CHADEMA na wapinzani wameshinda

CHADEMA na wapinzani wameshinda

Hii ni baada ya kampeni yao ndogo sana na ya muda mfupi ya kuhamasisha wananchi kususia uchaguzi feki wa serikali za mitaa kuungwa mkono na wananchi kwa zaidi ya 90%, hii ni rekodi.

Kwa mfano, msimamizi mmoja wa kituo cha uchaguzi jijini Dar es salaam ametoa siri kwamba kati ya watu zaidi ya 500 waliojiandikisha, waliopiga kura hawakufika 50, hii ni pamoja na wale wanaojifanya wanaccm, maana ya jambo hili ni kwamba ccm imekataliwa hata na wanaojiita wanachama wake yenyewe, hii ni hatua kubwa sana na ya kujivunia kwa wapinzani, maana sasa ni wazi kwamba wamefanikiwa mipango yao ya kupenya kwenye ngome za ccm na hivyo kujitengenezea mtaji wa baadaye.

Hakika Utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana!

======
Maoni ya wadau
Takwimu na uhalisia zinakusuta. Isitoshe kitendo cha viongozi wa vyama vya upinzani kutangaza kususia uchaguzi kumepunguza ari ya wapiga kura kwenda kupiga kura. Je, utaita hicho kuwa ni ushindi wa vyama vya upinzani?
 
Takwimu na uhalisia zinakusuta. Isitoshe kitendo cha viongozi wa vyama vya upinzani kutangaza kususia uchaguzi kumepunguza ari ya wapiga kura kwenda kupiga kura. Je, utaita hicho kuwa ni ushindi wa vyama vya upinzani?
Hata sijui umeandika madudu gani ?
 
Kwanza naomba nikueleze kwamba mihuri ni mali ya serikali si mali ya wenyeviti wa vijiji , ndio maana hata mwenyekiti akifa bado mihuri inaendelea kutumika , kuna wakati wenyeviti wa vijiji waliamriwa kukabidhi mihuri kwa watendaji wa vijiji , sijui kama umesahau hili.

Kwahiyo wananchi kutumia mihuri ama kupewa barua ya utambulisho haihusiani na kutomtambua Mwenyekiti aliyepachikwa uongozi , ndio maana hata baada ya wenyeviti kumaliza muda wao mihuri iliendelea kugongwa na barua za utambulisho ziliendelea kutolewa .
Baada ya wenyeviti kupatikana watakuwa na mihuri hiyo hivyo utatakiwa kwenda kwao ili uandikiwe barua na haohao na kugongewa mihuri. lakini ili kutii agizo, itabidi msiende kwao.
 
Ushindi maana yake nini ni kushinda kwa kushindana mwenyewe ama ni kushinda baada ya kushindana na wengi,? Hamna aibu hata Mrema aliyewapa support mumenyanganya Kiraracha yake!! Loh !
 
Back
Top Bottom