Chadema na Ukawa hawakubali Ushauri, Wanaanza Kunitia Hasira!

Chadema na Ukawa hawakubali Ushauri, Wanaanza Kunitia Hasira!

Busara ingine nyepesi ambayo inatumika kupima ustaarabu katika mambo mengi ktk jamii yeyote, ni kujalibu kuvaa kiatu cha upande mwingine, kwa maana ya uhalisia.chukulia kama CDMA wangekuwa wamekabidhiwa dora kikatiba, kwa maana ya kura zao kutosha,ikatokea chama cha upinzani wakaanza kuhamasisha maandamano na kuchochea uvunjifu wa amani, wangekubali??,
Kwa tulipokuwa tumefikia na serikali zilizopita kusingekuwa na tatizo ila kama ingekuwa wamechukua baada ya awamu hii kungekuwa na walakin
 
Kuzuia Kuchakachuliwa Ni pamoja na Kuweka Mgombea ambaye Yupo Tayari Kufa Kutetea Kura Zake, CCM wanapima, Wakiona Mtu wa Namna Hiyo watafikiri Mara Mbili na Sio CCM tu, Hakuna sehemu Afrika ambao wako Tayari Kurudia ya Chief Abiola. Ningegomebea Mimi Ningewajulisha CCM kuwa Wakiniibia Ushindi Nalianzisha, Wakishakujua Mapema Watafikiri Mara Mbili, au wakuue na Wadeal na matoke, NA MIMI NINGEGOMBEA NITAKUWA TAYARI KUFA. Vinginevyo CCM wanakusoma, Woga na Upole wako Kwao Ni Mtaji na bima ya Kufanya watakalo kwako. Mandela was Ready to Die! Kenyatta Was Ready to Die. Na Wanadamu Wakishaona Hivyo wana Mawili, Wakuue na Bado Uwashinde Ukiwa Umekufa, Au Wakuogope na Wakupe haki yako wote Muondoke kwa amani.

Katika yote uliyosema, hapa ndipo penye kufikirisha: kuwa tayari kufa! Ni isiwe wewe peke yako. Ukifa wewe mwenyewe utahesabika kama mkorofi mmoja aliyelazimu serikali (polisi) kumzima ili kulinda amani yetu kwa gharama yeyote. Lakini ukiweza kushawishi umati mkubwa zaidi ya ule wa Tahrir square au kule Tunis ujiunge na wewe katika huo utayari wa kufa huenda kweli ukaitisha serikali/CCM kukuachia kura zako.

Hayo mengine uliyoandika serikali imeshajipanga kikamilifu kuyadhibiti. Utauza wapi ndani ya nchi hii khanga zenye ujumbe wa kudai katiba mpya, tume huru na kukandia wizi wa kura? Kwaya kanisani ziimbe kudai haki? Na nani hao watakaoendesha makongamano nje ya nchi dhidi ya serikali? Wawe wakimbizi au wanaotarajia kwenda huko na kisha kurejea nyumbani? Halafu mtu apewe "motisha" wa bilioni 2 kupigania demokrasia? Na hao maelfu wanaojitoa mhanga bila hata kupewa shilingi wasemeje? Yaelekea wewe ndiye usiyejua mazingira ya kisiasa uliyomo.
 
Mkuu ushauri wako hautekelezeki.
1. Basata na Nape awatoachia hizo nyimbo zipigwe. Mfano mzuri ni nyimbo za Roma
2. Juzi hapa polisi wamevamia duka la vifaa vya CDM,unategemea iko kiwanda au hayo maduka yatapona?
3. Hili haliwezi kutekelezeka,maisha ya hao OCD na RPC yatakua shakani na watapotezwa mapema sana.
4. Nani atakae mlinda uyo mtu? Umeona kwa Ulimboka ni nini alifanyiwa. Usitegemee uyo mtu atapona au atakua salama.
5. Hili la makongamano nakubaliana na wewe kwa 100%
 
