CHADEMA ni tawi tiifu la CCM

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
16,567
2,000
Ndugu zangu,

Huwa ninasema na nitaendelea kusema kuwa CHADEMA ni tawi tiifu la CCM. Hata sasa mijadala ya kisiasa inayoendelea wafuasia wa Chadema ni "follower" wa makada wa CCM. utasikia "Samia amteue fulani amuache fulani" au "urais mwaka Fulani twende na fulani"..


Nimeambatanisha uzi nikionyesha jinsi kada wa CCM anavyofanya kazi ndani ya Chadema kama Mwenyekiti.

Mbowe katangaza kuwa Chadema haitashiriki uchaguzi wowote nchini, hii ni dhahiri anataka kuhakikisha CCM inashika hatamu kwenye kila nyanja bila kupingwa.

Tuendelee kusubiri
 

Themagufulianz

JF-Expert Member
Apr 15, 2017
4,510
2,000
Wakimbizi wasanii wawili?
Wenye hilo tawi la CCM ndiyo hawa hawa mliowaibia kura, mkawaambie pita mali zao, mkawauwa, wengine wao wakakimbilia ukimbizini nk?

Inabidi uwe na dishi lililoyumba kuwa na mawazo kama yako mjomba.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
8,284
2,000
Wakimbizi wasanii wawili?

Wakimbizi ambao aghalabu mabalozi wazito wazito walilazimika kuhakikisha wanakimbia salama kuepuka meno ya mamba watoa roho za watu nyie, wanakuwaje ghafla wanachama wenu watiifu?

Mnaowaita wanachama wenu watiifu nao wanayaridhia hayo au ni kuwa mnajitekenya na kucheka tu?

Madishi yenu yako sawa kweli? Au ni kiwewe cha awamu ya tano kusambaratishwa ghafla na aliye bwana wa majeshi ya ukweli?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom