CHADEMA ngoma mbichi Arusha

Nasikia HARUFU ya Madiwani waliofukuzwa Chadema kuja hapa na KUBWABWAJA, au ndugu zao?

Nawaomba wawalilie CCM ili ile sheria ya WAGOMBEA HURU ipitishwe Chap Chap na hawa jamaa wataendelea kuwa MADIWANI.

Vinginevyo basi walie tu. Ni kweli hawa jamaa HAWAJAFUKUZWA Udiwani. Wamefukuzwa ndani ya Chama.

Mengine hayo yanayofuata ni CCM EFFECT.

Ni utovu wa nidhamu kujiamulia mambo kama hayo ya kukubaliana na muuaji aliyeua watu unaowatumikia bila ya makubaliano ya pamoja na viongozi wakuu wa chama.

Kwa vile CDM siyo kama Magamba inabidi wachukue hatua ambazo zitaonekana waziwazi ili iwe kielelezo cha kwamba, hata wakitawala wako tayari kuchukua maamuzi magumu bila kuangalia nani ana nini!

CDM mlichofanya nawapongeza sana.

Wajue wasaliti wa Chadema na wananchi

L-R: Estomih Mallah(Kimandolu), John Bayo(Elerai), Ruben Ngowi(Themi), Rehema Mohamed(Special Seat) and Charles Mpanda(kaloleni).

Kweli kuna kitu kinanipanda ninaporudishwa kuwafikiria "Madiwani waliofukuzwa" Sahihisho nijuavyo mimi wamefukuzwa uanachama CDM kwa hiyo mimi nakushauri elekeza mawazo yako kwenye kuboresha siasa za Arusha hata kama ni kufikiria ubora wa CCM ambao sisi wa Arusha hutuuoni.

Labda nikupe wazo la kufikiri. Kwani lazima kuwa madiwani? Kama jibu ni ndio wakatafute chama cha kugombea mbali na CDM.

1. matakwa ya chadema hayatekelezeki

2. wananchi wanataka kuona mabadiliko tangu wapewe madaraka

3. mbunge hakupita kuchukua hoja za kwenda nazo bungeni kutoka kwao pia hana msaada kwao mfano hakupita kwenye kata zao kuchukua wagonjwa na kuwapeleka kwa babu

4. kutuhumiwa kuchukua rushwa kitu ambacho sio kweli na hili ndiyo wanataka kufungua kesi ili chadema iwasafishe kwenye mikutanoitakayofanywa na chadema, hayo ni baadhi ya madai yao ila ngongo akija atayaelezea vema zaidi..

Asante sana mwakilishi wao sikuwa naelewa kumbe kupeleka wagonjwa kwa babu ni jukumu la mbunge ngoja nimtafute mbunge wangu.

mkuu kuna siku dr slaa alianzisha thread na aliliweka vema sana swala hili hakika kama ningekuwana pc ningeyaweka hapa..hawa jamaa waliokuwa madiwani mwanzo walipewa rungu la kutafuta mwafaka kabla ya tarehe 29.4 kuzuiliwa ili mbowe na waziri mkuu pinda waendelee na majadiliano baada yapo wao wakaendelea na majadiliano huku wakiwafisha baadhi ya madiwani je kama kulikuwa na nia njema kwanini waliendelea na majadiliano tena kwa siri kwanini siku ya uchaguzi naibu meya haukutangazwa

Asante sana mwakilishi wao sikuwa naelewa kumbe kupeleka wagonjwa kwa babu ni jukumu la mbunge ngoja nimtafute mbunge wangu.
jamani msinisakame bure mimi nimemjibu huyo alieuliza madai yao..na kwa ukweli nimekuwa nikiwasiliana na madiwani hawa kujua madai yao lakini kamwe siwaungi mkono..nisomeni vizuri mabandiko yangu

Thanks

Madiwani hawakufukuzwa kwa kosa la kuingia kwenye muafaka wala kupokea rushwa. Point ya msingi ni kwamba walikaidi maagizo halali ya kamati kuu.

Kumbuka kuwa kamati ni chombo cha mwisho cha maamuzi ndani ya chama. Hivyo kilichotakiwa ilikuwa nikutekeleza agizo halali ya kamati kuu, then kama wana complains zozote ndio wanatoa.

Amri lazima itekelezwe. Viva chadema kwa maamuzi magumu

Hivi hata wewe crashwise umeshachakachuliwa?
haha haha..mkuu usinichekeshe wakati nina hasira..ongopa mtu una msapoti kwa hari na mali..leo anasimamia madai kama eti mbuge hana msaada wowote hakuja kuchukua wagojwa kwenye kata yangu kwenda kwa babu kweli huyu ndie diwani tulie mhangaikia..

CDM kazi wamemaliza na wamerudisha heshima ya chama. Wahuni hawana nafasi ndani ya chama makini.

Hivi hata wewe crashwise umeshachakachuliwa?
Mimi namweshimu sana crashwise kwa jinsi anavyotuletea habari za AR lakini siku za hivi karibuni anaonekana kama kaumizwa na kitendo cha madiwani kufuzwa ila bado anajitahidi sana ku balance habari asionekane yuko upande gani.

Mkuu umemaliza, kwani lazima wakafanye uhuni ndani ya CDM?

mkuu freedom of flag, tunachojaribu kukiangalia ni kwanini hawakutii mapendekezo ya kamati kuu pamoja kushauriwa na watu mbalimbali mfano mzee mtei..

Mkuu umekamilisha yote
Nidhamu,heshima na uwajibikaji,kuogopana, kubembelezana,kupigiana magoti ni mwiko!
Hatuwezi kuendesha mambo kama Magamba!

CDM kazi wamemaliza na wamerudisha heshima ya chama. Wahuni hawana nafasi ndani ya chama makini.

Kamanda umemaliza na sina la nyongeza. Twanga kotekoteeeeeeeeeeeee!!

Mimi sina wasiwasi kabisa hata samaki akivuliwa huwa hafi mara moja atarukaruka baadae atanyooka mwenyewe

hata hawa tuwape muda tutawasahau muda si mrefu.

mia

Saharavoice,
Afadhali tukose viti in the short term ili tujenge uongozi bora in the long term.

ni kweli kabisa na hili nampongeza sana dr slaa chama lazima kiwe imara kuliko kuyumba yumba na in future kitadhaminika sio magamba wanaogopana wao kwa wao ndio maana EL anawaambia mkiwaga mboga namwaga ugali!!

na hiyo isiishie hapo tu iende mbali kuondoa watu wanafiki, wasifuata utaratibu then mtaheshimika kwenye kusimamia msimamo! hope mgekuwa madarakani mgekuwa mshawafutilia mbali leseni wauza mafuta kwa kugoma!

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…