CHADEMA, punguzeni mikutano ingieni mitaani!

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
chadema+10.jpg

Mikutano ya hadhara imezoeleka kuvuta watu wengi. Mvuto huo wa watu wengi sijausahau tangu uchaguzi mkuu uliopita, lakini wahudhuriaji hawa walio wengi si wapiga kura, bali ni wazururaji, wasio na makazi maalum na wasio na kazi zinazowashinikiza kutohudhuria mikutano hiyo. Pengine wapiga kura katika umati kama huo hapo juu ni robo ya huo umati.

Chadema waige tabia ya mnyama mdogo sana anayeitwa FUKO ambaye anafurukuta na kufukua chini ya ardhi na kumaliza mihogo na viazi, mwenye shamba akija ni kuchomoa makuti ambayo matupu wakati viazi na mihogo imeliwa. Ndiyo tabia wanayotakiwa kuifanya sasa hivi Chadema.

Chadema baada ya kuelekeza nguvu za kanda, ni mbinu nzuri ambayo itaweka mwenya wa kupenya hadi ndani viijini, na mijini kupenya mitaani. Kuunda makada wa kuzunguka nyumba kwa nyumba kusaka na kuwashawishi wapiga kura.

Wapiga kura wazuri ni watu wenye makazi yao mitaani, na kuwapata wakazi ni huko mitaani wanakoishi, na kampeni za uchaguzi zinapofanyika ni huko mitaani unakuwa na hakina nani anapiga kura na anamwelekeo wa kukipigia chama au la. Kutegemea huu umati wa mikusanyiko mikubwa ni kwa nafasi chache sana na mara chache kwani tumejifunza walio wengi katika umati ule ni vibaka, wazururaji, wasio na makazi maalum nk.

Mpiga kura anakuwa na makazi maalum ndio maana kitambulisho chake kabla ya kupata lazima serikali za mitaa zitambue na kuridhia uwepo na ukazi wake.

Wapiga kura wazuri ni wale wenye makazi na wanapatikana mitaani kwenye makazi yao, sio wazururaji na wababaishaji mitaani.
Kuwa makini na makundi makubwa ambayo hayapigi kura lakini wahudhuriaji wazuri wa mikutano.

:nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono:​
 
Analysis ya kipuuzi sijawahi kuona tangu nizaliwe. Eti unawaita wanaohudhuria mikutano ya Chadema kuwa ni vibaka, wazururaji na watu wasio na makazi maalum?! Ulifanya utafiti gani kulibaini hilo? Hata kama ushauri wako ni mzuri kiasi gani, umeshauharibu kwa kauli zako za kashfa. Ulipaswa utambue umuhimu wa hayo makundi yanayojaza mikutano ya Chadema kisha utoe huo ushauri wako.
 
Nimeipenda sana comment yako, maana kinachoongelewa kikidharaurika matokeo ndio ya kulalamikia kuibiwa kura kumbe wenzako wanaofukua mitaani kama mnyama FUKO wamefanikiwa kuwakokotoa wapiga kura. Siasa za leo zinaendeshwa kisayansi.

Nadhani ungefahamu maudhui ya habari zaidi. Kundi kubwa hilo si wapiga. Nani aliye kazini ataacha kazi na kwenda mkutanoni kuanzia na wewe mwenyewe mdau utaacha kazi uende mkutanoni wakati unawajibika?
 
Mikutano na maandamano ndani ya CHADEMA ni zaidi ya siasa mkuu kama haujui, kuna siri nzito imejificha huko, suala la kupata kura na watu wachache kujitafutia umaarufu ni vitu viwili tofauti. Mikutano ile inayoambatana na maandamano ni mahsusi kwa ajili watu wachache kujipatia umaarufu ha haizalishi watachaguliwa au la ilimradi umaarufu huo unawawezesha wao kula. Usitemegee waache.
 
