CHADEMA na Mnyika waongo katika suala la Gesi

CHADEMA na Mnyika waongo katika suala la Gesi

namtumbo

Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
78
Reaction score
102
Chadema wamejitokeza kuhamasisha watu wa Mtwara tusikubali ujenzi wa bomba la gesi. Waziri kivuli wa Nishati na Madini wa Serikali hiyo Mhe Mnyika ametoa matamko ya kuunga mkono hoja za watu wa Mtwara kuhusu kukataa ujenzi wa bomba la gesi. Lakini ni wazi kwamba Chadema hawasemi ukweli,ni vigeugeu, na wadandia hoja kwa ajili ya kutafuta umaarufu wa chapchap.

Ushahidi wangu huu hapa........angalia hansard uone walichosema Bungeni katika taatifa ya kambi rasmi ya upinzani Bungeni....


http://polis.parliament.go.tz/PAMS/docs/HS-8-34-2012.pdf

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani ilitaka kiwango cha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kuongezwa ili vipaumbele vifuatavyo viweze kuzingatiwa kwa uzito unaostahili: Kuwekeza fedha za kutosha kwenye sekta ya umeme na Gesi ili kumaliza kabisa tatizo la nishati ya Umeme na kupunguza gharama za maisha.

Mheshimiwa Spika, hatua hizo ziambatane na kuwekeza katika Bomba la Gesi, pamoja na ujenzi wa mtambo wa kutengeneza Gesi (LPG extraction Plant) ili kuwezesha gesi kutumika kwenye magari, viwandani na majumbani; kuhakikisha tunazalisha 360MW za umeme kila mwaka ili kufikia malengo ya Mpango wa Maendeleo wa miaka Mitano na kumaliza tatizo la mgawo wa umeme na mwisho kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya usafirishaji na usambazaji wa umeme vijijini ili kuchangia katika ukuaji wa uchumi vijijini

Mheshimiwa Spika, mzigo huu usingekuwa mkubwa iwapo Serikali ingetekeleza katika mwaka wa fedha 2011/2012, maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani ya kuhakikisha nyongeza ya fedha kwenye bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa upande wa Sekta Ndogo ya Gesi kwa ajili ya mitambo ya umeme na kuharakisha kuwekeza katika Bomba la Gesi pamoja na ujenzi wa mtambo wa kutengeneza Gesi (LPG extraction Plant). Mheshimiwa Spika, kutokana na hatimaye Serikali kuzindua ujenzi wa bomba la gesi katika mwaka wa fedha 2012/2013 na ahadi ya Wizara ya Nishati na Madini kuwa ujenzi huo utakamilika katika kipindi cha miezi kumi na nane ijayo, Kambi Rasmi ya Upinzani inataka Serikali kutoa kauli ya uhakika kwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, mradi mkubwa wa maendeleo ambao umepangwa katika mwaka wa fedha ni ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es salaam.

ambapo kwenye kasma 3162 umetengewa kiasi cha shilingi 93,000,000,000 huku kiwango kingine cha fedha za mradi huo kikitarajiwa kupatikana kutokana na mkopo kutoka nje. Mheshimiwa Spika, kutokana na unyeti wa mradi huo kwa mustakabali wa nchi na maisha ya wananchi wa sasa na baadaye, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuwasilisha Bungeni na kuweka wazi kwa umma mkataba wa mradi husika ili Bunge liweze kuishauri na kuisimamia Serikali kuanzia katika hatua za awali kuhakikisha kwamba maslahi ya Taifa yanalindwa katika hatua zote na pia wananchi wananufaika kutokana na fursa za uwekezaji


Hivi watu wa wa aina hii wanaoadilisha misimamo kutokana na upepo, watafaa kweli kuongoza nchi?
 
Kwani hapo kosa ni nin? Wajibu wa wabunge ni kusikiliza kilio cha wananchi,mradi uliandaliwa na serikali ya ccm,wananchi wa mtwara inabidi wasikilizwe kwanza. Na kama serikali ingeongozwa na cdm nina uhakika suala hili lingetatulika kwa sera ya majimbo.hakuna chadema walichodanganya hapa,bali bungeni wameshauri mpangowa serikali.
 
Mleta mada labda ungeweka na hiyo kauli yao (cdm) rasmi kuhusu mtwara gas, ili tuweze kudadavua vizuri uongo, ugeugeu na udandaaji hoja wao. Vinginevyo kwa quote hiyo ya hansard huwezi kuwabana hata chembe.
 
Ubongo wa mleta post hii ungekuwa na ukubwa wa peanut size ungetosha kumpa akili ya kujua hoja katika bomba la gesi ni nini!Wana Mtwara is kwamb hawatak bomba lijengwe bali wahakikishiwe wanafaidikaje na hasa kwa ujenzi wa mtambo wa kutengeneza gesi hapo hapo Mtwara.Pia kuimarishwa kwa bandari yao.Halafu bomba ndipo lijengwe.Wasikilize vizuri watu wa Mtwara usitafute ubaya wa CDM dada.
 
Hata kama msimamo wao kabla ilikuwa ni kuwa bomba lijengwe toka mtwara kuja dar,kwa hali ilivyo sasa ni mwendawazimu tu (serikali ya magamba) asingebadili msimamo kuhusu suala hili. Kama watu wamekataa lazma uwasikilize
 
Ni kweli Chadena waongo tu ukisoma maneno ya Mnyika ni tofauti anachosema sasa hivi. Chadema acheni siasa za matukio.
 
Hapo kwenye 'kuweka wazi mkataba husika' ndo maneno iko. Wanamtwara wanataka kujua hatima yao. Watanufaikaje? Sio bomba linaenda dar na mwisho wanajengewa madarasa matatu yasiyo na walimu, ama wodi moja isiyo na vitanda!
 
Ni kweli Chadena waongo tu ukisoma maneno ya Mnyika ni tofauti anachosema sasa hivi. Chadema acheni siasa za matukio.

Ni ushabiki wa kitoto na u.j.i.n.g.a uliopitiliza kila kitu kushabikia bila kutumia hata chembe ya akili kufikiri,matukio ya fujo eg Dumila,Mtwara etc inatokana na wananchi kuamka kifikra na kutambua haki zao,nyie bado mnakumbatia u.j.i.n.g.a na kujiaminisha uongo ndio silaha yenu,tena uongo wa kitoto!paragraph ya mwisho imejitosheleza kuonyesha uwezo wa kufikiri wa mleta mada maana ndio paragraph haswa iliyobeba dhamira nzima aliyokua amedhamiria mleta mada huku akiwa ajijui kua anajiweka uchi kwa kutokua na uwezo wa kuchambua hata masuala madogo kama haya,hii ndio aina ya vijana waliopo C.c.m! "mtu aliyefikia hatua ya kujidanganya hata yeye mwenyewe ni mtu wa kumsikitikia sana" - John Mnyika
 
Mkataba wa mkopo wa ujenzi wa bomba haukuwekwa wazi kama ilivyotakiwa na kambi ya upinzani Bungeni, hivyo ni dhahiri kuna mchezo mchafu sana, mkopo ni mkubwa sana kulinganisha na gharama halisi, hivyo basi, ukijumlisha na riba, faida yote ya Gesi hiyo itaishia kulipa deni, ni sahihi kuwaunga mkono wananchi wa Mtwara wasifanywe kama wa Kahama na dhahabu yao. Sidhani kama CDM wanadandia hoja kwani wao ndio walioianzisha hoja hii ya 'kudai manufaa' kutokana na gesi hiyo mwaka jana wakati wa opereshen M4C kule Mtwara na Lindi.
 
"Mheshimiwa Spika, kutokana na unyeti wa mradi huo kwa mustakabali wa nchi na maisha ya wananchi wa sasa na baadaye, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuwasilisha Bungeni na kuweka wazi kwa umma mkataba wa mradi husika ili Bunge liweze kuishauri na kuisimamia Serikali kuanzia katika hatua za awali kuhakikisha kwamba maslahi ya Taifa yanalindwa katika hatua zote na pia wananchi wananufaika kutokana na fursa za uwekezaji"

hapa uongo uko wapi?
 
"Mheshimiwa Spika, kutokana na unyeti wa mradi huo kwa mustakabali wa nchi na maisha ya wananchi wa sasa na baadaye, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuwasilisha Bungeni na kuweka wazi kwa umma mkataba wa mradi husika ili Bunge liweze kuishauri na kuisimamia Serikali kuanzia katika hatua za awali kuhakikisha kwamba maslahi ya Taifa yanalindwa katika hatua zote na pia wananchi wananufaika kutokana na fursa za uwekezaji"

hapa uongo uko wapi?

labda uwe na kichaa cha mbwa lakin hili lipo wazi kabsaa..labda anaikejeli serikal kwa kujifanya haisikii..
 
Ni kweli Chadena waongo tu ukisoma maneno ya Mnyika ni tofauti anachosema sasa hivi. Chadema acheni siasa za matukio.

CDM hata kama ndo wao wamepanga gesi isafirishwe hata Bukoba wangebadili msimamo kutokana na falsafa ya nguvu ya umma,kwamba wananchi waamue wenyewe mustakabali wa maisha yao,uache uzumbukuku.
 
kwa kweli nillingiwa na ghazabu sana,lakini nilipokuja kuona maneno ya huko chini nikakumbuka kumbe nilishawahi kuiskia hotuba hii na kumwona mnyika kwa macho yangu kipindi anachangia hoja ile,actually ayeye alikuwa anasoma tuh mpango ule uliofanywa na serikali kama ulivoainishwa,ila wao kama chadema mule bungeni walitaka mkataba wauone na usiwe siri kwao ili waweze kuishauri vema serikali,yumkni wangeuona na kuyaona madudu ya humo tusingefika hapa,na wala mradi huo usingetekelezwa,kwa hoja ya majimbo na mustakabali wa matumiz ya rasilimali za taifa chadema wasingeweza kujicontradict katika hilo.
 
Kwani hapo kosa ni nin? Wajibu wa wabunge ni kusikiliza kilio cha wananchi,mradi uliandaliwa na serikali ya ccm,wananchi wa mtwara inabidi wasikilizwe kwanza. Na kama serikali ingeongozwa na cdm nina uhakika suala hili lingetatulika kwa sera ya majimbo.hakuna chadema walichodanganya hapa,bali bungeni wameshauri mpangowa serikali.

Kazi ya chama cha upinzani sio kushauri mipango ya serikali, hata ile ambayo hawaiungi mkono. Chadema wameweza mara kadhaa wameipinga mipango ya serikali ambayo hawakubaliani nayo....walishawahi hata kutoka nje ya Bunge ku protest. Hivyo wewe usitudanganye hapa kwa wameshauri mipango.....wameunga mkono, tena wakashinikiza mradi ukamilishwe haraka. Uzuri hii kitu ipo kwenye hansard...sio umbea wala majungu
 
Back
Top Bottom