CHADEMA na Lowassa kwa Ushindi huu wa Raila Odinga mtaweka wapi sura zenu?

Aibu Mi nahama Chadema
Uhuru aliungwa mkono pekee kama mgombea. Ndio maana mahakama ilimsafisha kuwa hana hatia katika kesi hii. Mwenye hatia ni IEBC kutokuendesha uchaguzi kwa kufuata katiba. IEBC wamelitia taifa la Kenya hasara na nadhani hata Uhuru mwenyewe atawawajibisha. Kumuunga mkono mgombea tarajia mawili; kushinda au kushindwa na unapostahimili hili na kushindwa, wewe ni jasiri. Kuhama ni woga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lowasa na chadema wataficha wapi sura zao baada ya Uhuru kufutiwa matokeo??

Hii haitaleta tafsiri ya kwamba Chadema walimuunga mkono uhuru ili kumfundisha wizi wa kura??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikuelewi, mimi nilichofurahia ni katiba ya Kenya. Mahakama kuwa na uhuru wa kuhoji na kutengua uchaguzi wa Rais, mimi ni Chadema lakini kwa katiba ile atakayepita nitamkubali.
Kwani kuwa Chadema ndio nini? Unaweza ukawa Chadema mchana, usiku ccm.
Siasa ni mchezo wa kubadilisha gia angani,
 
Mahakama ya juu(Supreme Court) imetoa maamuzi ambayo yamebatilisha matokeo ambayo yalimpa Ushindi ya kiti cha Urais Bwana Uhuru Kenyatta pale Agosti 8 mwaka huu.

Ikumbukwe kwamba chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Mwenyekiti wake Freeman Mbowe walitangaza kumuunga mkono Bwana Uhuru Kenyatta katika uchaguzi huo.

Hiyo ilishangaza watu kwani kwa mara ya kwanza chama cha upinzani kiliunga mkono chama tawala kushinda uchaguzi.

Baada ya hapo tulimshuhudia Mjumbe wa kamati kuu ya chadema lowassa akajipeleka nchini Kenya akapanda jukwaani kumnadi Bwana Uhuru Kenyatta.

Baada ya matokeo ya uchaguzi viongozi na wanachama wa chadema walifurahia sana baada ya Uhuru kushinda uchaguzi na wakasema eti Kenya kuna demokrasia na uchaguzu ulikua wa huru na haki.

Sasa kwa maamuzi haya ya leo ambayo mahakama imegundua kasoro nyingi ambazo ziliufanya uchaguzi ule wa tarehe 8 Agost usiwe huru na haki,sijui lowaasa na chadema yote wataziweka wapi sura zao kwani hii ni habari mbaya kwao .

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani raila katangazwa mshindi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nuksi, hii nuksi sasa!
Ukiwa na nyota ya kukatwa unaambikiza hata wenzako wakatwe. Ona sasa Uhuru kakatwa na supreme court.
image.jpeg
 
Ushabiki wa SIMBA na YANGA umeingia hadi siasani, ujinga na wajinga ni wengi mno nchi hii.

Kenya ni nchi ya kwanza/au moja ya nchi za mwanzo kabisa ku-practice democracy, hili haliwezi kutokea Tanzania chini ya hawa viongozi wetu waliopo, iwe chama tawala au upinzani, tupo na very mediocre leaders, wachumia tumbo na wasio na sifa ya kuwa viongozi wa vyama.

Binafsi naamini hata uwezo wa fikra wakenya wamepewa kutuzidi watanzania.

Hongereni sana watu wa Jamhuri ya Kenya.
 
Mahakama ya juu(Supreme Court) imetoa maamuzi ambayo yamebatilisha matokeo ambayo yalimpa Ushindi ya kiti cha Urais Bwana Uhuru Kenyatta pale Agosti 8 mwaka huu.

Ikumbukwe kwamba chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Mwenyekiti wake Freeman Mbowe walitangaza kumuunga mkono Bwana Uhuru Kenyatta katika uchaguzi huo.

Hiyo ilishangaza watu kwani kwa mara ya kwanza chama cha upinzani kiliunga mkono chama tawala kushinda uchaguzi.

Baada ya hapo tulimshuhudia Mjumbe wa kamati kuu ya chadema lowassa akajipeleka nchini Kenya akapanda jukwaani kumnadi Bwana Uhuru Kenyatta.

Baada ya matokeo ya uchaguzi viongozi na wanachama wa chadema walifurahia sana baada ya Uhuru kushinda uchaguzi na wakasema eti Kenya kuna demokrasia na uchaguzu ulikua wa huru na haki.

Sasa kwa maamuzi haya ya leo ambayo mahakama imegundua kasoro nyingi ambazo ziliufanya uchaguzi ule wa tarehe 8 Agost usiwe huru na haki,sijui lowaasa na chadema yote wataziweka wapi sura zao kwani hii ni habari mbaya kwao .

Sent using Jamii Forums mobile app
soma hapa chini mkuu...
Mh. Tundu Lissu alonga mambo mhimu na makubwa juu ya yaliyotokea Kenya
 
Back
Top Bottom