Watumishi wa Magamba mnafanya kazi kubwa sana na ya kuchosha kweli kweli. lakini ima ni niliyo nayo ni kwamba hamlipwi inavyotakiwa. Hebu fikiria namna mnavyofanya bidii kutunga uongo na kuufanya uwe na sura ya ukweli. Fikiria mnavyofunga macho na masikio yenu msione ukweli kweupe na hatimaye mkaabudu uongo mkubwa na kuitaka jamii iamini ujinga wenu.
Ninajua kuwa kama watu wengine mngependa kuheshimiwa kama wajanja wengine lakini mmejitoa sadaka muhesabiwe kuwa uchafu kwa maneno yenu ya siasa za maji taka. Kwa hakika mnastahili pongezi kwa bidii hii na kujitolea sadaka.
Tatizo ni kwamba mnajitolea sadaka kwa mungu mkengemfu. mungu aliyelaaniwa, mungu wa mafisadi.
Poleni sana!!!!!!!!!!