Hawataweza Kwani Kama Mwanamziki akifanya Concert hawatangazii Polisi ataimba Nyimbo Gani Wanashtukia Tu anaimba, Polisi Watanyang'anya Kamga Zimemazo 1) TUNATAKA TUME HURU YA UCHAGUZI, Watatoa utetezi Gani? au Vijana Wakisema TUNATAKA KATIBA MPYA, Polisi watanyang'anya Tshirt hizo kwa Kisingizio Kipi? Kanisa La Lutheran au Pentekoste Wakiimba Kanisani Jumapili, Wimbo Usemao, HAKI HUINUA TAIFA, SERIKALI ISIONEE, Polisi watafanyaje? Chadema Wakikusanya Michango na Wakatangaza OCD atakayejiuzulu Mbele ya Luninga Kupinga Kuonewa Watamtwanga na Tsh Bilioni 3 Hilo Litazuilikaje? Mbowe akiomba watu US wamkusanyie Na Masenator wachache aongee nao Dunia Ijue Yanayoendelea Tanzania atazuiwa na Nani?
Kwa Hilo Mimi Naomba Nitofautiane na Wewe, Naafiki Maandamano lakini Isiwe Ndiyo Mbinu Kubwa na Pekee!
Kwa hili jambo ni la UKAWA peke yao ? Wote wenye akili timamu tunataka Demokrasia kwa mapana yake.
Wewe ungefanya kwa mbinu zako labda umuhimu wa UKUTA ungekufa kifo cha Asili Tu.

Play your part bro.
 
Mkuu mbali ya ushauri wako ila juwa wazi hayo mambo ndo njia ya sahihi ya viongozi wa kitaifa kupiga ruzuku ya chama
kwanza viongozi wa kitafa ndio njia yao ya kujipatia kipato ndo mana utaona wana zunguruka kwenye hizi mambo ni walewale kutoka ufipa huku kwetu wanakuja kututimulia vumbi na chopa harafu wanarudi dar
kwa ushauri wako huu sizani kama utakubaliwa mana kutakuwa hakuna ziara za kupiga pesa yan nyimbo? ununue ma OCD unategemea viongozi wa kitaifa watapataje pesa
mwisho utaundiwa zengwe utukanwe mpaka mwisho kuna vijana hawana taki kusikiliza hoja kama zina kinzana na kile walicho kalili
Acha tuone wakati ukuta
 
Hawataweza Kwani Kama Mwanamziki akifanya Concert hawatangazii Polisi ataimba Nyimbo Gani Wanashtukia Tu anaimba, Polisi Watanyang'anya Kamga Zimemazo 1) TUNATAKA TUME HURU YA UCHAGUZI, Watatoa utetezi Gani? au Vijana Wakisema TUNATAKA KATIBA MPYA, Polisi watanyang'anya Tshirt hizo kwa Kisingizio Kipi? Kanisa La Lutheran au Pentekoste Wakiimba Kanisani Jumapili, Wimbo Usemao, HAKI HUINUA TAIFA, SERIKALI ISIONEE, Polisi watafanyaje? Chadema Wakikusanya Michango na Wakatangaza OCD atakayejiuzulu Mbele ya Luninga Kupinga Kuonewa Watamtwanga na Tsh Bilioni 3 Hilo Litazuilikaje?

Mkuu umesema unaishi wapi?

Labda nikwambie tu mkuu...Huku Tanzania mambo sio rahisi kama udhanivyo

Kuwa mpinzani Tanzania ni mateso makubwa sana

Hayo unayoyaona kwako ni mambo rahisi nakuhakikishia ukiyafanya huku utaishia kwenye matatizo makubwa..........

Kwa kifupi hata sasa waliokamatwa hakuna sababu za mashiko kisheria...ni vile tu ubabe unafanyika....na ni kwa sababu tu nchi huru tunaoishi katika mfumo wa kikoloni....

Ikitokea kiwanda kikaanza kuproduce hicho usemamcho nakuhakikishia kitafanyiwa mizengwe na hata kufungwa....hakuna msanii mwenye guts hizo Tanzania.....atafanyiwa mambo ya ajabu maisha yake yote.Hawa jamaa huwa hawahitaji kisingizio kwa ajili ya kunyang'anya ...watakunyang'anya tu...na watakusweka

Mkuu una mawazo mazuri sana....lakini hali halisi kwenye ground ni ngumu....ukitaka jaribu kuja mara moja uandamane na viongozi wa chadema katika kazi zao uone ugumu wake

