CHADEMA na Wanaharakati wajipange na wawe makini na taarifa za kuuzwa kwa hazina ya dhahabu

CHADEMA na Wanaharakati wajipange na wawe makini na taarifa za kuuzwa kwa hazina ya dhahabu

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,620
Reaction score
6,510
Baada ya MO29, Wanaharakati na CHADEMA walisisitiza kwamba lazima haki ipatikane na kuwe na uwajibikaji kutokana na matukio yote yaliyotokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Kampeni zikaanza ikiwemo za kukusanya vielelezo, kupinga tume feki ya Chande na kupeleka vielelezo vya kufungua mashitaka kule ICC.

Jumuiya ya Kimataifa ikaanza kutoa mrejesho. Misaada ikakatwa, viza zikasitishwa, Kanisa nalo likapaza sauti, Jumuiya ya Kimataifa ikitumia lugha ya diplomasia, ikasema inatafakari hatua zaidi za kuchukua.

Ndani ya Tanzania juhudi za serikali zilionekana za zimamoto zisizo na muelekeo unaofanana. Huyu anasema hilo, kesho anasema lile, huyu anafanya hili, yule anafanya lile. Yaani vururuvururu.

Wakati huo huo, wanaharakati wakasisitiza serikali iliyopo sasa siyo halali na kwamba jumuiya ya kimataifa isitoe ushirikiano wowote wa kifedha, kibiashara wala kidiplomasia kwa serikali hiyo haramu.

Natoa maelezo haya yote ili tujue muktadha wa haya yanayotokea sasa, hususani hili suala la kuuza akiba ya dhahabu.

Badala ya CHADEMA na wanaharakati kuingia katika mkumbo wa kujifanya wema na wanajali sana na kuililia hazina hiyo isiuzwe, badala yake ni muhimu kuikumbusha serikali na kuelimisha umma tumefikaje hapa na nini kifanyike ili kujinasua hapa tulipo bila kufanya maamuzi hayo ya kuuza hiyo hazina ya dhahabu ambayo inaenda kuleta hatari kubwa katika thamani ya shilingi, akiba inayowekwa kwa ajili ya hali ya hatari na suala zima la usalama wa nchi kwa ujumla.

Ni muhimu kuikumbusha serikali na kuendelea kuongeza shinikizo la mabadiliko ya msingi ya sheria, katiba na mifumo ya haki na uchaguzi ili baada ya mabadiliko hayo kujenga tena imani ya jumuiya ya kimataifa.

Ni muhimu kuongeza shinikizo la kuachiwa huru na kufutiwa mashitaka yote yanayomkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA.

Badala ya kulialia, ni muhimu kuelimisha umma kuwa serikali imeanza kuuza mali za familia kisa tu ina jeuri, kiburi na kutojali kwa kugoma kusikiliza vilio vya kudai haki na uwajibikaji vya Watanzania.

Watanzania wengi hawana ufahamu mkubwa wa mambo makubwa ya uchumi wa nchi. Ukilialia kwamba dhahabu inauzwa watakushangaa. Watakuuliza mbona bado ipo nyingi mashimoni huko Geita na inaendelea kuchimbwa? Lazima maelezo yako yawe ya kueleweka na uyaweke katika muktadha ambao rai wa kawaida ataguswa ili afanye maamuzi sahihi.

N.B Kwa sasa nchi nyingi zinanunua na kuhifadhi dhahabu na haziuzi. Tanzania tunaenda kinyume na muelekeo wa sasa wa dunia. Hii ni hatari sana.
 
Lazima maelezo yako yawe ya kueleweka na uyaweke katika muktadha ambao rai wa kawaida ataguswa ili afanye maamuzi sahihi.
Maamuzi gani? Wakati hakuna tume huru so hawezi kuondoa uongozi kidemokrasia lakini pia maandamano hata ya amani yamepigwa marufuku!!

Mkiambiwa no reform no election muelewe, haya yote ni matokeo ya kukosekana chaguzi huru maana ingekua ndio kiboko kwa viongozi wanaopishana na maslahi ya wananchi.

Lakini pia Watanzania sio wajinga kama unavyodhani waliosoma pia wameongezeka na wapo mtaani tu hawana ajira. Mitandao ya kijamii pia inasaidia watu kupata taarifa hata kabla mwanasiasa hajachambua!! So wanaelewa sana kuwa awamu hii ni ufisadi kila kona.
 
Maamuzi gani? Wakati hakuna tume huru so hawezi kuondoa uongozi kidemokrasia lakini pia maandamano hata ya amani yamepigwa marufuku!!

Mkiambiwa no reform no election muelewe, haya yote ni matokeo ya kukosekana chaguzi huru maana ingekua ndio kiboko kwa viongozi wanaopishana na maslahi ya wananchi.

Lakini pia Watanzania sio wajinga kama unavyodhani waliosoma pia wameongezeka na wapo mtaani tu hawana ajira. Mitandao ya kijamii pia inasaidia watu kupata taarifa hata kabla mwanasiasa hajachambua!! So wanaelewa sana kuwa awamu hii ni ufisadi kila kona.
Maamuzi ya wananchi kuamua kutoa mashinikizo watakayoona yanafaa.

Maandamano na mashinikizo ya kisiasa ambayo ni "organic" ndiyo yana nguvu zaidi maana hayawapi mamlaka muda na uwezo wa kuyadhibiti.
 
ni muendelezo ule ule wa hatua moja mbele mbili nyuma, Christians wanajenga ikifikia zamu yao wanabomoa kuturudisha tulipokuwa, hazina yote kubwa ya dhahabu ilifanikishwa na conservative Christian leadership kuanzia B.Mkapa wakaingia wao wakabomoa, na kila mahali ni the same pattern, banking hivyo hivyo B.Mkapa alijenga crdb, leo hii wamekuja kuingiza islamic sharia banking crdb wakati ni benki ya wote na siyo islamic ilianzishwa na kujengwa na Christians kwa ajili ya kila mtu hata kwa wasio na dini na ninaweza kukuhakishia hapa crdb itakufa ndani ya mikono yao na kuturudisha tulipotoka, ndani ya miaka 5 crdb kwishney..

hivyo siyo ngumu kuelewa kinachoendelea angalia tu patterns, ni the same game over and over again, tunajenga, wanakuja wanabomoa.

swali ni kwamba ni lipi suluhisho la kudumu? kwa maana pattern inajulikna tayari ...
 
Back
Top Bottom