Siasa za kuwatembelea watu majumbani ni ngumu kwa sababu lazima uwe na hoja ya kuwaambia watu na vilevile ujiandae kuwa na majibu ya maswali watakayouliza. Chadema hawawezi kujibu hoja face to face ndio maana wanapendelea kupanda jukwaani kusema maneno wanayotaka halafu wanatawanyika.
 
Nafikiri hujamuelewa mtoa mada.......suala ambalo analizungumzia ni kuhusu strategy ambayo CDM wanaweza kuitumia....i.e. tumeshuhudia umati mikubwa kwenye mikutano mbali mbali ya CDM....lakini hiyo haikutosha ku-turn out into votes za ukweli in favor of CDM!!.....bado unataka kuamini wahudhuriaji wa mikutano ile ni for REAL!!......you must be joking......mwishowe ndio maana CDM wanaishia kulalama wameibiwa kura......

wenzenu Magamba mkiwaona wanapeleka "viduku" kwa wananchi mjue kuwa ile ni marashi tu....nguo za kuvaa (kura) zilishajulikana...............
 
Mikutano na maandamano ndani ya CHADEMA ni zaidi ya siasa mkuu kama haujui, kuna siri nzito imejificha huko, suala la kupata kura na watu wachache kujitafutia umaarufu ni vitu viwili tofauti. Mikutano ile inayoambatana na maandamano ni mahsusi kwa ajili watu wachache kujipatia umaarufu ha haizalishi watachaguliwa au la ilimradi umaarufu huo unawawezesha wao kula. Usitemegee waache.

Hilo ulilosema ndo tatizo kubwa ambalo siasa katika nchi za kiafrika ni kama viini macho. Kwa ufahamu wangu hiyo mikutano haiongezi idadi ya wapiga kura ingawa kwa namna fulani inasaidia kutangaza sera za chama. Ukweli ninaoufahamu wahudhuriaji walio wengi si wapiga kura, wapiga kura wengi ni watu waliotulia na familia nyingi mitaani na majumbani mwao.

Huko kwenye mikusanyiko ni kule wanakofika wale ambao hata ngurumo tu ya mvua watageuka kushangaa inatoka wapi ingawa ni kitu walichokizoea kukisikia tangu wazaliwe na kwamba inyeshapo mvuta na uwepo wa mawingu ngurumo huwepo. Lakini wao watafuata tu hata kama hawaihitaji mvuti inyeshe.
 
Nimeipenda sana comment yako, maana kinachoongelewa kikidharaurika matokeo ndio ya kulalamikia kuibiwa kura kumbe wenzako wanaofukua mitaani kama mnyama FUKO wamefanikiwa kuwakokotoa wapiga kura. Siasa za leo zinaendeshwa kisayansi.

Nadhani ungefahamu maudhui ya habari zaidi. Kundi kubwa hilo si wapiga. Nani aliye kazini ataacha kazi na kwenda mkutanoni kuanzia na wewe mwenyewe mdau utaacha kazi uende mkutanoni wakati unawajibika?

Hivi unaongea nini wewe? Unasema watu wanaokuja mikutanoni siyo wapiga kura halafu unaishauri Chadema iwafuate wapiga kura majumbani. Ina maana hao watu wanaokuja mikutanoni wanatokea mapangoni?
Kwa mtazamo wangu Chadema haipati idadi ya kura inayoendana na umaarufu wake kwasababu huwa haisimamishi wagombea wenye mvuto na wanaokubalika kwenye jamii. Chaguzi nyingi za chini zimekuwa zikigombewa na watu bora liende tu. Kinyume chake CCM wamekuwa wakizipa uzito mkubwa na kuweka watu ambao wanakubalika na kukusanya idadi ya kura inayozihitaji.
 
Siasa za kuwatembelea watu majumbani ni ngumu kwa sababu lazima uwe na hoja ya kuwaambia watu na vilevile ujiandae kuwa na majibu ya maswali watakayouliza. Chadema hawawezi kujibu hoja face to face ndio maana wanapendelea kupanda jukwaani kusema maneno wanayotaka halafu wanatawanyika.

Kwa maana hiyo.........wameshashindwa tayari.......

Hivi Jamani......hivi kweli CDM wanategemea mahudhurio yale ya mikutano ya hadhara ndio itawepeleka Ikulu kweli!!??......hivi CDM wameshashiriki chaguzi ngapi...ili ijifunze/kutambua kuwa wanatakiwa kufanya zaidi ya mikutano ya hadhara.......!!!.....kwa upande mwingine wale wachache waliohudhuria mkutano wa Lissu ndio wanaweza kuwa for Real.....
 
Analysis ya kipuuzi sijawahi kuona tangu nizaliwe. Eti unawaita wanaohudhuria mikutano ya Chadema kuwa ni vibaka, wazururaji na watu wasio na makazi maalum?! Ulifanya utafiti gani kulibaini hilo? Hata kama ushauri wako ni mzuri kiasi gani, umeshauharibu kwa kauli zako za kashfa. Ulipaswa utambue umuhimu wa hayo makundi yanayojaza mikutano ya Chadema kisha utoe huo ushauri wako.

Nadhani unakasirika tu bure mkuu, watanzania hivi sasa ndivyo wanachukulia CHADEMA kuwa ni wahuni hasa ukizingatia kuwa hakuna hata siku moja wamefanya mkutano bila kuwepo na vurugu, maandamano tena ya kulazimisha na vitu kama hivyo, unafikiri watu watawaelewaje? Ni vibaka na wahuni.
 
Siasa za kuwatembelea watu majumbani ni ngumu kwa sababu lazima uwe na hoja ya kuwaambia watu na vilevile ujiandae kuwa na majibu ya maswali watakayouliza. Chadema hawawezi kujibu hoja face to face ndio maana wanapendelea kupanda jukwaani kusema maneno wanayotaka halafu wanatawanyika.

Kama wameweza kuuza sera kwa wananchi na mafanikio yameanza wananchi kuamka usingizini na kudai haki zao, unafikiri itashindikana hilo? Au mbinu zinazotumiwa na CCM kuwapata wapiga kura unaona zitakuwa zimetifuliwa?
 
Kwa maana hiyo.........wameshashindwa tayari.......

Hivi Jamani......hivi kweli CDM wanategemea mahudhurio yale ya mikutano ya hadhara ndio itawepeleka Ikulu kweli!!??......hivi CDM wameshashiriki chaguzi ngapi...ili ijifunze/kutambua kuwa wanatakiwa kufanya zaidi ya mikutano ya hadhara.......!!!.....kwa upande mwingine wale wachache waliohudhuria mkutano wa Lissu ndio wanaweza kuwa for Real.....

Nadhani chadema wameamua kuwa kwa sasa focus yao siyo kusinda uchaguzi ila ni kupata umaarufu ili jina lao lizoeleke masikioni mwa watanzania na kuvipiku vyama vingine vya upinzani. Baada ya hatua hiyo kuota mizizi then wataanza kupanga mikakati ya kuingia ikulu.

Hata hivyo kwa jinsi siasa zilivyo, katika harakati za kutafuta umaarufu wanaweza "kuokota" urais kama dodo chini ya mnazi.
 
.............Kwa mtazamo wangu Chadema haipati idadi ya kura inayoendana na umaarufu wake kwasababu huwa haisimamishi wagombea wenye mvuto na wanaokubalika kwenye jamii. .......

....kwa mtazamo huo....ina maana kuwa una safari ndefu sana ya kufahamu nini maana ya politics za Tanzania.........Magamba/CUF kuna sehemu nyingi tu wamesimamisha wagombea wasio na mvuto wala kukubalika kwenye jamii na wagombea hao wakashinda uchaguzi.......Kigamboni, Rungwe (Prof Mwakyusa)..........Pemba.......hiyo ndio tunaita kuna "mashine" ndani ya chama husika..........
 
