CHADEMA na UKAWA tukubali ku surrender, hatukujipanga

CHADEMA na UKAWA tukubali ku surrender, hatukujipanga

Dr slaa amekosaje mvuto?
Nachokijua mwanasiasa huwa anakosa mvuto kwa kashifa au kutekeleza ahadi zake je dr slaa unamuweka upande upi??
Ni kweli Slaa mvuto umepungua sana Slaa wa sasa hivi ni wakwenda kufanyia mkutano Kawe kwa Gwajima ili apate watu wa kumsikiliza.
 
Unataka UKAWA wajipangaje? Kama kreti za bia au? Nani kakuambia Slaa amekosa mvuto? Ni lini umefanya utafiti na kupata data za ushindi wa Magufuli?

Tulia wewe acha kuweweseka..
Ukweli unauma ila ndo UKWELI. Dr. Slaa hana mvuto kwa sasa hivi! Subiri utaona, alikuwa na mvuto ila sio sasa!
 
ku surrender ni kosa kubwa ambalo halipaswi kufanywa kabisa. katika siasa za bongo mgombea Urais huwa ana mchango mkubwa sana katika kuongeza kura za wabunge refer uchaguzi wa 2005 JK alichangia sana CCM kupata wabunge wengi na wengine walikuwa hovyo kabisa walioshindwa kurudi awamu ya pili katika uchaguzi wa 2010. Ambapo hata mvuto wa JK ulikuwa umepungua sana sio kama 2005

Watanzania wengi bado wanafanya maamuzi kwa kuzingatia vigezo vichache ni wachache sana wenye kuamua kupiga kura tofauti tofauti wengi mtu akiamua chadema basi ni Chadema kuanzia Rais hadi Diwani bila hata kuzingatia uwezo na sera za wagombea. Ukisema wasisimamishe mgombea Urais inaweza kuwa Karata nzuri sana ambayo CCM wanaweza kuitumia katika kampeni na kwa uelewa huu wa watanzania basi Ukawa usishangae tukachapwa Knock out katika kila nafasi
 
dume zima unasema mwanaume mwenzio hana mvuto, utakuwa mpenda 0713
 
Unazani kujipanga kisiasa kama kupanga mafungu ya nyanya ukawa wanajua wanachokifanya kama unazani kumwandaa mgombea mpaka wewe ujue chadema wanajua nini wanafanya cuf wanajua nini wanafanya nccr wajua nini wanafanya nld pia wanajua nini kinafanyika kuchukua dola sio sawa na kuchukua mke Kwa hiyo ukawa wana mbinu na mikakati yao kuwa mwanachama mtifu kamanda endelea kukinadi chama mabadiliko hayana muda ata Leo unaweza kuyapata ukiyaitaji Mimi na wewe ndio Wa kufanya mabadiliko
 
Hivi uliyeleta mada hii unajielewa kweli. Nyie ndio vigeugeu hebu nipe jinsia yako kwanza.
 
Nilidhani post ingeandamana na tafiti za kuonyesha kushuka kwa mvuto wa Dr. Slaa.. Anyway kila mtu ana mtazamo wake.. Ninasubiri mgombea yeyote ambae atapeperusha bendera ya Ukawa nimpe support yangu..
 
ku surrender ni kosa kubwa ambalo halipaswi kufanywa kabisa. katika siasa za bongo mgombea Urais huwa ana mchango mkubwa sana katika kuongeza kura za wabunge refer uchaguzi wa 2005 JK alichangia sana CCM kupata wabunge wengi na wengine walikuwa hovyo kabisa walioshindwa kurudi awamu ya pili katika uchaguzi wa 2010. Ambapo hata mvuto wa JK ulikuwa umepungua sana sio kama 2005

Watanzania wengi bado wanafanya maamuzi kwa kuzingatia vigezo vichache ni wachache sana wenye kuamua kupiga kura tofauti tofauti wengi mtu akiamua chadema basi ni Chadema kuanzia Rais hadi Diwani bila hata kuzingatia uwezo na sera za wagombea. Ukisema wasisimamishe mgombea Urais inaweza kuwa Karata nzuri sana ambayo CCM wanaweza kuitumia katika kampeni na kwa uelewa huu wa watanzania basi Ukawa usishangae tukachapwa Knock out katika kila nafasi

