CHADEMA ni kama vile mmetususia Watanzania

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
13,960
Reaction score
26,135
Mambo ya hovyo yanafanyika hapa nchini na nyinyi mpo tu hata hamtoi matamko wala kumobilize watu tuandamane.

Hali ngumu ya maisha imetawala na ndio kwanza tabaka tawala wao wanafuja mali za umma tu kutwa kuzurura na midege yetu huko angani.

Nchi ni kama haina kiongozi mkuu kwa sasa kwani kila mtu anajiamlia mambo yake mwenyewe.
Chadema nyinyi ndiyo wa kutuvusha kwenye hili,msitususe tafadhali.
 
Bwashee kama bado unawategemea chadema 'to get your back' imekula kwako. Chadema ya hivyo aliondoka nayo Dr slaa, hii ya sasa ni porojo tu
Jamani chadema imekufa hata CCM wanajua hilo
20220414_215028.jpg
 
Ni kweli miaka ya nyuma tulikuwa tunawaona CHADEMA na vyama vingine vya upinzani pamoja na wasomi maarufu wanakuja kutupa ufanunuzi kwa lugha rahisi juu ya report ya mkaguzi mkuu. Na baadaye wanakuja tena kutufafanulia bajeti mara tu inapotangazwa. Sasa mwaka huu ripoti ya mkaguzi mkuu imeshatoka lakini naona wapo kimya sijui wamepigwa ganzi na nini.
 
Mambo ya hovyo yanafanyika hapa nchini na nyinyi mpo tu hata hamtoi matamko wala kumobilize watu tuandamane.
Hali ngumu ya maisha imetawala na ndio kwanza tabaka tawala wao wanafuja mali za umma tu kutwa kuzurura na midege yetu huko angani.
Nchi ni kama haina kiongozi mkuu kwa sasa kwani kila mtu anajiamlia mambo yake mwenyewe.
Chadema nyinyi ndiyo wa kutuvusha kwenye hili,msitususe tafadhali.
Mnaitaka Chadema ya nini wakati mnaiombea usiku na mchana ife? Tulieni dawa iingie hadi kwenye misuli ya seli.
 
Ni kweli miaka ya nyuma tulikuwa tunawaona CHADEMA na vyama vingine vya upinzani pamoja na wasomi maarufu wanakuja kutupa ufanunuzi kwa lugha rahisi juu ya report ya mkaguzi mkuu. Na baadaye wanakuja tena kutufafanulia bajeti mara tu inapotangazwa. Sasa mwaka huu ripoti ya mkaguzi mkuu imeshatoka lakini naona wapo kimya sijui wamepigwa ganzi na nini.
Hiyo miaka ya nyuma CDM wakishatoa huo ufafanuzi kuhusu report ya CAG huwa mnachukua hatua gani?

By the way Leo Mbowe akiwa Sinza ametoa neno kuhusu ufisadi uliojaa kwenye report ya CAG.
 
Inatusaidia wakati wa uchaguzi tujue tunampigia kura mgombea gani na wa chama kipi.
 
Mbowe sijui aliambiwa nini pale Ikulu. Nadhani kuna makubaliano fulani yalifikiwa.
 
Walio uuwa upinzani na wao waliuwawa, Wakitekwa na kubambikiziwa kesi hamleti ata uzi wa kuwatetea Tunabaki kuona uzi wa Mboga mboga ukipongezana, Leo kwenye magum yenu Mnawahitaji mmesahau waliwapambania mkawageuka na wao ikabidi wakubali kununuliwa wawe upande wa kijani ili walishe family zao, CDM Endeleeni kuvunga
 
Anafanya mambo akiwa amepoa. Mi mpaka nisikie kongamano la katiba tena, ndio nitaamini. Haya mambo ya kupita mtaani na kundi la watu 10, naona ni utani tu.
Uje ufute hii baada ya kuona video ya Mbowe ya leo akiwa Sinza ametoa neno kuhusu ufisadi ulifanywa na kuwekwa wazi kwenye report ya CAG na ametoa mapendekezo yake.
 
Chadema watuletee Ndugai tumtingishe Mama kikweli kweli
 
Mambo ya hovyo yanafanyika hapa nchini na nyinyi mpo tu hata hamtoi matamko wala kumobilize watu tuandamane.
Hali ngumu ya maisha imetawala na ndio kwanza tabaka tawala wao wanafuja mali za umma tu kutwa kuzurura na midege yetu huko angani.
Nchi ni kama haina kiongozi mkuu kwa sasa kwani kila mtu anajiamlia mambo yake mwenyewe.
Chadema nyinyi ndiyo wa kutuvusha kwenye hili,msitususe tafadhali.
Tumewaacha kidogo nyie wenye nchi
 
Nimefurahi sana kuona Uzi huu.

Kila kitu kimeharibika kifupi disco limeingia Masai.

1. Bunge limepoooa kama kikao Cha vikoba au Cha msiba. Halivutii hata kuangalia sembuse kusikiliza. Watu wenye mvuto hawapo. Kipindi hicho tukisomewa ratiba za nani atachangia basi hata bar mziki unazimwa tunasikiliza Mnyika, Sugu, Lema, Mbowe au Tundu Lissu anachangia.

Baada ya hao kutoa mchango wao basi DJ anafungulia mziki - bunge la Anna Makinda na Samwel Sitta.

2. Tangu uchafuzi wa 2020 kufanyika wananchi hatujui hata majina ya mawaziri. Serikali imepooooooaaaa kama maji ya bwawani. Serikali Haina mvuto.

Mlimwacha yule marehemu ameharibu utaratibu Kila kitu kiko hovyooo.

Sasa limekufa alafu imeshindikana hata kurekebisha.

Bunge limekiwa kikao Cha CCM.
 
Back
Top Bottom