Chadema na Ukawa hawakubali Ushauri, Wanaanza Kunitia Hasira!

Chadema na Ukawa hawakubali Ushauri, Wanaanza Kunitia Hasira!

TL. Marandu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
3,625
Reaction score
5,815
Ni Kweli Chadema na Vyama Vyote vya Upinzani Tanzania Vinaonewa sana Na serikali ya Kidictator ya Magufuli. Na Naona Huruma sana Kwa Kuwa ni Kama Wamebaki wenyewe Bila Watetezi!

Hasira Yangu Juu yao Ni Kuwa Mwenyekiti Mbowe Pamoja na Viongozi wa Chadema wanang'ang'ania Mbinu za Kipumbavu Kupambana na Uonevu wa Kisiasa, Maandamano! Nasema ni Mbinu ya Kipumbavu Kwa Kuwa, Adui wao CCM ameshaijua Hiyo Mbinu yao kwa Miaka zaidi ya 10. Nimeshauri Mbinu zingine Hawajafuata hata Moja, Na hata Wakati wa Kampeni Mikakati yote Niliyoshauri wakapuuza Nikaamua Niingie Kupiga Kampeni Online kwa Kadiri Nilivyoweza Guess who aliizingatia 100% Magufuli, Na najua Aliangalia Hotuba zangu Na Kwa Hilo Nampongeza!
Ushahidi huu hapa, siku Chache za Utawala wake alienda Muhimbili, Na Nilimsikiliza alipovamia Airport Nikajua, alitumia staili yangu ya Argumentation ya Kutetea Hoja Kwa Mifano sii chini ya Minne Back to back.

Msikilize Airport, I know Mh. Magufuli alikunwa na Mimi Mida ya Mwanzoni wa Utawala wake Lakini Sijui sasa! Msikilize Akiongea kama Mimi Pale Airport. Sikiliza Kuanzia Dk 8.17 (Well don't take my word inaweza ikawa ni Mawazo yangu au imetokea tu na akawa hata hajawahi kuona Video yangu)

Ila Na Kwa Mbinu Ya Kusaidia Chadema Nimejitahidi Nimechoka, Sio Kwa Kuwa nawapendelea Nataka equilibrium ya Kisiasa na Uwezekano wa Yeyote Kushinda Uchaguzi, Kwa Manufaa ya Wananchi.

1) Nimeshauri, Chadema Watumie Pesa Kwa Kutoa Tenda za siri Kwa Wanamiziki Kuimba Miziki ya Kudai Haki, Demokrasia na Katiba Mpya wamenisikiliza 0%
Nimeshauri Chadema na Ukawa Watumie Senema, Kuonyesha Umuhimu wa Haki na Demokrasia Wamenisikiliza 0%
2) Nimeshauri Chadema Watengeneze Khanga za Bure Kwa Wafuasi wao, Na hizo fedha za Ruzuku, Kanga zenye Ujumbe Usio na Uchochezi, Mfano, a) TUNATAKA KATIBA MPYA SASA au b) WIZI WA UCHAGUZI NI FEDHEHA, TUME HURU YA UCHAGUZI SASA Maneno haya yanaweza Pia Kuwekwa Kwenye Tshirts na Zikavaliwa na Wafuasi, na Wananchi wanaotaka Mabadiiko, The *** Ruzuku Mnafanyia Nini? au Ombeni basi Michango. Wamenisikiliza 0%
3) nNimeshauri Watoe Tangazo Kwa OCD au RPC atakayejiuzulu kwa Kukataa Kutumiwa Kisiasa Wampe Mtaji kama Bilioni 2 hivi? Watafute Michango, Watumie Fedha za Ruzuku etc. It is Worthy sio Kila OCD anataka Kutumiwa lakini akale wapi? Wamenisikiliza 0%
4) Nimeshauri Watangaze Kama Kuna Mwenye Siri ya Hujuma (Zenye Ushahidi wa sauti na Video) Juu ya Ukawa Chadema azawadiwe Kiasi cha fedha Kitakachoshawishi watu wa Upande Mwingine Kuwaletea Taarifa za Hujuma, Wamenisikiliza 0%
5) Nimeshauri Wafanye Makongamano ya Kimataifa Nje ya Nchi Kuelezea Hali halisi ya Siasa za Tanzania Ili Dunia Iwaelewe wamenisikiliza 0%

