CHADEMA na TBC kunani?

CHADEMA na TBC kunani?

TBC inaheshimika sana duniani, haipo tayari kumualika mtu kama Mh. Lema ambaye anaonekana wazi kabisa kwamba uwezo wake wa kufikiri ni mdogo na malezi yake ya utotoni hayakuwa mazuri.

  1. Lema hana akili lakini aliwahi kuitwa na kubembelezwa na Kikwete agombee kwa tiketi ya ccm pale Arusha
  2. Lema hana akili lakini huyu ndiye ambaye imebidi magamba watumie muda na pesa nyingi sana kwenda kumfungulia kesi ili asifanye kazi za chama chake na waliomtuma.
  3. Arusha ni mji wa kitalii, sorry, pia ni miongoni mwa miji ambayo tunayaita majiji kwa hapa kwetu, hawa watu unaodhani hawana akili ndio walimchagua bwana Lema kua Mbunge wao.
  4. TBC haina hadhi ya kuitwa hata TV ya Taifa, sembushe kua ya kimataifa? Niambie ni kitu gani cha kitaifa hua inaonesha zaidi ya Bunge ambalo sheria inawabana? Meli ile ya Zanzibar ilipozama, TBC waliendelea kuonesha miziki ya Kikongo n.k, TV ya taifa yaani ITV ndio iliotupa update za kile kinachoendelea, ile inaitwa TV ya ccm na sio ya taifa, acha kudhihaki watu.
 
Haina athari kwa kuwa wananchi wengi wanaoiunga mkono CHADEMA ni hohe hahe (wasio na hela ya king'amuzi) na baadhi ya watu ambao hawana hata umeme....wanategemea zaidi magazeti...
Wanaoangalia TBC wengi ni wale wazee wa dar es salaam.
Mkuu sio kweli.Nakutolea mfano mdogo tu hapa Lindi tupo analojia bado na wakazi wengi wanatumia antena ndogo maarufu kama chadema na wanakamata TBC tu.TBC ni mali ya watanzania wote na Chadema ni chama cha wananchi.Tuna kila sababu ya kulisemea hili.
 
Chadema wana vita na Ccm,
Tbc ni Ccm
vita ya Ccm ni ya Tbc pia, wewe hujui hilo? Watakucheka watu!

Tunahitaji kuwa na uelewa wa ziada na kujiongeza zaidi! CCM wana bifu na CHADEM lakini TBC ni mali yetu watanzania wote na tusipolionesha hilo kwa sauti moja, basi watakuja kujimilikisha kama walivyojimilikisha viwanja vyote vya michezo wakati tulibeba zege sote na wengine kukamatiwa kuku wetu kwa nguvu. Ipo siku hata mawe yatatoa ushahidi.
 
Kwani mnaenda wapi...?
Kwani wewe sio mtanzania?Muelekeo wetu kama nchi tunataka kuona mageuzi makubwa katika nyanja za kiuchumi,kijamii na kisiasa hususani maeneo ya kilimo,madini, utawala bora,uhuru wa vyombo vya habari,ukuaji wa demokrasia na nk na hatimaye kufikia malengo ya millenia.
 
Tunahitaji kuwa na uelewa wa ziada na kujiongeza zaidi! CCM wana bifu na CHADEM lakini TBC ni mali yetu watanzania wote na tusipolionesha hilo kwa sauti moja, basi watakuja kujimilikisha kama walivyojimilikisha viwanja vyote vya michezo wakati tulibeba zege sote na wengine kukamatiwa kuku wetu kwa nguvu. Ipo siku hata mawe yatatoa ushahidi.
Mkuu umenena vema.
 
Nasikitishwa sana kuona wabunge wa CHADEMA hawashiriki katika mijadala inayoendeshwa na television ya taifa (TBC) hususani vile vipindi vya asubuhi.

Sifurahishwi kwa sababu kuna watanzania wengi wana access na station hii na wanahitaji sana michango murua kutoka kwa wabunge machachari wa CHADEMA.

Niwaulize enyi viongozi wa CHADEMA,je mna mgogoro na TBC na nyinyi TBC je mna mgogoro na CHADEMA?Na kama jibu ni ndiyo kwanini msikae mkayamaliza?Hamuwatendei haki watanzania kwa kweli.

Jirekebisheni.

Huenda ulikuwa safarini na pia unakaa mbali na vyombo vinginevyo vya habari isipokuwa TBC na washirika wake. Hii ni kwa sababu CHADEMA walipofanya mkutano wao wa uongozi baada ya rabsha zilizotokana na kuzuiwa kwa mkutano wao na kuuwawa kwa Mwangosi, waliitangaza TBC kama janga la taifa na kutangaza kuisusia rasmi ikiwa ni pamoja na kuwataka wapenzi wake na wananchi kwa ujumla kuisusia. Taarifa hizi zilitolewa na vyombo mbalimbali vya habari, ila sina hakika kama TBC na washirika wake walizitoa. Kwa bahati mbaya, kwa kuwa wewe ni mshirika mzuri wa TBC ndio sababu huenda hukupata nafasi ya kufahamu lililokuwa nje ya box. Kwa msingi huo basi, sitegemei kiongozi yeyote wa CDM kushiriki katika jambo lolote lifanywalo na TBC hadi pale chombo hicho kitakapojirekebisha na kuwa cha kitaifa na sio kipeperushi cha CCM (maneno ya Mbowe).

Bahati mbaya, binafsi nilikuwa sinaga mpango kabisa na TBC kama nisivyojua kama RTD bado ipo hewani (Niliachana navyo tokea maigizo ya Mzee Jongo na Jangala).
 
