Chadema na mbio za mwenge....

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,886
Jamani wale waliotazama tv leo mmeona nchimbi

alivyozungumza kuhusu mbio za mwenge mwaka huu

utasema jambo la maana sana......

sasa najiuliza hivi hizi mbio za mwenge zitapigwa lini
marufuku?????????

hivi sera za vyama vingine hasa CHADEMA kuhusu

hizi mbio za mwenge ni nini?????????

mimi nataka kuona zinapigwa marufuku haraka sana...........
 
Du! sikujua kama mwenge bado unakimbizwa! Nafikiri ungefaa ukumbizwe usiku sioni logic kwa nini kuukimbiza mchana
 
Sijasikia alichosema nchmbi lakini kwa maoni yangu mwenge ni matumizi mabaya ya Fedha na muda kwani hiyo miradi inayofunguliwa, zinduliwa na mwenge ingezinduliwa na madiwani tulio wachagua tu. Sasa utakuta magari zaidi ya 20 (nimeambiwa maana sijaona mifukuzano ya mwenge miaka mingi) yanafukuza,na kuuendesha huo mwenge sio kuukumbiza maana haukimbii. Ushauri ukaweke Makumbusho ya taifa utasomwa na kuangaliwa kama kumbukumbu
 
Kuna watu vijijini wanachangishwa pesa kwa ajili ya huo mwengo

na pia unasambaza ukimwi vijijini...
 
Kuna watu vijijini wanachangishwa pesa kwa ajili ya huo mwengo

na pia unasambaza ukimwi vijijini...
Vijiji? Thubutu hadi kwenye majiji makubwa watu wanachangishwa fano wafanyakazi, makampuni, Teksi, daladala , mahoteli, shule n.k
 
kwa taarifa mwaka huu wananchi wa Mbeya wamechangishwa shilingi milioni 100/= kugharamia mbio za mwenge. Halafu eti serikali imetoa milioni 200/= kwa maana hiyo unagharimu milioni 300/= kwa mkoa wa Mbeya. Hata hivyo umeahirishwa kuwashiwa Mbeya wakati wananchi weshachangishwa. Hivi wataalamu wa uchumi mtusaidie, hizo milioni 300/= zingefanya yepi ya maana zaidi?
 
Back
Top Bottom