Mpaka Nimechoka, Hivi Natetea Amani, Uhuru na Demokrasia ya Watanzania au Natetea Wabunge wa Chadema Kupata Mashangingi na Posho. These Guys are getting in My Nerves Niseme Ukweli.
Wao Wameshikilia tu Maandamano, Maandamano, Ni kweli yana Impact lakini Ni swa Kwa Warombo tunasema Ni Kufungia Kichwa Kwenye Kisangu cha Nyama, Wazo Moja tuuuuu hata hali Ikibadilika! That is Stupid Nikwambieni Kweli CHADEMA! Na Mnajua Mimi Nawapenda Ila Nawapa Live N soon I will stop to advocate for you Guys. Sina Muda Mchafu Kutetea Watu wenye Kuignore Ushauri wa Maana.
 
Maandamano hata US yapo na tumeona majuzi kwenye kupinga mauji ya polisi kuua watu weusi huko Marekani.
Ni sawa na Siwapingi ila Wanakiburi au Ni Wagumu sana Wa Kutumia Njia Nyingine. Wakati Nelson Mandela akiwa Jela, Au Uhuru wa Msumbiji, Namibia, Zimbabwe, etc. Kulikuwa na Nyimbo na Miziki (eg Chico, Pat Shanghe, Ivone Chakachaka) za Mchaka Mchaka, Senema eg Sarafina, soweto) Hotuba za Kimataifa (Mwal Nyerere na Wengine) Mavazi, Mabango, Kugomea Bishara za Makaburu etc. Lazima Ukawa Wawe more Advanced! Vinginevyo Tutawachoka, Kutupuuza, We got important things to Do, Na inatia Hasira Kujijengea Maadui Kuishi kwa Wasiwasi Kuwatetea Watu wasiosikiliza. They should not take people for granted, People's Power my ass!
 
Ushauri wako ulioutoa hautekelezeki kwa sababu ni kuhusu kutumia fedha za ruzuku,hautekelezeki kabisa yaani Chadema itoe fedha kuchapisha kanga,itoe fedha kuwapa wanamuziki.
Matumizi ya ruzuku yanaanzia kwa Mbowe na yanaishia kwa Mbowe kidogo akina Tundu na wanasheria wenzake nao wanapata kiduchu kwa ajili ya kufanya kazi za uwakili za Chadema.
 
'Polisi' kama wanaingia maduka ya vifaa vya chama wanachukua, kiwanda cha kutengeneza khanga kikiwekewa ban na wasambazaji kukamatwa, mikanda ya cinema kupigwa ban na waonesha cinema kuswekwa rupango....

Yes, maandamano na mikutano ktk wingi wetu na amani. Dunia ijue Haki zetu kisiasa zimevamiwa na polisi, bunge aliwakilishi wananchi isipokuwa ccm, mahakama zinasikiliza watawala kuhusu kesi za uchaguzi. Ndio, watu wajue tunaumia ndani kwa ndani. Tumevumilia na kuelimisha wenzetu wa ccm lakini mameamua kutumia nguvu za kijeshi ktk masuala ya siasa.

Ushauri wako si mbaya but tulipofikia ni pagumu kwa baadhi ya shauri zako kuwa effective...refer ya zenj
 
I hope Not, Ingekuwa Hivyo, Wasingekuwa Wamoja. Ila wanaweza hata Kutafuta Michango, Niliwashauri hayo Wakati wa Kampeni, Nikawashauri Wamwandikie Hotuba Lowassa Kwa Kuwa Yeye sio Msemaji sana Tangu mwanzo. Tazama Hotuba yake ya Kufunga kampeni ilivyokuwa Nzuri, Lakini it was too late too little! Nilimtuma Mpaka Rafiki yangu Mkubwa, Nikawaandikia Ujumbe wenye Proposals Hata Moja hawakufuata! Labda Mimi Najiwekea Matumaini Makubwa sana juu yangu hivyo Labda Niliwashauri Upuuzi. Sijui, Lakini Nikaamua Kuingia Kupiga Kampeni Mwenyewe Online Kwa Kuwa Niliamini Niliyowashauri!