Yaani ni kujitoa sadaka na kuonekana huna haki yoyote kwa nji yako
 
Busara ingine nyepesi ambayo inatumika kupima ustaarabu katika mambo mengi ktk jamii yeyote, ni kujalibu kuvaa kiatu cha upande mwingine, kwa maana ya uhalisia.chukulia kama CDMA wangekuwa wamekabidhiwa dora kikatiba, kwa maana ya kura zao kutosha,ikatokea chama cha upinzani wakaanza kuhamasisha maandamano na kuchochea uvunjifu wa amani, wangekubali??,
Unasema Uwongo au Nisikuhukumu, Unasema Jambo ambalo halipo halafu unataka Nikujibu Nikibase kwenye jambo Hilo. Ni Kwa Jinsi Gani Maandamano au Mikutano Inavunja amani? Mimi Naona Wanaovunja amani Ni Wanaowazuia Watu Kufanya Mikutano, Mahafali, Kumzika Mawazo, Na Kukamata Wabunge ovyo kwa Kuwaita wachochezi, Huko ndiko Kuvuruga amani. Anayevuruga amani ni Nani? Anayejitetea akionewa au Anayeonea? Rekebisha Usemi wako kwanza Ndio Upate Jibu. Mimi Naona Kama Chagema Wakiwaambia Wananchi Wavunje Watu Utu wa Mgongo Kama anavyosema huyu wa CCM, Huko ndiko Kuvunja amani. Na Ni Nani aliwaambia Viongozi Tanzania Kuwa Mtu akifanya Civil Disobedience au Kuandamana basi Ni Sheria Kumpiga? Kutamka tu Polisi avunje Mtu Uti wa Mgongo Ni Uhalifu, Nimelishangaa sana hili Limalaya (Nisameheni hasira yangu)

Huyu anadhani Magufuli Ni Mfalme! Kama Unatafuta Watu wanaovuruga amani Ndio hawa.
 
Haya mawazo yako nayaona yote ni ya msingi sana, kwakua mawazo haya hasa ya kuandika hizo nguo ni kuweza kuwaivisha watu kisaikolojia, na hili la mwisho kwakua CCM wako tayari kuua nalo nalipongeaza sana, kufanya maandamano nchi ambazo zina demokrasia.

Chadema wanataka ukuta lakini ukiwaangalia wananchi hawana hamasa sijui ukuta huu utajengwaje? haya yanakua ni mambo ambayo yanahitaji matayarisho.
 
TL. Marandu,
Usihofu wala kupanda hasira juu ya ''maandamano ya UKUTA'' maana wanaokandamizwa wakikosa nafasi ya kujieleza katika majukwaa huru kama Bunge au kuzuiwa kufanya mikutano ya kisiasa au vyombo vya habari kubanwa basi ''maandamano'' ni njia mojawapo ya kufikisha ujumbe kwa ''watawala gandamizi'

Hili vuguvugu la ''maandamano ya UKUTA'' yamewafanya watawala kukosa usingizi kadiri siku zinavyokaribia Sept 1. Kukosa usingizi kwa ''watawala'' kunaweza kupelekea mabadiliko kabla ya Sept 1 , 2016 ukasikia tamko la serikali kulainika na kufungua majadiliano ya muufaka ya namna gani serikali ya utawala wa awamu ya tano kupunguza ''mgandamizo'' kwa vyama vya siasa vya upinzani ktk majukwaa ya Bunge, huru wa kufanya mikutano ya kisiasa na pia uhuru wa vyombo vya habari.

Madhumuni au lengo kuu la ''vuguvugu'' za maandamano duniani kokote hutokana na sababu zifuatazo inaweza kuwa zote au baadhi tu:
  1. Hali ngumu ya kiuchumi
  2. Kudai huuma za kijamii kama elimu, afya, ardhi
  3. Uhuru wa kusikilizwa na ''watawala''
  4. kuikumbusha serikali iliyopo madarakani kuwa mwelekeo wake unabidi ubadilike
  5. Demokrasia kama ilivyo katika katiba ya nchi
  6. uhuru wa kujumuika kisiasa
Tukitazama sababu za Serikali ya awamu ya tano kukataza maandamano kwa vile huu ni wakati wa '' Hapa Kazi Tu'' na uchaguzi umekwisha.

