Maisha+
Member
- Mar 9, 2013
- 76
- 6
Nadhani unakasirika tu bure mkuu, watanzania hivi sasa ndivyo wanachukulia CHADEMA kuwa ni wahuni hasa ukizingatia kuwa hakuna hata siku moja wamefanya mkutano bila kuwepo na vurugu, maandamano tena ya kulazimisha na vitu kama hivyo, unafikiri watu watawaelewaje? Ni vibaka na wahuni.
Sasa wewe ndio unataka kutuaminisha uongo kuwa ukweli. Wanaokwenda mikutano si wahuni kama unavyotaka tuamini, ni watu waliojikomboa kifikra, ni kundi kubwa la watu ambao wamekuwa sensitized ndio maana wanatembea kwa miguu kuifuata mikutano hiyo bila kubebwa kwenye malori na bila kupewa posho ya sh. 5,000. Mbona umati huo hatuuoni kwenye mikutano mingine ya vyama vingine?
Pamoja na kuongeza strategy nyingine, mikutano inatoa nafasi watu kufahamu sera za chama na kupata elimu ya uraia. Mikutano kama hiyo hawatoki watupu, amini nakuambia wengi hubadilika na kama walikuwa hawapigi kura sasa wanaamua kupiga kura, kama walikuwa hawajajiandikisha sasa watajiandikisha n. k. Kujenga chama is a long process.