Mfano. Walipuuza Kujibu Baadhi ya Watu kwa Kina, watu ambao waliaminiwa Kama Mkapa, au Walishindwa Kucapitalize kwenye Makosa ya Magufuli Kuchukukua Nembo yao ya M4C, Nikakaamua Kujitahidi But little impact, Hakuna anijuaye, Ni Jambo Moja tuu walilofanya ambalo Linalingana na Ushauri wangu, lakini nadhani walikuwa wameshalipanga hivyo ilitokea tu Nikafiti kwenye maamuzi yao, Kumpokea Lowassa hili nalo Nililishauri.

1)Ushauri wa Kumpokea Lowassa

Ushauri wa Kujibu Hoja za CCM, kwa Ushawishi na Kwa Kirefu

Ushauri wa Kucapitalize Kwenye Makosa au Kauli za Mh Magufuli, Wakati wa kampeni, (Use you opponent mistakes for your advantage or to reverse his gain, na Bila Matusi)
Hii ilikuwa Ni Kama Unabii Ukiangalia hotuba za Magufuli za sasa za Polisi Walaze Raia, Wanyang'anye Silaha Haraka.

Magufuli Kupora Nembo ya M4C, Imeonyesha Wazi how far Magufuli anavyoweza Kwenda Kunyanganya haki ya Wengine Kisiasa! Aliiba Nembo sasa Amepora Haki ya Kufanya Mikutano. Nilishauri Waaddress issue hizo kwa Mkazo wakapuuza!

'Polisi' kama wanaingia maduka ya vifaa vya chama wanachukua, kiwanda cha kutengeneza khanga kikiwekewa ban na wasambazaji kukamatwa, mikanda ya cinema kupigwa ban na waonesha cinema kuswekwa rupango....

Yes, maandamano na mikutano ktk wingi wetu na amani. Dunia ijue Haki zetu kisiasa zimevamiwa na polisi, bunge aliwakilishi wananchi isipokuwa ccm, mahakama zinasikiliza watawala kuhusu kesi za uchaguzi. Ndio, watu wajue tunaumia ndani kwa ndani. Tumevumilia na kuelimisha wenzetu wa ccm lakini mameamua kutumia nguvu za kijeshi ktk masuala ya siasa.

Ushauri wako si mbaya but tulipofikia ni pagumu kwa baadhi ya shauri zako kuwa effective...refer ya zenj
Hawataweza Kwani Kama Mwanamziki akifanya Concert hawatangazii Polisi ataimba Nyimbo Gani Wanashtukia Tu anaimba, Polisi Watanyang'anya Kamga Zimemazo 1) TUNATAKA TUME HURU YA UCHAGUZI, Watatoa utetezi Gani? au Vijana Wakisema TUNATAKA KATIBA MPYA, Polisi watanyang'anya Tshirt hizo kwa Kisingizio Kipi? Kanisa La Lutheran au Pentekoste Wakiimba Kanisani Jumapili, Wimbo Usemao, HAKI HUINUA TAIFA, SERIKALI ISIONEE, Polisi watafanyaje? Chadema Wakikusanya Michango na Wakatangaza OCD atakayejiuzulu Mbele ya Luninga Kupinga Kuonewa Watamtwanga na Tsh Bilioni 3 Hilo Litazuilikaje? Mbowe akiomba watu US wamkusanyie Na Masenator wachache aongee nao Dunia Ijue Yanayoendelea Tanzania atazuiwa na Nani?
Kwa Hilo Mimi Naomba Nitofautiane na Wewe, Naafiki Maandamano lakini Isiwe Ndiyo Mbinu Kubwa na Pekee!
 
kwa nini usishauri upande wa pili wasivunje katiba?
 
Ni sawa na Siwapingi ila Wanakiburi au Ni Wagumu sana Wa Kutumia Njia Nyingine. Wakati Nelson Mandela akiwa Jela, Au Uhuru wa Msumbiji, Namibia, Zimbabwe, etc. Kulikuwa na Nyimbo na Miziki (eg Chico, Pat Shanghe, Ivone Chakachaka) za Mchaka Mchaka, Senema eg Sarafina, soweto) Hotuba za Kimataifa (Mwal Nyerere na Wengine) Mavazi, Mabango, Kugomea Bishara za Makaburu etc. Lazima Ukawa Wawe more Advanced! Vinginevyo Tutawachoka, Kutupuuza, We got important things to Do, Na inatia Hasira Kujijengea Maadui Kuishi kwa Wasiwasi Kuwatetea Watu wasiosikiliza. They should not take people for granted, People's Power my ass!

