Nimefurahi sana kuona Uzi huu.
Kila kitu kimeharibika kifupi disco limeingia Masai.
1. Bunge limepoooa kama kikao Cha vikoba au Cha msiba. Halivutii hata kuangalia sembuse kusikiliza. Watu wenye mvuto hawapo. Kipindi hicho tukisomewa ratiba za nani atachangia basi hata bar mziki unazimwa tunasikiliza Mnyika, Sugu, Lema, Mbowe au Tundu Lissu anachangia.
Baada ya hao kutoa mchango wao basi DJ anafungulia mziki - bunge la Anna Makinda na Samwel Sitta.
2. Tangu uchafuzi wa 2020 kufanyika wananchi hatujui hata majina ya mawaziri. Serikali imepooooooaaaa kama maji ya bwawani. Serikali Haina mvuto.
Mlimwacha yule marehemu ameharibu utaratibu Kila kitu kiko hovyooo.
Sasa limekufa alafu imeshindikana hata kurekebisha.
Bunge limekiwa kikao Cha CCM.