Ni Kweli Chadema na Vyama Vyote vya Upinzani Tanzania Vinaonewa sana Na serikali ya Kidictator ya Magufuli. Na Naona Huruma sana Kwa Kuwa ni Kama Wamebaki wenyewe Bila Watetezi!
Hasira Yangu Juu yao Ni Kuwa Mwenyekiti Mbowe Pamoja na Viongozi wa Chadema wanang'ang'ania Mbinu za Kipumbavu Kupambana na Uonevu wa Kisiasa, Maandamano! Nasema ni Mbinu ya Kipumbavu Kwa Kuwa, Adui wao CCM ameshaijua Hiyo Mbinu yao kwa Miaka zaidi ya 10. Nimeshauri Mbinu zingine Hawajafuata hata Moja, Na hata Wakati wa Kampeni Mikakati yote Niliyoshauri wakapuuza Nikaamua Niingie Kupiga Kampeni Online kwa Kadiri Nilivyoweza Guess who aliizingatia 100% Magufuli, Na najua Aliangalia Hotuba zangu Na Kwa Hilo Nampongeza!
Ushahidi huu hapa, siku Chache za Utawala wake alienda Muhimbili, Na Nilimsikiliza alipovamia Airport Nikajua, alitumia staili yangu ya Argumentation ya Kutetea Hoja Kwa Mifano sii chini ya Minne Back to back.
Msikilize Airport, I know Mh. Magufuli alikunwa na Mimi Mida ya Mwanzoni wa Utawala wake Lakini Sijui sasa! Msikilize Akiongea kama Mimi Pale Airport. Sikiliza Kuanzia Dk 8.17 (Well don't take my word inaweza ikawa ni Mawazo yangu au imetokea tu na akawa hata hajawahi kuona Video yangu)
Ila Na Kwa Mbinu Ya Kusaidia Chadema Nimejitahidi Nimechoka, Sio Kwa Kuwa nawapendelea Nataka equilibrium ya Kisiasa na Uwezekano wa Yeyote Kushinda Uchaguzi, Kwa Manufaa ya Wananchi.
1) Nimeshauri, Chadema Watumie Pesa Kwa Kutoa Tenda za siri Kwa Wanamiziki Kuimba Miziki ya Kudai Haki, Demokrasia na Katiba Mpya wamenisikiliza 0%
Nimeshauri Chadema na Ukawa Watumie Senema, Kuonyesha Umuhimu wa Haki na Demokrasia Wamenisikiliza 0%
2) Nimeshauri Chadema Watengeneze Khanga za Bure Kwa Wafuasi wao, Na hizo fedha za Ruzuku, Kanga zenye Ujumbe Usio na Uchochezi, Mfano, a) TUNATAKA KATIBA MPYA SASA au b) WIZI WA UCHAGUZI NI FEDHEHA, TUME HURU YA UCHAGUZI SASA Maneno haya yanaweza Pia Kuwekwa Kwenye Tshirts na Zikavaliwa na Wafuasi, na Wananchi wanaotaka Mabadiiko, The **** Ruzuku Mnafanyia Nini? au Ombeni basi Michango. Wamenisikiliza 0%
3) nNimeshauri Watoe Tangazo Kwa OCD au RPC atakayejiuzulu kwa Kukataa Kutumiwa Kisiasa Wampe Mtaji kama Bilioni 2 hivi? Watafute Michango, Watumie Fedha za Ruzuku etc. It is Worthy sio Kila OCD anataka Kutumiwa lakini akale wapi? Wamenisikiliza 0%
4) Nimeshauri Watangaze Kama Kuna Mwenye Siri ya Hujuma (Zenye Ushahidi wa sauti na Video) Juu ya Ukawa Chadema azawadiwe Kiasi cha fedha Kitakachoshawishi watu wa Upande Mwingine Kuwaletea Taarifa za Hujuma, Wamenisikiliza 0%
5) Nimeshauri Wafanye Makongamano ya Kimataifa Nje ya Nchi Kuelezea Hali halisi ya Siasa za Tanzania Ili Dunia Iwaelewe wamenisikiliza 0%
Mpaka Nimechoka, Hivi Natetea Amani, Uhuru na Demokrasia ya Watanzania au Natetea Wabunge wa Chadema Kupata Mashangingi na Posho. These Guys are getting in My Nerves Niseme Ukweli.
Wao Wameshikilia tu Maandamano, Maandamano, Ni kweli yana Impact lakini Ni swa Kwa Warombo tunasema Ni Kufungia Kichwa Kwenye Kisangu cha Nyama, Wazo Moja tuuuuu hata hali Ikibadilika! That is Stupid Nikwambieni Kweli CHADEMA! Na Mnajua Mimi Nawapenda Ila Nawapa Live N soon I will stop to advocate for you Guys. Sina Muda Mchafu Kutetea Watu wenye Kuignore Ushauri wa Maana.