Ukiangali sababu hizo sita za ''vuguvugu la maandamano' hapo juu utaona ''Hapa Kazi Tu'' utaona haina majibu ya kiuchumi kuhusu 1. Hali ngumu ya kiuchumi mitaani' 2. Huduma za Kijamii Afya, Elimu hazipo sawa pamoja na kuchonga madawati au kuvamia mahospitali. 3. Uhuru wa kuzungumzia / kushauri matatizo hayo matatu haupo. Pia Demokrasia imeganamizwa ndani ya Bunge na nje ya Bunge.

Nini kifanyike na serikali kupunguza ''pressure'' ya kufanyika maandamano hapo Sept 1.: Ni serikali kuwa ''sikivu'' na kutoa tamko ''ruksa'' mikutano ya kisiasa nchi kote na kuwaelezea wananchi kuwa ni ruhusa sasa wanasiasa/wananchi kufanya mikutano na shughuli kisiasa bila kuwekewa vizuizi vya kufika maeneo fulani ya nchi kwa sababu katiba ya nchi inatamka hivyo.

Pia maneno kama dikteta uchwara n.k yanayo akisi hali ilivyo sasa yatapotea kama serikali itakuwa ''sikivu'' kubadili msimamo ''mkali'' wa kugandamiza uhuru wa kujumuika kisiasa au kusikilizwa kupitia majukwaa mbalimbali ''huru'' kama Bunge, mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Pia Bungeni chama chenye wabunge wengi wasiwe na hofu kusikiliza michango ya wapinzani kwa kuwawekea mizengwe isiyo na maana au kuzuia Bunge kuonekana ''Live'' kwani mwisho wa siku kura zao nyingi zitaamua mustakabali wa miswada gani ipite kwa kura nyingi na ipi ipingwe kwa kura nyingi.
 
Katika yote uliyosema, hapa ndipo penye kufikirisha: kuwa tayari kufa! Ni isiwe wewe peke yako. Ukifa wewe mwenyewe utahesabika kama mkorofi mmoja aliyelazimu serikali (polisi) kumzima ili kulinda amani yetu kwa gharama yeyote. Lakini ukiweza kushawishi umati mkubwa zaidi ya ule wa Tahrir square au kule Tunis ujiunge na wewe katika huo utayari wa kufa huenda kweli ukaitisha serikali/CCM kukuachia kura zako.

Hayo mengine uliyoandika serikali imeshajipanga kikamilifu kuyadhibiti. Utauza wapi ndani ya nchi hii khanga zenye ujumbe wa kudai katiba mpya, tume huru na kukandia wizi wa kura? Kwaya kanisani ziimbe kudai haki? Na nani hao watakaoendesha makongamano nje ya nchi dhidi ya serikali? Wawe wakimbizi au wanaotarajia kwenda huko na kisha kurejea nyumbani? Halafu mtu apewe "motisha" wa bilioni 2 kupigania demokrasia? Na hao maelfu wanaojitoa mhanga bila hata kupewa shilingi wasemeje? Yaelekea wewe ndiye usiyejua mazingira ya kisiasa uliyomo.
huuzi Unazitoa Bure kwa wafuasi wanamama, na unahikisha design nzuri, ujumbe simple na hakuna matusi au kejeli. Wakikamata Watu wanashidwa kesi, Ujumbe "TUNATAKA TUME HURU YA UCHAGUZI" Ukisema Ni Matusi au Uchochezi, Ukamkamata Mtu, Utaonekana Kweli Kituko na Taahira!
 
Ushauri wa kiccm uko hivyo kutumia kanga kurubuni watu kwa hongo , chakula, kutumia wasanii kwa manufaa ya chama, Kumbuka kipindi cha kampeni ni hatari kuliko unavyofikiri ,ushauri huo watumie chama tawala ukawa inatumia hoja mjarabu kushawishi umma wewe unataka kuwatega ukawa kwa kisingizio cha ushauri tena huku povu linakutoka kwa ushauri tuu!! Unalako jambo si bure.

