funaku
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 39,119
- 31,640
Mimi nadhani muuliza swali alijichanganya mwenyewe,kujiunga na chama na mgongano wa maslahi kikazi ni vitu viwili tofauti,ndio maana naona uwezo wa wabunge wetu wa kuelewa mambo mle mjengoni ni mdogo,yeye alitakiwa amuulize tu kwa kifupi Dr Tulia je kwa kuwa yeye ni mwajiriwa wa serikali ni lini kajiuzuru nafasi ya Naibu mwanasheria mkuu?ikumbukwe huyu mgombea unaibu spika kateuliwa kuwa mbunge na hivi juzi sasa yeye ndie angesema kama ameandika barua ya kuacha unaibu mwanasheria wa serikali tarehe fulani kabla ya kwenda kuomba unaibu spika,sasa hata kabla hajajibu tayari waheshimiwa wa upinzani wakaanza makelele ,huo ni ujinga wamepoteza fursa ya kumsikiliza,hata mwizi naye anasikilizwa huko mahakamani,nao wabunge wanatakiwa wawe na hekima ni mfano mbaya kwa watu ambao tunatarajia mabadiliko.Kaka, kwenye mambo yanayohitaji uelewa uwe unakaa mbali. Unajidhalilisha na kujianika kama mwenye umri mkubwa lakini akili ndogo. Pale, paliulizwa suala la mgongano wa kimaslahi kwa maana ya kuwa mtumishi wa serikali kwa ngazi ya Naibu Mwanasheria Mkuu hakutarajiwa kujihusisha na siasa kwakuwa alikuwa mtumishi wa wote.
‪- Lowassa‬ aliingia CHADEMA saa mbili kamili Asubuhi, ilipofika saa mbili na dakika tano akawa mgombea Urais wa# CHADEMA.....
,Babu ‪#‎Duni‬ aliingia chadema saa sita na saa sita na nusu alikua mgombea Mwenza na Wote waliingia CHADEMA Wiki Moja kabla ya Kampeni kuanza,
- Leo CHADEMA wanamuuliza Dr ‪#‎Tulia‬ Bungeni alijiunga CCM lini? haya ni maajabu ya Musa!!,
KUMBE MZEE MKAPA ANA AKILI SANA, ALISHAWAJUA SIKU NYINGI SANA!!
Le Mutuz Nation
Akili yako haifanyi kazi vizuri unahitaji Psychology consultation inaonekana ubongo umeganda kutokana na kutawaliwa kwa muda mrefu.
Duni na Lowasa hawakuwa watumishi wa Serikali cha kushangaza huyu Tulia alikuwa ni mtu anayetakiwa kutetea masilahi ya Umma si chama. Lakini yeye alikuwa mwanachama wa chama fulani.
Tunakuwaje na imani na mtu kama huyo wakati mwingine hata akiongea jambo la maaana sana?
Majibu ya DR. Tulia ni haya hapa!
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA YA MWAKA 1977
67-(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa
kuwa Mbunge-
(g) ikiwa mtu huyo ameshika madaraka ya afisa
mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais aweza
au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa mujibu wa
Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge;
72. Iwapo mtu yeyote mwenye madaraka katika utumishi wa
Serikali, madaraka ya aina iliyotajwa katika ibara ya 67(2)(g)
ataamua:-
(a) kuwa mgombea uchaguzi wa Rais au wa nafasi
nyingine yoyote chini ya Katiba hii;
(b) kugombea uongozi wa ngazi yoyote katika chama cha
siasa kinyume na masharti ya ajira,
mtu huyo atahesabiwa kuwa utumishi wake umekoma tangu
tarehe yake ya kuwa mgombea uchaguzi au ya kugombea
uongozi katika chama cha siasa.
wagogo akili zenu mbovu sana.ndo maana milembe ikajengwa dodoma.yaani we ni jamii ya dinnosaurs.mwili mkubwa akili pilton
CHADEMA wanamuogopa sana Dkt Tulia. Kitendo cha wao kumnyima nafasi kuongea ni ushahidi tosha kuwa wanamuogopa vibaya sana.
Maana Dkt Tulia naibu wetu wa spika anasema kwa vifungu...anasema kwa kutaja Ibara...bila kusoma mahali popote pale...mtu wa namna hiyo ni moto wa kuotea mbali! Jitu kama Lissu bila kuwa na katiba...haliwezi kutaja Ibara yoyote ile mpaka asome. Tofauti kabisa na Dr Tulia. Vitu vipo kichwani tu.
Asante Mungu kwa kutupa naibu spika msomi.
Ni kweli maana tumeona wakati akijieleza hakusoma mahali.CHADEMA wanamuogopa sana Dkt Tulia. Kitendo cha wao kumnyima nafasi kuongea ni ushahidi tosha kuwa wanamuogopa vibaya sana.
Maana Dkt Tulia naibu wetu wa spika anasema kwa vifungu...anasema kwa kutaja Ibara...bila kusoma mahali popote pale...mtu wa namna hiyo ni moto wa kuotea mbali! Jitu kama Lissu bila kuwa na katiba...haliwezi kutaja Ibara yoyote ile mpaka asome. Tofauti kabisa na Dr Tulia. Vitu vipo kichwani tu.
Asante Mungu kwa kutupa naibu spika msomi.
Hapa mngekuwa mnatuelimisha wajamani maana wengine hapa tunataka kusikia kitu kutoka kwa waelewa wa huu waraka wa utumishi wa Umma una apply vipi maana huku uraiani watumishi kibao katika ngazi za chini wana hamu kushiriki hata kwenye Udiwani lakini wengine wanaogopa au wanashindwa kupambambanua
Hakujiuzulu bali uteuzi wake ulitenguliwa na Rais. Utakuwa wa ajabu kuuliza hivyo ulivyosema wakati inafahamika kilichotokea!Mimi nadhani muuliza swali alijichanganya mwenyewe,kujiunga na chama na mgongano wa maslahi kikazi ni vitu viwili tofauti,ndio maana naona uwezo wa wabunge wetu wa kuelewa mambo mle mjengoni ni mdogo,yeye alitakiwa amuulize tu kwa kifupi Dr Tulia je kwa kuwa yeye ni mwajiriwa wa serikali ni lini kajiuzuru nafasi ya Naibu mwanasheria mkuu?ikumbukwe huyu mgombea unaibu spika kateuliwa kuwa mbunge na hivi juzi sasa yeye ndie angesema kama ameandika barua ya kuacha unaibu mwanasheria wa serikali tarehe fulani kabla ya kwenda kuomba unaibu spika,sasa hata kabla hajajibu tayari waheshimiwa wa upinzani wakaanza makelele ,huo ni ujinga wamepoteza fursa ya kumsikiliza,hata mwizi naye anasikilizwa huko mahakamani,nao wabunge wanatakiwa wawe na hekima ni mfano mbaya kwa watu ambao tunatarajia mabadiliko.