Hivi unaongea nini wewe? Unasema watu wanaokuja mikutanoni siyo wapiga kura halafu unaishauri Chadema iwafuate wapiga kura majumbani. Ina maana hao watu wanaokuja mikutanoni wanatokea mapangoni?
Kwa mtazamo wangu Chadema haipati idadi ya kura inayoendana na umaarufu wake kwasababu huwa haisimamishi wagombea wenye mvuto na wanaokubalika kwenye jamii. Chaguzi nyingi za chini zimekuwa zikigombewa na watu bora liende tu. Kinyume chake CCM wamekuwa wakizipa uzito mkubwa na kuweka watu ambao wanakubalika na kukusanya idadi ya kura inayozihitaji.

Hoja yako ya chama kutosimamisha wagombea bora naikubali. Lakini kwa upande mwingine hujaelewa ninachoongelea kwamba ukipiga baragumu kuita watu mkusanyiko wa ghafla watakaoitikia mara moja ni wale wasio na kazi maalum na pengine wasio na kazi. Walio makazini itawawia vigumu kwani itabidi wapate ruhusu kwa mwajiri na sababu ziwe nzito na hao waaajiriwa ndio walio wengi wapiga kura. Waliojiajiri hali kadhalika wataangalia mambo mengi umuhimu wa kwenda mkutanoni au kuendesha shughuli yake inayomfanya aishi.

Kwa vyo vyote kuna kitu ambacho kinatakiwa kibadilike kwa kubuni mbinu bora zaidi za kupata wapiga kura. Kama sera zao zinaeleweka na wananchi wameshawasikia sana tu. Je, kwa mikutano hiyo kwa umati huo uliozoeleka unasaidia kuongeza kura kwenye ballot box au ni wahudhuriaji tu?
 
Kila siku hakuna wanachozungumza zaidi ya ufisadi kwanini watu wasiwachoke.Wabadilishe maneno kwenye mikutano yao basi
 
Nadhani chadema wameamua kuwa kwa sasa focus yao siyo kusinda uchaguzi ila ni kupata umaarufu ili jina lao lizoeleke masikioni mwa watanzania na kuvipiku vyama vingine vya upinzani. Baada ya hatua hiyo kuota mizizi then wataanza kupanga mikakati ya kuingia ikulu.

Hata hivyo kwa jinsi siasa zilivyo, katika harakati za kutafuta umaarufu wanaweza "kuokota" urais kama dodo chini ya mnazi.
ZeMarcopolo
Umeandika wazo zuri sana na ndilo naliongelea. Umeshashuhudia mijini hata vijijini kikitokea kitu kidogo tu watakusanyika hapo na kushangaashangaa na kutawanyika itawachukua muda, hao ndio wanaojaza mikutano ya Chadema. Hao ndio wanaojaza mikutano ya vyama vya upinzani kwenye kampeni ambao hawapigi kura bali ni mashabiki tu.

Cheers wa timu hawafungi magoli bali wachezaji wasajiliwa walio uwanjani ndio wafungaji wa magoli.
 
Kila siku hakuna wanachozungumza zaidi ya ufisadi kwanini watu wasiwachoke.Wabadilishe maneno kwenye mikutano yao basi

Hahaha! Hiyo imeshachuja, wajitahidi kufuata ushauri, maana naona hiyo mikutano pengine inaingiza gharama nyingi labda wanaipendelea sababu ya mapato ya michango ya wananchi ya papo kwa papo? M-pesa haiwezi kutumika? Hata michango inaweza kuwa mizuri huko wanakoishi watu.

Chadema ifuate wapiga kura si wao kudanganyika kwa kufuatwa mikuanoni na watu wengi ambao wengi wao si wapiga kura.
 