Mwisho ushauri ni ushauri sio sheria wala amri , CDM NA UKAWA wana haki ya kuufuata ushauri wako ama kukataa huna haja ya kutoka jasho kisa ushauri wako haujafanyiwa kazi.
 
huuzi Unazitoa Bure kwa wafuasi wanamama, na unahikisha design nzuri, ujumbe simple na hakuna matusi au kejeli. Wakikamata Watu wanashidwa kesi, Ujumbe "TUNATAKA TUME HURU YA UCHAGUZI" Ukisema Ni Matusi au Uchochezi, Ukamkamata Mtu, Utaonekana Kweli Kituko na Taahira!

Mpaka hapa mkuu hapana shaka nimeshakuelewa vizuri. Nakutakia kila la heri katika mikakati hiyo. Lakini nina hakika CHADEMA hawawezi kukuelewa wala kukubaliana nawe. Hivyo, badala ya kukasirika, ama anzisha chama chako au jaribu kushawishi chama kingine kichukue na kutekeleza mikakati hiyo.
 
Ni Mahakama tu inaweza thibitisha mtu ni fisadi
Kama ambavyo Lowassa sio fisadi kwa nn Muhongo awe fisadi?
Mahakama gani ilimtia hatiani Mama Tibaijuka
Lkn kwenye ethics huoni kama tulikosea kumleta Lowassa CHADEMA wakati for years akina Lissu walikuwa wanamtuhumu kwa udokozi wa mali za UMMA?
Dr Slaa ndiyo kiongozi wangu mm sio hawa ambao wenyewe akina Lema wlaituambia hafai
Hapo ndipo wengi tunaingia kwenye mtego mkuu siasa sio mtu ukisema slaa ndio kiongozi wako wakati hayupo kwenye siasa unapoteza muda wako bure kwenye siasa.

Siasa ni sera itikadi na katiba za sheria zake kama CDM bado inaendelea kutetea wananchi inaendelea kupambana na ufisadi ina sera nzuri kwa raia hiyo ndio siasa yangu hata aongoze nani tutaenda naye kwa kwa itikadi hiyo kinyume chake siangalii watu.

Mfano ukimtoa magufuli nje ya ccm na sera zake ni kiongozi mzuri ukimchanganya na (ccm ina wenyewe ) ndio unasikia kinachotokea coz hawezi kutenda nje ya sera na itikadi za kiccm baasi.
 
Mkuu siasa ngumu sana, zione tu hivi hivi, ushauri unaoutoa ni wa maana, mimi mwenyewe naona kitendo cha Mbowe kutoka bungeni, ku tangaza maandamano huku akijua huu ni uongozi brutal naona alikuwa impulsive, anaenda kupambana jicho kwa jicho wakati mwenzake ana silaha za moto yeye hana, na hata hivyo timing ilikuwa mbaya sasa hivi bado watanzania wamejawa na mihemko na wana msapoti magufuli, maana matumaini bado yapo kwa kuwa ni mpya, sasa ukitaka kumpinga Magufu kwa kutumia mass asingeanza sasa hivi angetulia walau miaka 2 au 3 ipite ambapo wananchi wengi watakuwa wameshaona ubovu wa Magufuli

Na kuhusu kwenye kampeni mimi nilishangazwa sana hotuba za Lowassa kwa kweli, nikilinganisha watu waliouwa naye kama Mbatia, mbowe, lema, sugu ambao wanajua stratergy nilishangaa wanamruhusu mgombea wao kutoa hotuba ambazo hazikuwa na stratergy yoyote ya maana zaidi ya longo longo na ndoto za alinacha za kuwaambia watu ataondoa foleni ndani ya siku 100 dar!!! Ukawa waliniangusha sana kwenye kampeni, walikuwa kama wao ndio CCM n
 
Wana muziki hawawezi kuimba nyimbo za upinzani kirahisi mkuu, hata kama wanasapoti upinzani... maana kwa afrika ukisapoti upinzani unakutana na figisu nyingi sana, na ukisapoti serikali unapata feva nyingi na fedha nyingi pia
 
Mkuu umesema unaishi wapi?

Labda nikwambie tu mkuu...Huku Tanzania mambo sio rahisi kama udhanivyo

Kuwa mpinzani Tanzania ni mateso makubwa sana

Hayo unayoyaona kwako ni mambo rahisi nakuhakikishia ukiyafanya huku utaishia kwenye matatizo makubwa..........

