Chadema na Mazagazaga ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema na Mazagazaga ya CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kibunango, Nov 11, 2008.

 1. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  2008-11-10 13:48:03
  Na Mashaka Mgeta


  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimezidi kukitesa Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kuwachukua wanachama wake kadhaa ambao ni wafanyabiashara maarufu wa wilayani Tarime, Mkoa wa Mara wanaoishi jijini Dar es Salaam.

  Kuhama kwa wafanyabiashara hao, kumefanyika wakati kampeni ya operesheni sangara, ikipangwa kuendelea kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria.

  Hatua hiyo ilifikiwa juzi jioni, katika hafla iliyoandaliwa nyumbani kwa mmoja wa matajiri hao, Chacha Kigula, Mikocheni na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, akiwemo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge mpya wa Tarime, Charles Mwera.

  Awali, hafla hiyo ilitangazwa kuwa mahususi kwa ajili ya kumpongeza Mwera, ambaye pamoja na Diwani wa kata ya Tarime Mjini (Chadema), John Heche, walishinda katika uchaguzi mdogo uliofanyika jimboni Tarime Oktoba 12, mwaka huu.

  Katika hafla hiyo, pamoja na Kigula, wafanyabiashara matajiri wengine waliojitokeza hadharani na kuchukua kadi za Chadema walizokabidhiwa na Mbowe, ni Mosama Mwita na James Binagi.

  ``Wapo waliochukua kadi lakini hawakupenda majina yao kujulikana, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo usalama mahali pa kazi,`` alisema msemaji wa Chadema wilayani Tarime, Chacha Daniel Okong`o.

  Okong`o, alisema watu wengine zaidi ya 20 wa kada tofauti, waliokuwa miongoni mwa washiriki katika hafla hiyo, walijiondoa katika vyama vyao na kujiunga Chadema.

  Akizungumza na Nipashe, Mwita alisema walifikia uamuzi wa kuachana na CCM ili kukidhi mwelekeo wa siasa na mwitikio wa wananchi wa Wilaya ya Tarime.

  Aidha, Mwita alisema tukio hilo ni sehemu ya ishara ya kuonyesha msimamo wa dhahiri kisiasa uliopo kwa wananchi wa Tarime.

  ``Sisi tulichangia kuwahamasisha vijana kutambua na kutetea haki zao, sasa tusingeeleweka kama tungeamua kuwa nje,`` alisema.

  Naye Kigula, aliwaambia washiriki wa hafla hiyo kwamba CCM imeelekea kupoteza mwelekeo katika uongozi, hivyo njia pekee ni kupata chama mbadala kitakachochukua dhamana hiyo.

  ``Kama ningekuwa bado kijana kama wewe Mbowe, ninaamini kwamba ingekuwa rahisi sana kuichukua nchi hii, CCM wameshindwa kuongoza,`` alisema.

  Kigula alisema viongozi na wabunge wa CCM, wameshindwa kutambua vipaumbele vya mahitaji na maendeleo ya wananchi, badala yake wanajihusisha na mambo yasiyoleta tija kwa umma.

  Alitoa mfano kuwa, baadhi yao wanapopata uongozi, wanafikiria kujiimarisha madarakani kwa njia za kishirikina, hali inayowafanya waelekeze rasilimali na mbinu zao katika eneo hilo badala ya kuwafikiria wananchi waliowachagua.

  Mbowe alisema kujiunga kwa wafanyabiashara hao, kutachochea ari ya mageuzi kwa wananchi ndani na nje ya Tarime.

  Alisema hivi sasa Tarime ni eneo linalotolewa mfano wa kuigwa kwa jamii inayohitaji mageuzi ya kweli ndani na nje ya Tanzania.

  Hata hivyo, alitahadharisha kuwa hatua ya watu kukihama chama kimoja na kujiunga katika chama kingine, isichukuliwe kama asili ya uhasama unaoweza kusababisha chuki miongoni mwa wananchi.

  ``Leo hii mmeiona CCM haiwafai, mmejiunga Chadema, hilo ni jambo jema kwa maana vyama vinatakiwa kujenga mazingira ya kukubalika kwa wananchi, kitu ambacho kinatukabili hata sisi huku Chadema,`` alisema Mbowe.

  Wakati huo huo, taarifa zilizopatiakana jana kutoka Makao Makuu ya Chadema zilieleza kuwa operesheni sangara iliyoanza baada ya uchaguzi mdogo wa Tarime, inaendelea wiki hii mkoani Mwanza.

  SOURCE: NIPASHE
   
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mmmm.. TONE NA TONE HUJAZA NDOO... GO ON CHADEMA!
   
 3. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu KIgula hajui what lays ahead of him!I have a living example ya tajiri mmoja Arusha wa Kimasai ambaye alikuwa na kiherehere cha kuunga mkono upinzani ila alikwama kwenye shughuli zake mpaka akarudi CCM.Hope he knows whats good for him heri ya hao walioomba identinty zao zifichwe!
   
 4. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu mimi nawasifu waliojitokeza hadharani kwa kuwa hakuna siri kujiunga na chama cha siasa.
  Mamluki lazima walikuwepo walishatoa taarifa sasa kwa nini kuwa kifichoni.