Demokrasia ni chaka linalotumiwa na hawa jamaa wenzio wamebanwa kodi na JPM.

Kuweka mashine ya TRA mpka bills unadhania mchezo
 
Hawataweza Kwani Kama Mwanamziki akifanya Concert hawatangazii Polisi ataimba Nyimbo Gani Wanashtukia Tu anaimba, Polisi Watanyang'anya Kamga Zimemazo 1) TUNATAKA TUME HURU YA UCHAGUZI, Watatoa utetezi Gani? au Vijana Wakisema TUNATAKA KATIBA MPYA, Polisi watanyang'anya Tshirt hizo kwa Kisingizio Kipi? Kanisa La Lutheran au Pentekoste Wakiimba Kanisani Jumapili, Wimbo Usemao, HAKI HUINUA TAIFA, SERIKALI ISIONEE, Polisi watafanyaje? Chadema Wakikusanya Michango na Wakatangaza OCD atakayejiuzulu Mbele ya Luninga Kupinga Kuonewa Watamtwanga na Tsh Bilioni 3 Hilo Litazuilikaje? Mbowe akiomba watu US wamkusanyie Na Masenator wachache aongee nao Dunia Ijue Yanayoendelea Tanzania atazuiwa na Nani?
Kwa Hilo Mimi Naomba Nitofautiane na Wewe, Naafiki Maandamano lakini Isiwe Ndiyo Mbinu Kubwa na Pekee!
Unajenga hoja na kuilinda. Take my like na ushauri upande mwingine usivuje katiba kwa makusudi ili upinzani usiingie gharama zote hizo.
 
TL. Marandu
Usiwe hata na wasi wasi,hamna mwana CHADEMA yyt wa kuandamana
CHADEMA itapata aibu Sept 1
Labda ndiyo watakaa chini kujiuliza kwa nn watz sasa wana wapuuza!!
 
kwa nini usishauri upande wa pili wasivunje katiba?
Nimefanya Hivyo Kwa Post Zaidi ya 700, Sasa Siwezi Kushambulia Tu Magufuli na CCM, halafu Niwe Blind Kwa Makosa ya Chadema Mimi sina Unafiki, Hata Baba yangu Marehemu sasa akikosea Nilikuwa Nikimwambia wazi.
 
TL. Marandu
Usiwe hata na wasi wasi,hamna mwana CHADEMA yyt wa kuandamana
CHADEMA itapata aibu Sept 1
Labda ndiyo watakaa chini kujiuliza kwa nn watz sasa wana wapuuza!!
Don't Get Me Wrong, Nadhani Wewe Ni CCM, Nataka waandamane Lakini Isiwe Maandamani Ndio Kila Kitu.
 
Maandamano yalipelekea tume ya uchaguzi Kenya kujiuzulu hivi majuzi. Maandamano ni njia nzuri lilazimisha mabadiliko.
 
Unajenga hoja na kuilinda. Take my like na ushauri upande mwingine usivuje katiba kwa makusudi ili upinzani usiingie gharama zote hizo.
Bro Mh. Magufuli na CCM Nifuatilie Nimewashambulia Kwa Mada Zaidi ya 700, Na Kama Unavyoona hata Kabla ya Kuwa Rais Magufuli Nilimpenda sana (Sio sasa) Lakini Bado Nikawapigia kampeni Chadema Ingawa wanatake Kilakitu for granted! Nilimpenda Magufuli sana, Ila Niliichukia CCM zaidi. Kwa sasa Nimefikia Kumdharau sana Mh. Magufuli Vitendo vyake hasa Teuzi zake za watu Kama Makonda na Yule Wa Arusha yule. Lakini Hilo Halinizuii Kusema Sasa Chadema Dharau zao Zinanitia Kichefuchefu. Nitakuwa Mnafiki Kumshambulia Mh. Magufuli Ninyamazie Upuuzi wa Chadema. Na Usidhani hapa Nawasema Wazi, Nimewachoka, Nilikuwa najitahidi Kuwasiliana nao Private, Nimemtuma haka Kiongozi Mmoja wa Dini Mzito wakati wa Kampeni, hawasikilizagi saa Nyingine! Nikawaandikia Ujumbe Mrefu, Nadhani Ndio Secretary wao hata akauiba na Akapeleka Kule Kwingine maana Niliona yakianza Kusemwa na Kutekelezwa na Ule Upande Mwingine.
 
Back
Top Bottom