Kinachowafanya watanzania kuwa masikini na mtaendelea kuwa masikini sio mtu katika nafasi ya uraisi, ni mfumo wa chama cha Mapinduzi ambao unamfanya mtu competent kuwa BOYA. Ni mfumo uliojengwa kimaslahi binafsi zaidi kuliko itikadi. Huyo Magufuli ambaye unamwona anang'ara ametumikia mfumo huu mbovu wa CCM na anajua jinsi ilivyo vigumu kuperform under this corrupt system, more so, yeye mwenyewe ameshiriki kikamilifu kufisadi nchi chini ya mfumo huu wa hovyo kabisa wa CCM
Kama watanzania wangekuwa na uwezo wa kudisect chanzo cha matatizo yao, ambayo ni ya kimfumo wa CCM, huyo Magufuli asingefua dafu.
Count my words, watanzania wakiirudisha tena CCM madarakani wataendelea na wimbi la umasikini kwa miaka yote 10 kwa sababu Magufuli hawezi kuvuka kihunzi cha mfumo wa KIFISADI na maslahi binafsi wa CCM.
 
Hamna jipya mbele ya slaa labda 2 mfocus kwenye ubunge joh urais mxapigwa bao
 
Uzuri wewe mwenyewe umesha admit uwezo wa watanzania wengi hata wasomi umewasikia sasa tunacho ki discuss basi pamoja na kutambua mazingira ya opposition kushinda nafasi ya urais ni ngumu basi tufanyeje atleast tulete uwajibikaji katika huu mfumo angalau hata kwa kupitia uwakilishi. na hawa hawa watanzania ndo kuna wakati hupiga kura kwa kuangalia nafasi ya mgombea Urais its like Ushindi wa Viti vingi vya chadema 2010 Dr.Slaa alichangia watu wabunge wengi kushinda tena wengine hata walikuwa hawakubariki ki vileee sasa tusipoweka mgombea Urais tutegemee nini
 
mnamuwaza Dr.SLAA kila kukicha jiandae kisaikolojia kukabidhi ncho kwa UKAWA. Msifikiri kuletewa mtu dhaifu ili mtambe kwa jeuri huyo ndo kiboko yenu. Magamba tulia mnyolewe taratibu mpaka octoba mtakuwa mko vipara tayari.
 
Unazani kujipanga kisiasa kama kupanga mafungu ya nyanya ukawa wanajua wanachokifanya kama unazani kumwandaa mgombea mpaka wewe ujue chadema wanajua nini wanafanya cuf wanajua nini wanafanya nccr wajua nini wanafanya nld pia wanajua nini kinafanyika kuchukua dola sio sawa na kuchukua mke Kwa hiyo ukawa wana mbinu na mikakati yao kuwa mwanachama mtifu kamanda endelea kukinadi chama mabadiliko hayana muda ata Leo unaweza kuyapata ukiyaitaji Mimi na wewe ndio Wa kufanya mabadiliko

wenzako ccm wanaenda kuchukua dola tena...wewe endelea kujifariji
 
UKAWA pamoja na kuwa wanasimamisha mgombea wa uraisi ila nguvu kubwa wailekeze kwa nafasi za ubunge, ili serikali iweze kufanya kazi zake kwa ufasaha ni lazima tupate bunge lenye nguvu sawa ili liweze kuisimamia serikali vizuri kuondokana na kasumba ya NDIYOOOO.
 
Freeland

Nini Magufuli kwa kikwete tulikuwa na matumaini 100 times haya ya Magufuli tena mpaka viongozi wa dini wakasema ni chaguo la Mungu. Sasa kwa kuwa wewe na wengine ni kama vichwa vya kuku hata mkiona mwenzenu kachinjwa hapo jana bado mtakuja machinjioni tuu even within 2 minutes difference, ndio maana umekuja na mada kama hii. Kama kweli ni mtu mwenye nia nzuri na hii nchi miaka yote aliyokuwa bungeni ulishawahi msikia akichangia hata hoja moja ya ufisadi? Lakini shida si Maguguli kisana zaidi ni system isipokufa hata kama ataenda Slaa ccm ni bure ndio maana waliamua kujitoa mapema kupambana kungoa mfumo. Kwa maono yangu hawa wote ni vibaraka wa mfumo mzima wa ccm unaodidimiza nchi. ndio maana alikuwa anasomewa mara mia mia jana kuhusu kutekeleza mfumo wa ccm na itikadi za chama na si wananchi. by the way alisema mwenyewe pia chama kwanza nchi baadaye
 
Last edited by a moderator:
Matapishi ya juzi haya.....!!!