  Pia sisiem ya leo si ile kama ya miaka ya nyuma.Kila mtu ana lake

  Ni kweli kabisa Ukiwahama miaka ya nyuma ilikuwa taabu,waliwahi kuwasumbua wafanyabiashara wawili maarufu pale Mwanza na mmojawapo alikuwa mmliki wa hotel ya pale ziwani ya ROCK BEACH HOTEL hadi akachizi,na mwingine Mchaga aliyemsapoti mrema akalazimishwa kukana hadharani mkutanoni kwa kurudisha kadi.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Acha wajitangaze kwa sababu wakisakamwa katika biashara zao ndio tutapata mfano mwingine wa jinsi mamlaka zinavyoendesha mambo kisiasa. Nao (wafanyabiashara watakaosakamwa) watakuwa wameshafanya sehemu yao ya kazi ya ujenzi wa demokrasia na wachacharikaji watakuwa na hoja za kubamiza
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Walipokuwa CCM ilikuwa ni rahisi kuwaita Mafisadi...! Sasa wakiwa Chadema wataitwa vipi?

  Labda mafisadi viwembe...!
   
 7. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Cowards die many times before their real deaths.Courage is not an absence of fear but a judgement that something is better than fear!
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kibunango si kila tajiri ni Fisadi hapana .Kuna watu wana pesa ya kutolea jasho na hao ndiyo wana diriki kujitoa CCM maana hawana uoga wa kushitakiwa .Naamini tuwe katika msitari hu kwa sasa .
   
 9. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #9
  Nov 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Watanzania hawana tena haja ya kuwa na hofu kujiunga na vyama vya siasa. Uoga huo ndio uliojenga ufisadi kiasi kikubwa ndani ya ccm. Uoga ulijengwa na serikali ya Mkapa kutokana nae kuingia ikulu kwa mbinde na akawa na shaka kuwa mambo yangeweza kubadilika wakati wowote, walibinya kweli wananchi hadi wakulima waliochagua upinzani siku za mwanzo. Lakini leo, kila mtu anafahamu kiasi kikubwa nini ni haki. Leo utakimbilia wapi? hata ukijificha nadni ya ccm, utapataje kupona? leo wote wanaosakamwa na wenye kashfa nyingi ni walio ndani ya ccm! Hii ina maana kuwa kinachofanyika sasa ni kujenga misingi mipya inayokubalika na jamii na siyo ile ya kusukumiza kama walivyofanya kina Sumaye kwa kuwaambia wafanyabiashara kuwa kama wanahitaji kushamiri lazima wafanye hivyo wakiwa ndani ya ccm.

  Tupo karne mpya, sasa mwendo ni mdundo, tunapingana kwa hoja na sera tu!
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Awali ya yote tunaambiwa kuwa matajiri wengi hutumia chama tawala kwa faida zao binafsi, hivyo matajiri wana uwalakin na sio safi hata kidogo, kwani wamepitia CCM.

  Ukisoma vizuri taarifa hiyo, ni wachache ambao wamekubali kutajwa kwa majina yao kwamba wanahama CCM, hapana shaka wana uhakika na utajiri wao. Je wale ambao wameogopa kutajwa majina yao hawana harufu ya kifisadi kweli?
   
 11. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #11
  Nov 11, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Neno mazagazaga lina matumizi maalumu kwa wakazi wa mpakani (kati ya kenya na tanzania) upande wa Tarime. Matumizi ya mazagazaga hapa yanamaanisha ipi?
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  Nov 11, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Katika mada hii lina maana ya second hand products....
   
 13. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #13
  Nov 11, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Okay,

  Asante kwa ufafanuzi
   
 14. M

  Mama JF-Expert Member

  #14
  Nov 11, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  ha ha ha ha haa, umepinda wewe?!
   
 15. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #15
  Nov 12, 2008
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nasikitika kuwa kauli hii hainiingii akilini. Kumbukeni kuwa wale wote walioko CHADEMA waliingia wakiwa na fresh mind, attitude, and political ambition. Kuwaita second hand product (mazagazaga) hakumaanishi ukweli wa watu wenyewe.
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Nov 12, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hawa wa kwenye mada hii walikuwa wakiifadhili CCM, kabla ya kujiunga na Chadema... Sasa hawa wana sifa yoyote ya kuwa na fresh minds attitude n.k?

  Tena wengine wakiitwa Mafisadi walipokuwa huko CCM..
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Nov 12, 2008
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Kibunango hiyo imetulia ..Siasa za kujificha zimepitwa na wakati .
  Go!!! On Chadema
   
 18. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #18
  Nov 12, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  this article is slightly hyperbolic.
   
 19. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #19
  Nov 12, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  ^Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Nov 12, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wameogopa kutajwa kwa sababu zile zile zinazotufanya tusitaje majina yetu hapa.
  Siku ukiacha kuitwa Kibunango, nakutumia jina lako halisi ndipo na wewe kaharufu hako katakuwa mbali nawe rafiki?
  Siamini kila ambaye hataki kutaja jina lake ni fisadi. Wengine wana sababu za muhimu kabisa ambazo wakizisema hata sisi tutakubali kwamba si vema wazitaje.
  Wengine ndio wanaotuletea dataz hapa sasa wakitajwa hapo si tumepunguza link?.
   
Loading...