CHADEMA na ubunge 2020

""Tulimpokea Lowasa si kwa sababu siyo fisadi bali tunaamnini ataipasua CCM vipande vipande na kutufikisha sehemu ambapo sisi hatuna wagombea""Adui yetu ni CCM siyo ufisadi """

Hizo eti ni sababu zilizowafanya wampokee Mh Lowasa na kumpa heshima ya kugombea urais!!

Sasa sijui Lowasa kawasaidia kweli kuipasua CCM?

Siasa za kilaghai hizi zinairusha nyuma Africa yetu!!

Chadema wanamini MTU siyo chama Chao!!

Sasa wajiandae kwa kipigo kama cha mbwa aliyeiba kipande cha nyama
 
Mkuu Nyani..Unaanza vipi wakati Siasa zimezuiwa mpaka 2020?
Sheria zipi unaweza kubadili Wakati kuna watu wako juu ya Sheria?
 
Ni wazi kuwa mkakati wa CCM umewashika pabaya upinzani kwa ujumla.Mkakati huu si mdogo na ulianzia katika uteuzi wa naibu spika,ukatiwa nguvu na kupiga marufuku live coverage na pia mikutano ya kisiasa.Mabunge ya bajeti yaliyopita ilikuwa upinzani wakikwazika weekend inayofuata wanafanya mkutano wa hadhara Iringa kwa Msigwa,HILI HALIPO KWA SASA.
Jambo jingine ni hofu iliyowaingia watendaji wa serikali ambao wako tayari kufanya lolote ili kuiridhisha mamlaka ya juu na kwa mantiki hiyo kitu kama maandamano ya kupinga jambo lolote hata la haki hayawezi kufanyika.
Jambo la tatu ni pre conceived mentality ya kuonewa hasa ndani ya bunge na inawafanya wawe rahisi kutolewa kwenye reli (jana ya Mnyika).
Kwa wale tunaopenda upinzani imara ni wajibu wetu kuasaidia hata ushauri tu,
  • Ndani ya bunge wajipange kwa hoja zenye mashiko na waache kutumia personal scenario katika mijadala (Bashe versus Lema).
  • Ndani ya bunge wajipange kimkakati-nani aseme nini wakati gani,hoja gani tumpe huyu na tusimpe yule (strenghs na weakness zao wazijue)
  • Wajifunze uvumilivu (Mnyika angetulia jana si ajabu Lusinde angetukana zaidi lakini ubishi ukavuruga).
Bila upinzani imara tutakuwa kila wakati tunarejea mambo yaleyale.
 
Kama hao wananchi hawakufunga macho 2015 jipeni moyo tu kuwa ati watafunga macho 2020! shauri lenu.
Mkuu Cdm Ni Wazembe Sna Hawana Mkakati Kabisa Wa Ushndi,mm Karibia Uchaguzi Zote Nimeshawahi Kuwa Wakala Wa Cdm Kusimamia Kura,cha Kushangaza Posho Za Mawakala Hakuna Wakala Unakaa Na Njaa Siku Nzima,matokeo Yake Mawakala Wanaacha Vituo Wanabaki Wa Ccm Peke Yao,embu Fikiri Umepewa Mda Mkubwa Miaka 5 Hata Alfu 5 Ya Wakala Shda Kweli Hata Hyo Tume Huru Ukiwanayo Utashnda Kweli?Kuna Tatizo Kubwa Ndani Ya Cdm
 

Halafu ukiangalia ni mambo yale yale wakati mwingine hadi yanaudhi. Hivi ni nani asiyemjua Lusine na uropokaji wake? Sasa kwanini kuingia kwenye mtegoa mbao mnajua mtanaswa nao? Yaani, mtu akitaka kuwatibua tu wapinzani alete masuala ya muongozo na mabishano na "kiti". Mara karibu zote ambapo wapinzani wametoka Bungeni ni kwa sababu ya mabishano ambayo hayakuwa ya lazima. Lengo ni kutaka kushinda mashindano ya nani gangwe na mbabe Zaidi.
 
Chadema wangeanza kupambana Sasa hivi wakianzia na tume huru ya uchaguzi
 
Mikakati waliyoingia nayo Chadema kwenye uchaguzi wa 2015 ilikuwa bora sana, japo walijichanganya mwishoni kwa kubadili gia angani.

Kwa uchaguzi wa 2015 wangewekeza kwa wabunge nguvu kubwa naamini wangebeba majimbo mengi sana .

Wabunge wengi wa Chadema walijihangaikia kupata ubunge, isipokuwa kwa yale majimbo pendwa ndio walipewa bajeti na chama.

Ila uchaguzi wa 2020 sidhani kama watafikia hata nusu ya mikakati ya 2015.
 