Kwa kifupi hata sasa waliokamatwa hakuna sababu za mashiko kisheria...ni vile tu ubabe unafanyika....na ni kwa sababu tu nchi huru tunaoishi katika mfumo wa kikoloni....

Ikitokea kiwanda kikaanza kuproduce hicho usemamcho nakuhakikishia kitafanyiwa mizengwe na hata kufungwa....hakuna msanii mwenye guts hizo Tanzania.....atafanyiwa mambo ya ajabu maisha yake yote.Hawa jamaa huwa hawahitaji kisingizio kwa ajili ya kunyang'anya ...watakunyang'anya tu...na watakusweka

Mkuu una mawazo mazuri sana....lakini hali halisi kwenye ground ni ngumu....ukitaka jaribu kuja mara moja uandamane na viongozi wa chadema katika kazi zao uone ugumu wake

Yaani ni kujitoa sadaka na kuonekana huna haki yoyote kwa nji yako
Nakubali Ni Ngumu Kazi zao, Nakubali Ni Mateso, Lakini Tunashauri Tukiwatakia Unafuu na Mafanikio Makubwa zaidi. Wanapoziba Masikio Tunaona ni dharau na hata huruma zetu zinaisha. Unadhani Ni Rahisi Mtu Mwenye Maisha yako Kupingana wa Watu waonezi Kila siku kwa Nguvu zote? Nimejitahidi Niwezavyo Na hata Sina Hata Kadi ya Chama Chochote. Angalau wasikilize Ushauri wa Kuwasaidi wao na Taifa, sio Kutoka Kwangu tuu maana Naweza Kuwa Naongea Utumbo, Na Kwa wengine Pia.
 
Wana muziki hawawezi kuimba nyimbo za upinzani kirahisi mkuu, hata kama wanasapoti upinzani... maana kwa afrika ukisapoti upinzani unakutana na figisu nyingi sana, na ukisapoti serikali unapata feva nyingi na fedha nyingi pia
Wawajenge Vijana Wao Wenye Vipaji vya Miziki, na Senema, Watumie Watu Kuanzisha Redio na Television, Na sio Unaenda Na Kuonyesha Wazi Kuwa Hii Redio ni ya Chadema, au Huyu Mwnamziki Ni chadema etc. Mimi Naamini Pesa hazijawahi Kushindwa Kitu. Mengine siwezi Kusema, Ila Kwa Kutumia Fedha Unaweza hata Kulipa OCDs RPCs etc Wakufanyie wewe Kazi. Counter Hujuma, Maana dawa ya Moto Ni Moto! Namlamba OCD Milioni 300 Naenda Kyela Arusha napiga Mkutano FFU wanakuja Kuzuia Mkutano Lisaa 1 na Nusu Baada ya Mkutano Kwisha Kisa? Walipotea Njia! Tunamwahidi, Akitishiwa Ajiuzulu Mbele ya TV, Tunamtwanga Mtaji wa Bilioni 3 CCM Kutakalika? Dawa ya Hujuma Ni Kumhujumu anayekuhujumu, Wakati wa Vita Baridi, Nchi za Ukomunisti Mawaziri Wengi Walikuwa Katika Pay Roll ya CIA, Kuna Ubaya Gani Ma OCD na Ma RPC Mkatumia Fedha za Ruzuku na hata Michango Mkawaweka kama 10 hivi kwenye Pay-Roll Nono Luliko wanayolipw.a na Serikali? Nakwambia Ningekuwa Katibu Mkuu Chadema CCM hata Panadol isingemaliza Maumivu Ningewapa.
 
Marandu pole sana
hivi unajua alietunga wimbo wa CHADEMA yuko kwenye medianow analia kutelekezwa?
hivi unajua mawakala wa CHADEMA wengi uchaguzi uliopita walishinda njaa vituoni?
na wengi hawakulipwa chochote hadi leo?
na wengi hata simu za wagombea tu hawana?

Imagine mtu kamlindia kura Halima Mdee hadi kashinda
halafu mtu huyo hakulipwa hata kkurudishiwa tu hela yake aliyoitumia kula na nauli
halafu huyo mtu hata Halima Mdee kumuita tu na kumwambia ahsante ya mdomo wapi...

CHADEMA wana safari ndefu mno kwenye organization...
 
Back
Top Bottom