Yaani mtu kuwa Memba wa Jf inakuwa kila mmoja sasa ni Mchambuzi wa siasa. Kila mmoja anasikia yuko sahihi kwa lolote asemalo..!!

Yaani katika.zama hizi mtu anakuja kujiaminisha na kuaminisha watu humu eti Magufuli atashinda kwa Asilimia 95.....!!! Huu ni ujuha wa hali ya juu sana, ni upinguani wa kiwango cha kwanza, ni Upumbavu wa kiwango cha uchizi kabisa...!!! Ccm wenyewe wanakili kwamba wao kwa idadi ya Wanachama wako milioni sita. Unajua idadi ya wanachama wa Cdm nchi nzima? Wanachama wa Cuf nchi nzima, Wanachama wa Nccr nchi nzima?? Jamani yaani mtu anajisikia raha tu kuja kuropoka hapa..!!

Hivi Magufuli ashinde kwa kiwango hicho kwa kipi alichonacho? Ukae na kutambua watu hii leo wameelimika sana, siyo wale wa miaka 40 iliyopita. Wanajua na kutambua wazi kwamba ktk mfumo wa nchi yetu, hata akapatikana mtu mzuri kiasi gani hawezi kufanya lolote kwasababu anautumikia mfumo uliooza, uliochoka, Uliodumaa..!! Ccm na Serikali yake ni mfumo chovu ktk kulingoza Taifa hili. Hata akapatikana kiongozi mzuri kiasi gani, hawezi kutukwamua Watanzania na Tanzania kama Nchi kutoka hapa Tulipokwama. Watanzania wanajua sasa kwamba ili tusonge mbele kama Taifa tunapaswa kuiweka pembeniccm pamoja na viongozi wake/Serikali yake.

Utambue na kuelewa kwamba hapa tulipo tunahitaji TAASISI IMARA NA SI MTU IMARA ILI KULIONGOZA TAIFA HILI. Na imethibitika wazi kwamba, ccm ni TAASISI CHOVU, IMESHINDWA KUONGOZA IMESHINDWA KUTAWALA no mission no vision..!! Hili hata babu yangu kule kijijini analijua, inakuwaje wewe kijana mdogo ushindwe kuyaelewa yote haya..!! Halafu unajiita mpinzani.. poor mind like this..!!!

Kwataarifa yako mlete huyo Magufuli wako, Wapinzani wako tayari kwa mapambano, liwake jua inyeshe mvua Hivi Magufuli ndiye nani? Huyu mwizi wa nyumba za Serikali, Huyu aliyeiingaza hasara kubwa ya mabilioni ya shilingi, kuanzia Wale Samaki, Meli za Wachina, Kituo cha Filling station pale Mwanza?? Huyo ndiyr unayemtambia wewe...mnxyuuuuuuuuu

Sijawahi kumdharau mtu kiasi hiki. bora ungejiita mccm ningesema unapiga propaganda..!!

BACK TANGANYIKA
 
Kwa wale wanaofikiri CCM is well organized they are wrong. CCM is not organized at all but it's simply in disarray! Look, Ritz can come from nowhere and give advice ti his father concerning party's crucial issues and the will simply consent without giving a thought, the same could apply when mama Ritz come with another idea 'to dislike' something in the party.
CCM has descended from being peasants and workers party to become owned by bourgeois class - mainly people like the 'slaughtered' one of the 'mapacha watatu' whose skins failed to shed.
CCM's time to walk on a tight rope lasted Friday night, and the heights were very high......

R.I.P CCM.
 
Back
Top Bottom