Mmmmmh!Hii nchi yangu kila kitu siasa sasa.Tutafika kweli?

Kufika ndg yangu 2tafika ila lazima tutakuwa hoi, kunawengine watakuwa hawana mikono, wengne mabubu wengne hawana miguu wengne hawana macho wengne wanalia wengne wanashangaa! Hatuna jinsi tumezaliwa tumejikuta tu wa tz nchi ya kisiasa kila kitu, shule zipo kisiasa, hospital kisiasa, polisi, kisiasa, kilimo kisiasa, amani kisiasa tutafika tu! Mbona watoto wa mitaani hawana walezi lakini wanakua?
 
TBC inaheshimika sana duniani, haipo tayari kumualika mtu kama Mh. Lema ambaye anaonekana wazi kabisa kwamba uwezo wake wa kufikiri ni mdogo na malezi yake ya utotoni hayakuwa mazuri.

Nitakugongea like. Umenigusa hapo kwenye malezi.
 
Huenda ulikuwa safarini na pia unakaa mbali na vyombo vinginevyo vya habari isipokuwa TBC na washirika wake. Hii ni kwa sababu CHADEMA walipofanya mkutano wao wa uongozi baada ya rabsha zilizotokana na kuzuiwa kwa mkutano wao na kuuwawa kwa Mwangosi, waliitangaza TBC kama janga la taifa na kutangaza kuisusia rasmi ikiwa ni pamoja na kuwataka wapenzi wake na wananchi kwa ujumla kuisusia. Taarifa hizi zilitolewa na vyombo mbalimbali vya habari, ila sina hakika kama TBC na washirika wake walizitoa. Kwa bahati mbaya, kwa kuwa wewe ni mshirika mzuri wa TBC ndio sababu huenda hukupata nafasi ya kufahamu lililokuwa nje ya box. Kwa msingi huo basi, sitegemei kiongozi yeyote wa CDM kushiriki katika jambo lolote lifanywalo na TBC hadi pale chombo hicho kitakapojirekebisha na kuwa cha kitaifa na sio kipeperushi cha CCM (maneno ya Mbowe).

Bahati mbaya, binafsi nilikuwa sinaga mpango kabisa na TBC kama nisivyojua kama RTD bado ipo hewani (Niliachana navyo tokea maigizo ya Mzee Jongo na Jangala).
Mmmmmmh..Je kususa ndio solution?Kujirekebisha kwa TBC ni kwa vigezo gani?
Angalizo:Mimi ni mdau wa TBC kwa maana ya mtazamaji tu na mlipa kodi kama watanzania wengine wote sio muajiriwa na wala sina maslahi mengine yoyote either na Tbc or chama chochote cha siasa.
 
TBC imekuwa kama radio ya chama,na haiaminiki kwa sababu imekuwa ikieneza propaganda na kusahau jukumu lake la kuelimisha wananchi.Watu wengi hawaisikilizi siku hizi.
 
TBC NI YA CCM,Na kawaida yao ni lazima waalikane wao wenyewe kujadili na kusifia sera zao wenyewe! Ccm ni tbc na tbc ni ccm
 
Nasikitishwa sana kuona wabunge wa CHADEMA hawashiriki katika mijadala inayoendeshwa na television ya taifa (TBC) hususani vile vipindi vya asubuhi.

Sifurahishwi kwa sababu kuna watanzania wengi wana access na station hii na wanahitaji sana michango murua kutoka kwa wabunge machachari wa CHADEMA.

Niwaulize enyi viongozi wa CHADEMA,je mna mgogoro na TBC na nyinyi TBC je mna mgogoro na CHADEMA?Na kama jibu ni ndiyo kwanini msikae mkayamaliza?Hamuwatendei haki watanzania kwa kweli.

Jirekebisheni.

meli ilizama huku tbc wakionyesha muziki wa taarabu, tbc ambao wanarekebisha mavavi waliyo yavaa wakati vipindi vinaendelea
 
Mkuu siasa za nchi za manyani ni uhadui, kwa hiyo usione ajabu
 
Mkuu Africa wapinzani huwa ni maadui, kwa hiyo usione ajabu CDM kususiwa na TBC. Kimsingi TBC ni nzuri kwa bunge tu
 
TBC inaheshimika sana duniani, haipo tayari kumualika mtu kama Mh. Lema ambaye anaonekana wazi kabisa kwamba uwezo wake wa kufikiri ni mdogo na malezi yake ya utotoni hayakuwa mazuri.
Thibitisha kwamba inaheshimika duniani..vyombo vinavyo heshimika duniani vinatambulika...SABC, CCTV, BBC, RT, CNN, Al Jazeera, Citizen!! Hakuna chombo chochote cha habari ndani ya bongo hii kinajulikana huko nje!!
 
TBC imekuwa kama radio ya chama,na haiaminiki kwa sababu imekuwa ikieneza propaganda na kusahau jukumu lake la kuelimisha wananchi.Watu wengi hawaisikilizi siku hizi.
Tokea TBC wamfukuze kazi Tido Mhando, kwa maagizo ya ofisi ya Lumumba,eti kwa kosa la kuandika balanced stories, hiyo stesheni, badala ya kujiita televisheni ya Taifa, jina ambalo linawastahili ni waitwe TBCCM!!

Haiwezekani TBC wakiwa wanajua kuwa televisheni yao inaendeshwa kwa kodi za wananchi wote, wakiwemo wanachama wa CDM na wa CCM, lakini wanakigeuza chombo hicho cha habari kuwa cha propaganda kwa wanamagamba!!
 
Back
Top Bottom