Kabla ya kuchangia chochote ninaomba majibu ya maswali hapo chini(Kama unafikiri mikutano ya CHADEMA haina Political Positive impacts kwa sasa)
1/Kwanini CCM tuko tayari kubeba watu hata na maroli, kuleta wasanii, Kutoa Posho na Ubwabwa ili kujaza mikutano?
2/Kwanini hao 'wazururaji' wajae kwenye mikutano ya CHADEMA zaidi na sio mikutano ya vyama vingine kama CCM nk?
3/Kwanini Serikali na vyombo vya dola wako tayari kuizuia mikutano ya CHADEMA kwa gharama yoyote isifanyike au isifanikiwe?
4/Kwanini Mwenyekiti wa CCM rais Kikwete anaigopa sana mikutano ya CHADEMA mpaka kufikia hatua ya kuamrisha makada wa CCM nao wajibu mapigo kwa kufanya mikutano kama CHADEMA?
5/Kwanini CHADEMA wako tayari kuhakikisha mkutano walioupanga lazima waufanye hata kama wamewekewa vikwazo na vitisho vya serikali na vyombo vya dola?
6/Kwanini CCM tuko tayari kuihujumu mikutano ya CHADEMA kwa gharama yoyote pale inapotakiwa kufanyika?
*Nitatoa maoni yangu na mapendekezo yangu positively, punde baada ya kupata majibu au ufafanuzi wa maswali yangu hapo juu.
Keep on watching!!!