Kama binadamu wote na mimi nina hisia za mapenzi, mapenzi yananoga yakitanguliwa na imani yaani kuwepo kuaminiana. Huyu kimwana CHADEMA nampenda kwelikweli kama vijana wengi marijali wanavyompenda lakini simuamini sana kama kweli ana mapenzi ya dhati kiasi cha kumkabidhi moyo wangu. Namuona kama mjanjamjanja tu kwenye lengo mahsusi na rasirimali zetu pale tutakapomkubalia na kuingia katika mapenzi naye kichwa kichwa, naomba ushauri wadau!