Silent Killer Wa Chadema Ni Mashinji, Hakuna Msemaji Wa Maana Wa Chadema Kwa Sasa! Amebaki Lissu Peke Yake, Anajitahidi Kupangua Makonde Ya Ccm
Lissu mwenyewe anatafuta umaarufu binafsi.
 
JokaKuu; if you wanna bet nitakuambia kwa mwendo huu kama unafikiria CCM wanatawala Bunge 2020 Bunge litakuwa ni la chama kimoja kabisa. Na wala hatolaumiwa Magufuli; atasingiziwa tu.
Muwe makini na kauli zenu tusije tukakimbiana hapa 2020/siyo mbali.
 
dalili ya kukosa matumaini, na kukata tamaa kwa cdm
Hatutishiki maana hizi dalili zinaletwa na vijana wa Lumumba. Adui yako muombee njaa.
Chadema inachana mawimbi tusikimbiane tu hapa hiyo 2020
 
Chungeni kauli zenu tukakimbiana hapa 2020 .mungu atupe uzima
 

..kwa maoni yako unadhani ni fikra/jambo gani ambalo CDM wanatakiwa kupambana nalo sasa hivi?

..my observation ni kwamba Mzee haamini ktk demokrasia ya vyama vingi. Haamini ktk uhuru wa mawazo. Hapendi uhuru wa wananchi kukusanyika freely au kuji express kwa njia ya maandamano.

..YES, kuna tishio kwa cdm. Lakini nadhani hicho nilichokieleza ni tishio kubwa zaidi kwa wananchi.
 

Kusema ukweli ni kwa upinzani kuongeza wabunge na madiwani na kuwa na uwiano unaokubalika bungeni na kwenye mabaraza ya madiwani pekee kutakakohakikisha kuwepo kwa checks and balances na hivyo kuleta uwajibikaji serikalini.

Kwenye mfumo wa vyama vingi ushabiki wa kivyama hauzi kukosekana. Tumeona maamuzi mengi yakifanyika kishabiki bila kuweka mbele maslahi ya taifa kutokana na bunge kutawaliwa na wabunge wa chama kimoja.

Lakini haitoshi tu kwa upinzani kuandaa wagombea makini katika kila jimbo. Ni lazima waje na ajenda na dira mbadala. Ni lazima waje na ujumbe wa kisera unaofafanua watafanya nini pale CCM waliposhindwa na kuusambaza kwa wananchi. Na hii kazi inapaswa iwe imeshaanza kwa maandalizi ya 2020.

Wakifanya haya hakika wataongeza idadi kubwa ya viti vya bunge na katika mabaraza ya madiwani. Nina wasiwasi kama uongozi wa Cdm unaliona hili!
 
Kuwa kweli na nafsi yako, unaona dalili au mkakati wowote wa CDM kuongeza majimbo 2020 ?
Ni wazi 2020 CDM wanaenda kupoteza majimbo mengi, na Dsm ndio watakaongoza kwa kupokonywa majimbo, visingizio vitakuwa lukuki ila ukweli ushajulikana.

..mikutano ya wazi ya vyama vya upinzani imepigwa " karantini ."

..hilo ni pigo kubwa kwa vyama vya upinzani hususan CDM.

..lingine ni hujuma za waziwazi zinazofanywa na wakuu wa mikoa na wilaya dhidi ya wabunge wa cdm.

..tunatakiwa tuilaimu serikali kwa kusigina demokrasia na uhuru wa kutoa mawazo.
 

..kwanini chama kijenge ofisi za kifahari wakati wananchi hawana maji, zahanati, na mahitaji mengine muhimu?

..ila nakubaliana na wewe kuhusu chama kuongeza nguvu ktk kuandikisha wanachama.

..vilevile kuwa na viongozi competent na dedicated ktk ngazi zote kuanzia taifa, kanda, mikoa, wilaya, mpaka vitongojini.
 

Hilo la kusema sijui mikutano ya wazi ya vyama vya upinzani imepigwa marufuku or whatever ni lame excuse tu.

They need to be creative.

They can use subterfuge to get around it.

Nadhani utakuwa ushausikia huu wimbo wa 'We Miss You Manelo'.

Ukisikiliza kwa makini utajua kuwa walikuwa wanasema 'we miss you Mandela'.

Lakini kwa vile serikali ya Kikaburu ilikuwa imepiga marufuku hayo mambo ya kumtukuza Mandela jamaa ikabidi waje na 'we miss you Manelo'.

Upinzani wa Tanazania nao inabidi wawe creative aisee. La sivyo watakuwa ni wapinzani daima na hawatokuja kushika madaraka...iwe bungeni au ikulu.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…