Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
- Thread starter
- #21
Mikutano iendelee, na sasa zaidi maeneo ya vijijini. Umati kwenye mikutano haishawishi tu wahudhuriaji au wasikilizaji, bali kwa kiasi kikubwa unawaaminisha watu kwamba chama kiko hai. Hata mtu ambaye hajahudhuria, akiona umatu ule basi anashawishika kuwa chama kile kipo hai...
Wakati mikutano ikipamba moto, mikutano ya ndani nayo iimarishwe ili kusuka network imara kwa ajili ya kulinda kura wakati wa uchaguzi.
Jambo moja ni kwamba CDM imeanza kupata mwitikio mkubwa baada ya uchaguzi wa 2010. Na tangu wakati huo hakujawa na fursa ya watu kujiandikisha. Wengi wa wanaosapoti cdm ni watu wasioiunga mkono CCM na hawa, hawakujiandikisha kwa kuwa walidhani kwamba hakujawa na upinzani wa kutosha. Lakini sasa watu wengi wanaona nguvu ya upinzani na watajiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi ujao
Pamoja na maoni yako mazuri, kuna jambo ambalo naliangalisha sana katima mienendo ya siasa, mambo ya kufikirika zaidi yakwepwe inavyowezekana. Kwamba kuona umati ndio dalili njema za kuvutia watu ni jambo ambalo pengine linaweza kusababisha majuto wakati wa kupiga kura.
Pendekezo lako la mikutano ya ndani ndilo naliona lina uzito mkubwa sana na ndi siri ya mafanikio ya CCM. Kwenye mikutano ya hadhara kila mtu atanyosha mikono kuashiria kuunga mkoni lakisi sio watanyosha mikono kutumbukiza kura sandukuni.
Sina maana ya kupinga mikutano, lakini iwe ya mara chachaze zaidi ya mikutano ya ndani. Huko vitongojini wanakojifungia CCM ingieni nanyi mjifungie na wanavitongoji siri ya kura ndio huko. Jukwaani ni kutangaza seria kisha nendeni kuwafuata mlio wanadisha kura mitaani.