuwa iliishaje, mtu mwenye akili atasemaje?
 
How will that help Tanzania..... pse tafuta muda wako peke yako uulize hayo otherwise hapa unawaste our and your time as well

How will that help Tanzanians? Tunaongelea President to be, he has to be responsible. Even kwa mke wa mtu, if he can not be responsible, kama kuna ukweli katika shutuma zilizompeleka kushitakiwa, of ones wife how can he be responsible for the wives and daughters of all Tanzanians? Be a thinker not a tinker.
 
Naona kaenda kubadili ID arudi na majibu yaliyo nyooka hapa.
 
Kaka Mwanakijiji nilikupenda sana kwa michango yako sasa umeharisha kama mdogo wako zitto. watu siku hizi wako makini jamani taratibu jamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…