CHADEMA nawapongeza sana kujigawa kikanda kueneza chama

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Huu utaratibu wenu naona umekua wa mafanikio sana na umuwasaidieni kuwafikia wananchi kwa haraka sana.
Nimeona jinsi viongozi wenu wa kanda walivyojipambanu siku ya mkutano mkuu wenu, inaonekana kila kanda inawajibika ipasavyo. Pengine hiki ndicho kitu ambacho kimemfanya chama chenu kuanguka na zaidi kimeimarika. Hongereni sana, Hongera Dr Mashinji kwa kuiratibu mipango hii vizuri ingawa upo CCM kwa sasa

Kazi kubwa sasa nimeona inafanywa kwa kiasi kikubwa na wenyeviti na makatibu wa kanda pamoja na idara zake za kanda. Nimeona kila mahali nchini anakofika Tundu Lissu uungwaji mkono mkubwa sana kumbe ni matunda ya kanda hizi.

USHAURI KWENU
Imarisheni zaidi ofisi zenu za kanda ikiwa ni pamoja na maslahi ya viongozi wa kila kanda.Kanda hizi zinafanya kazi kubwa kuliko hata kurugenzi zenu za makao makuu. Ziimarisheni ofisi zenu za kanda kuliko hata makao makuu. Kwani mpaka sasa uhai wa chama chenu ni kwa sababu ya kanda hizi

Hawa viongozi wa kanda ndio Viongozi wakuu wa chama baadae, waandaeni vizuri maana ndiko watakapopatikana makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu wa chama. Mwenyekiti wa chama anatakiwa awe pia ni zao la chama
 
USHAURI KWENU
Imarisheni zaidi ofisi zenu za kanda ikiwa ni pamoja na maslahi ya viongozi wa kila kanda.Kanda hizi zinafanya kazi kubwa kuliko hata kurugenzi zenu za makao makuu. Ziimarisheni ofisi zenu za kanda kuliko hata makao makuu. Kwani mpaka sasa uhai wa chama chenu ni kwa sababu ya kanda hizi.
Ushauri mwema sana Mwanahabari Huru
 
Mimi nawapenda wapinzani wote maana ndiyo wanaochochea Maendeleo,

Na ikumbukwe kuwa kanuni ya Uumbaji Ni vitu viwili viwili, Usiku,Mchana, Mke,Mume,Shida,Raha,Unanja,Ujinga. Hata Bungeni kuna Waziri na Waziri kivuli.

Kuuchukia upinzani Ni kukosea hata kanuni ya Maisha na Uumbaji wa Mungu.
 
Mimi nawapenda wapinzani wote maana ndiyo wanaochochea Maendeleo,

Na ikumbukwe kuwa kanuni ya Uumbaji Ni vitu viwili viwili, Usiku,Mchana, Mke,Mume,Shida,Raha,Unanja,Ujinga. Hata Bungeni kuna Waziri na Waziri kivuli.

Kuuchukia upinzani Ni kukosea hata kanuni ya Maisha na Uumbaji wa Mungu.
Sawa kabisa! Waziri mkuu leo kesho anakuwa waziri mkuu kivuli! Ukitaka kuongoza ukubali kuongozwa
 
Back
Top Bottom