Hoja yako ya chama kutosimamisha wagombea bora naikubali. Lakini kwa upande mwingine hujaelewa ninachoongelea kwamba ukipiga baragumu kuita watu mkusanyiko wa ghafla watakaoitikia mara moja ni wale wasio na kazi maalum na pengine wasio na kazi. Walio makazini itawawia vigumu kwani itabidi wapate ruhusu kwa mwajiri na sababu ziwe nzito na hao waaajiriwa ndio walio wengi wapiga kura. Waliojiajiri hali kadhalika wataangalia mambo mengi umuhimu wa kwenda mkutanoni au kuendesha shughuli yake inayomfanya aishi.

Kwa vyo vyote kuna kitu ambacho kinatakiwa kibadilike kwa kubuni mbinu bora zaidi za kupata wapiga kura. Kama sera zao zinaeleweka na wananchi wameshawasikia sana tu. Je, kwa mikutano hiyo kwa umati huo uliozoeleka unasaidia kuongeza kura kwenye ballot box au ni wahudhuriaji tu?

Unajijachanganya sana mkuu unaposema watu wanaokuja mikutanoni ni watu wasio na kazi na wasio na makazi. Kama unahisi kuwa idadi kubwa ya wapiga kura ni watu wenye kazi na makazi basi utakuwa unajidanganya sana. Kwa taarifa yako ni asilimia mbili ya hao watumishi wako unaowathamini na kuwalenga ndiyo huwa wanaojitokezaga kupiga kura siku ya uchaguzi.
Sababu za Chadema kutoshinda chaguzi kama inavyotarajiwa inaenda zaidi ya kutopata idadi ya kura za kutosha. Pamoja na kutosimamisha wagombea wanaokubalika, kuna tatizo la nchi kiujumla la watu kutojitokeza siku ya uchaguzi. Hili sidhani kama lipo ndani ya uwezo wa Chadema kusuluhisha, kwasababu linahitaji elimu zaidi itolewe kwa watu kuelewa umuhimu wa kupiga kura kwenye maisha yao.
Chadema wanaweza kugonga hodi kila nyumba, lakini kama watu hawajaona uhusiano kati ya kupiga kura na mabadiliko yao hakuna kitakachotokea.
 
Ulilolijadili ndiloninaloliongelea. CCM ushindi wao ni kutokana na kuhakiki na kuhakikisha wapiga kura wao kuanzia shina, matawi na vitongoji, wakati Chadema wanategemea mkusanyiko wa mikuano ambao hauhakikishi nani kati ya wahudhuriani ni mpiga kura. Hilo ndilo linalotakiwa kufanyiwa kazi, na upatikanaji wa wapiga kura hali kadhalika kuhakiki wanachama hai ambao watakipigia chama kura ni huko kwenye vitongoji wanakoishi. Hii ndiyo siri ya ushindi wa CCM ambao chadema wanatakiwa kuipiku CCM kwani dawa ya moto ni moto ati.
 
Mikutano iendelee, na sasa zaidi maeneo ya vijijini. Umati kwenye mikutano haishawishi tu wahudhuriaji au wasikilizaji, bali kwa kiasi kikubwa unawaaminisha watu kwamba chama kiko hai. Hata mtu ambaye hajahudhuria, akiona umatu ule basi anashawishika kuwa chama kile kipo hai...
Wakati mikutano ikipamba moto, mikutano ya ndani nayo iimarishwe ili kusuka network imara kwa ajili ya kulinda kura wakati wa uchaguzi.
Jambo moja ni kwamba CDM imeanza kupata mwitikio mkubwa baada ya uchaguzi wa 2010. Na tangu wakati huo hakujawa na fursa ya watu kujiandikisha. Wengi wa wanaosapoti cdm ni watu wasioiunga mkono CCM na hawa, hawakujiandikisha kwa kuwa walidhani kwamba hakujawa na upinzani wa kutosha. Lakini sasa watu wengi wanaona nguvu ya upinzani na watajiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi ujao
 
Back
Top Bottom