Chadema nakupenda lakini sikuamini

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Kama binadamu wote na mimi nina hisia za mapenzi, mapenzi yananoga yakitanguliwa na imani yaani kuwepo kuaminiana. Huyu kimwana CHADEMA nampenda kwelikweli kama vijana wengi marijali wanavyompenda lakini simuamini sana kama kweli ana mapenzi ya dhati kiasi cha kumkabidhi moyo wangu. Namuona kama mjanjamjanja tu kwenye lengo mahsusi na rasirimali zetu pale tutakapomkubalia na kuingia katika mapenzi naye kichwa kichwa, naomba ushauri wadau!
 
Kama binadamu wote na mimi nina hisia za mapenzi, mapenzi yananoga yakitanguliwa na imani yaani kuwepo kuaminiana. Huyu kimwana CHADEMA nampenda kwelikweli kama vijana wengi marijali wanavyompenda lakini simuamini sana kama kweli ana mapenzi ya dhati kiasi cha kumkabidhi moyo wangu. Namuona kama mjanjamjanja tu mwenye lengo mahsusi na rasirimali zetu pale tutakapomkubalia na kuingia katika mapenzi naye kichwa kichwa, naomba ushauri wadau!
 
Mkuu Mwakidondo sitofautiani sana na wewe, hata hivyo jina lako limenifurahisha sana wee mnyalu!!!
 
Mkabidhi "magamba" moyo wako, who cares????? Nyinyi si ndio wale mliozoea kudanganywa? Endelea kuvaa hayo magamba wakati wenzio wanayavua.
 
utakuwa unamatizo kichwa, unawezaje kumpenda mtu au kitu usichokiamin. Kaa mbali na sisi kama mezoea kutoamniana hukohuko. M4C FOR LIFE.
 
kama humuamini kimwana chadema ambaye ni bikra basi nenda kwa gumegume lyenzako chama cha matapeli(???) ambalo wanaume wenzako wazee kwa vijana wamelichoka
 
wakuu mbona mnakuwa wakali hivyo? mimi bado sija-lose hope na Chadema ndiyo maana nimeomba mwenye uelewa wa ndani kabisa wa CDM anisaidie ili nifanye maamuzi sahihi. Kabla sijajitoa rasmi kwa CDM ambao mko deep mnijuze ili nisijekuwa nadandia gari la taka bila kujua.
 
Mi nakereka sana na mijitu inayojiona yenyewe ndo chadema halisi.Badala ya mshauri mtu yenyewe yanaanza kutoa mapovu.Mtu amesema anakipenda chadema huyu ni wakumweka sawa tu kwa hoja na sio kama matahira mengine yanayotaka kuharibu mwelekeo.
 
Kwa kuwa umetumia mfano wa kimwana na kusema humwamini, basi ungetoa mfano kwa kusema labda unamwona akizungumza ovyo na kila mtu au kitu kama hicho.

Kusema kweli nimekuelewa. Hata TANU ilipoanza kuna watanganyika wengi waliona ni chama uchuro tu! Tena mbele ya serikali ya mkoloni! Vivyo hivyo,mtu waweza kuwa na waswas wa Chadema mbele ya ccm!

Kwa bahati mbaya sana ccm ya sasa siyo ile TANU ya 1960 au ccm ya 1980. Chama kimebadilika sana kiasi cha kuwasahau wananchi wajitafutie wenyewe kama kuku wa kienyeji. Sasa yapo mawazo mapya na mwelekeo mpya na mitazamo mipya.Hivi vitu vipo CHADEMA

Nimalize kwa kukuambia, usichelewe kaka utakuta mwana si wako. Karibu utoe posa!
 
Achana kabisa na mademu wa kipalestina ( machame) utakuja kujuta! Wako kibiashara zaidi!
 
Kama binadamu wote na mimi nina hisia za mapenzi, mapenzi yananoga yakitanguliwa na imani yaani kuwepo kuaminiana. Huyu kimwana CHADEMA nampenda kwelikweli kama vijana wengi marijali wanavyompenda lakini simuamini sana kama kweli ana mapenzi ya dhati kiasi cha kumkabidhi moyo wangu. Namuona kama mjanjamjanja tu mwenye lengo mahsusi na rasirimali zetu pale tutakapomkubalia na kuingia katika mapenzi naye kichwa kichwa, naomba ushauri wadau!

Hapo kwenye red, kweli raslimali tunazo, ila tatizo ni nani anafaidi hizo raslimali kwa hivi sasa.
Pole sana kwa kuwa na wasiwasi na raslimali zetu, maana nakuona kama mnafiki vile.
Kwanini nasema hivyo:-
Raslimali hizo zoote unazozizungumzia wewe zimeshaporwa zamani sana na mafisadi na wawekezaji. Hivyo hakuna kilichobakia cha kukitilia shaka kuwa kitaporwa na chadema. Kwa ufupi zote zimeshaporwa. Mpaka wanyama pori nao wanaenda.
Hakuna raslimali iliyobaki, hivyo hao chadema wakiingia madarakani, hata wakitaka kupora hawataweza maana hawatakuta raslimali yoyote iliyobaki.
Hivyo kusema una wasiwasi na raslimali zetu ni unafiki tu, hizo raslimali zilishaporwa zamani saaaana.
 
..haya uliyosema ni kweli hawa watu hawaaminiki kabisa,ni movement for killing,kila mtu anatafuta maslahi yake hapa wasitudanganye

Dah eti movement for killing!!!! Hivi CHADEMA wameshaua Watanzania wangapi tangu chama hicho kianzishwe!? Magamba Vingwendu mauaji yao mbona hukuyasema!?

...We endelea na mapenzi yako na Magamba Vingwendu na ahadi zake chungu nzima za kuboresha maisha yako lakini miaka inakatika nawe bado maisha yako yako shaghalabaghala. Bado unaishi kwenye nyumba ya mbavu za mbwa, umeme na maji alioahidi kukuvutia hadi kwenye kibanda chenu imebaki kuwa ni hadithi yenye mlolongo mrefu, mlo wako mmoja kwa siku hujui utapatikana vipi lakini bado unadai una mapenzi na Magamba Vingwendu!!!!! Kama usipojipenda mwenyewe na kumtafuta mtu mwenye mapenzi ya kweli kwako basi ukae kimya tumechoka kusikia malalamiko yako miaka nenda miaka rudi kuhusu vipigo unavyovipata toka kwa mpenzi wako Magamba Vingwendu na jinsi maisha yenu yanavyozidi kudidimia kila mwaka na huku wenzio na wapenzi wao wengine maisha yao yanaimarika kwa kasi ya kutisha...Pole zako nyingi kwa kuwa na mawazo mgando.

Hii hoja ya Mwakidondo yaweza kuwa taken easy and lightly......but it sound like a million dollar question kwa atakayeamua kuichukua kwa uzito wake

I mean hoja na sio maneno aliyotumia
 
Back
Top Bottom