Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,101
- 136,749
- Thread starter
- #61
Mi navyoona mambo yanavyokwenda, hakuna wa kuitoa CCM madarakani... labda CCM ipasuke vipande viwili.
Wamemiliki kila kitu kinachoweza kuwapa ushindi wa haki au wa wizi.
Kwa mfumo huu, CDM na ndugu zao wote, watasubiri sana kuwatoa hawa wezi madarakani.
Lakini unajua nini Komredi...?
Vipi kuhusu kitu kama ile 'Arab spring'?
Mbona ilimng'oa yule Hosni Mubarak wa Misri na yule Ben Ali wa Tunisia...
Tatizo ninaloliona kuhusu hapa kwetu ni uoga.
Tulio wengi hatupo tayari kupoteza damu zetu, maisha yetu, au hata kutandikwa mijeredi na kupigwa virungu vya polisi katika kudai haki zetu.
Mimi naamini kabisa kuwa mwisho wa siku sisi wananchi tuna nguvu kuliko polisi, jeshi, Magufuli, na CCM.
Tukiamua kuwatoa watatoka tu ingawa pia watu watalipa gharama kubwa sana.
Hebu ona kwa mfano kule Zimbabwe...yaani kile kibabu kinawapeleka puta hadi watu wanaishia kukamata panya ili wamfanye kitoweo lakini cha kushangaza eti bado kipo madarakani!
Hivi kweli unadhani Wazimbabwe wakiamua na kusema sasa basi imetosha...kile kibabu unadhani kitaendelea kuwepo madarakani?
Tatizo letu sisi Waafrika wa huku kusini mwa Sahara wengi wetu tuko waoga sana.
Waarabu huwezi ukawafanyia huo ujinga ujinga aisee....watajilipua wenyewe na kukulipua wewe.
Unakumbuka jinsi UKUTA ulivyochimbiwa biti na hatimaye ukaishia kuporomoka wenyewe?
Kwa kweli saa ingine hata sisi wananchi ni wa kulaumiwa kwa kuwaendekeza hawa viongozi.
Sisi wananchi tupo wengi mno kushinda hayo majeshi yao, tupo wengi kushinda usalama wa taifa, tupo wengi kushinda CCM.....lakini tunavyopelekeshwa sasa....
Hata sisi kwa kiasi chetu tunastahili lawama....