Miss Madeko
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 4,420
- 5,700
Mngekuwa mnafanya mambo yenu kisayansi, hii ilikuwa ni fursa yenu nzuri sana ya kuanzia kampeni zenu, kuanzia sasa na kwenda mbele.
Mngekuwa mmejipanga vizuri kunasa namba sahihi ya:
- waTanzania waliojiandikisha kupiga kura
- waTanzania waliojitokeza kupiga kura
- sababu hasa zilizosababisha kuwepo upungufu, kama namba zenu hizo zitawaonyesha hivyo
- ni maeneo yapi hasa ya nchi yanayohitaji kulengwa kwa karibu na ufuatiliaji wa mara kwa mara
- ni viongozi (watu) gani hasa kwenye jamii mnaotakiwa kuwalenga ili kazi yenu ifane, n.k,. n.k.
Haya yote yangewasaidia kuelekeza nguvu zenu huko huko wananchi wanakoelekea ili kuwasaidia kujipanga vizuri kukabili yajayo.
Kwa bahati mbaya sana Erythro, mipango yenu bado mnaifanya kishaglabagara na kama kubahatisha tu, kama unavyotueleza katika mada yako hii.
Namba za hayo unayosema hapo zipo wapi na wapi?
Kazi ya kufanya siasa ni aina ya sayansi fulani. Inazo taratibu zake, sio kurukia tu mambo.
Kuna wakati, miaka michache iliyopita niliwaona kama mmeanza kuelekea huko, lakini hapa katikati, mmeonyesha kuvurugwa sana, na zile hatua za mwanzo mlizokuwa mmezianza zote zimepotea.
Ajabu ni kwamba, ruzuku yenu iliongezeka, na kila mtu angetegemea muitumie vizuri kuwafundisha vijana wenu wafanye kazi zao kisayansi, - matokeo yanaonyesha kinyume cha hapo!
Hata kuajiri ma-'consultant', nguli wa mambo haya kwa muda tu pia imewawia vigumu? Raslimali zenu mmezitawanya wakati ambapo mlitakiwa mzitumie kwa makini sana wakati huu ambao mabavu yanatumika kuwamaliza.
Haya maguvu mngeweza kuyapiku kwa kutumia sayansi, huku mkitumia akili zaidi.
Ona sasa mnavyoendeshwa!
KNCU
Waliojiandikisha 166
waliopiga kura
CCM 21
TLP 6